Sunday 22 March 2015

Mo Farah ashinda mbio za Lisbon Marathoni



LISBON, Ureno
BINGWA mara mbili wa Olimpiki Mo Farah ameshinda mbio za nusu marathoni za Lisbon na kuweka rekodi ya muda bora kwa Ulaya, na kuwa Muingereza wa kwanza kukimbia mbio hizo chini ya dakika 60.
 
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 31 alishinda mbio hizo za maili 13.1 kwa kutumia dakika 59 na sekunde 32, na kuvunja rekodi iliyowekwa miaka 14 kwa sekunde 20 na Mhispania Fabian Roncero.

Farah, pia ndiye bingwa wa dunia wa mbio za mita 5,000 na 10,000m, `akimchapa Mkenya Micah Kogo.

Rekodi ya dunia ya 58:23 iliwekwa na mwanariadha wa Eritrea Zersenay Tadese katika mashindano ya mwaka 2010 yaliyofanyika Lisbon.

Mkenya Kogo, mshindi wa medali ya shaba wa mbio za mita 10,000 kutoka katika Olimpiki ya Beijing mwaka 2008, alikuwa mmoja wa watu sita walishiriki mbio hizo na Farah wakiwa na rekodi ya kukimbi chini ya dakika 60 kwa umbali huo.

Pia kulikuwa na mafanikio kwa Muingereza David Weir aliyeshiriki katika mbio za `wheelchairna Shelly Woods ambaye anaendelea kujiandaa kwa mbio za mwezi ujao za London Marathon.

Weir alimshinda mpinzani wake Mswis Marcel Hug, ambapo mshindi aliamriwa kwa picha au `photo-finish wakati Woods alifanya kweli dhidi ya mpinzani wake Muingereza Jade Jones.

No comments:

Post a Comment