Saturday, 21 March 2015

Mchumba wa de Gea akana kuponda jiji la ManchesterLONDON, England
MCHUMBA wa kipa wa Manchester United David de Gea Edurne Garcia amekana madai kuwa Manchester sio mahali pazuri pakukaa, akisisitiza kuwa, maneno hayo aliwekewa mdomoni na vyombo vya habari.

Uvumi kuwa De Gea yuko mbioni kuondoka Manchester United ulizagaa mapema mwezi huu wakati wa mahojiano ya Garcia, aliyedaiwa kutangaza kuwa hapendi kuishi katika jiji hilo.
'Sio mahali pazuri sana, huo ndio ukweli,' anasema Garcia akijibu madai ya mtangazaji.

Lakini sasa, muimbaji huyo, atakayeliwakilisha Hispania katika shindano la kuimba, alisisitiza kuwa maneno yake yalibadilishwa.

'Sijui kama walikuwa wakisaka habari au walitaka kuleta utata, lakini ilinishangaza mimi wakati nilipoona sentensi hiyo kila mahali ambayo kamwe si kuisema. Nafurahishwa na Manchester, naipenda, na ni mji wa aina yake.'
 
Siku mbili baada ya mahojiano Meya wa Halimashauri ya Jijini la Manchester Pat Karney alimkaribisha Garcia katika ziara ya kuzunguka jiji ili kuona hali halisi.

Garcia anakiri kuwa amefurahi kuzungushwa katika jiji hilo.

No comments:

Post a Comment