Saturday, 21 March 2015

Ibrahimovic apiga `hat-trick' PSG ikishika uongoziPARIS, Ufaransa
MCHEZAJI Zlatan Ibrahimovic alifunga mabao matatu pekee yake `hat-trick wakati Paris St-Germain ikiifunga Lorient 3-1 na kushika uongozi wa Ligue 1.

Msweden huyo  alifunga penati mapema baada ya kufanyiwa madhambi na kipa wa timu pinzani Benjamin Lecomte.

PSG ilitawala mchezo huo na bado ilikosa nafasi kadhaa kabla Jordan Ayew hajasawazisha kwa shuti la umbali wa kama mita 20 na muda mfupi baadae alikosa bao baada ya shuti lake kuzuiwa.

Lakini Ibrahimovic alifunga la pili kwa penati baada ya kuchezewa vibaya na Javier Pastore na dakika za majeruhi alipachika bao la tatu.

Mshambulijai huyo hivi karibuni alikuwa anawekwa benchi kimakosa. Wiki iliyopitaalitolewa nje walipocheza dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, hivyo amefungiwa mchezo mmoja na atakosa mechi dhidi ya Barcelona.
 Lakini uongozi huo wa PSG unaweza kuwa ni wa muda tu endapo Lyon iliyokuwa ikikalia kiti hicho leo Jumamosi itaibuka na ushindi dhidi ya Nice.

No comments:

Post a Comment