![]() |
Diego Costa akichuana na beki wazamani wa Chelsea David Luiz wakati timuhizo zilipochuana. |
LONDON, England
KOCHA wa Chelsea Jose
Mourinho amesema kuwa wachezaji wake hawakuweza kabisa kubadili akili yao na
kucheza na mazingira wakati timu yao ikitolewa katika hatua ya 16 ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya na Paris St-German iliyokuwa na wachezaji 10.
Mabingwa hao wa
Ufaransa mara mbili walitoka nyuma katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja
wa Stamford Bridge na kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.
"Mchezo wetu
haukuwa mzuri kabisa," alisema Mourinho. "Wapinzani wetu walikuwa
bora zaidi yetu, waliendana na shinikizo la mchezo.
"Tulijaribu
kushinda lakini kipindi wakati wamebaki wachezaji 10 tulihisi shinikizo zaidi."
Aliongeza:
"Paris St-Germain walistahili kushinda. Wakati timu haiwezi kuzuia kona
mbili na kuruhusu magoli mawili ya kona hatukustahili kushinda."
Wageni walicheza saa
moja ya muda wa kawaida na dakika 30 za nyongeza wakiwa bila ya mshambuliaji
wake Zlatan Ibrahimovic baada ya mchezaji huyo kutolewa nje baada ya kumchezea
vibaya Oscar.
Lakini, kufuatia
sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza huko Paris, bao la kichwa la Thiago Silva
limewawezesha kufuzu kwa faida ya bao la ugenini na kufanikiwa kulipa kisasi
chamsimu uliopita walipotolewa na Chelsea katika robo fainali.
"Wanasababu
ya kushangilia na niliwaambia wachezaji wangu baada ya mchezo nilipiga meza na
kiti na milango, lakini ni muda wa kutulia na kuchambua kama timu, “alisema
Mourinho.
No comments:
Post a Comment