![]() | |
Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania, Suleiman Nyambui. |
Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya mkutano maalum wa kujadili mabadiliko ya Katiba ya
Riadha Tanzania (RT) utakaofanyika mjini Morogoro Aprili 14, yamepamba moto.
Katibu Mkuu wa RT Suleiman Nyambui alisema kuwa, maandalizi ya
mkutano huo yamefikia pazuri na utafanyikia katika hoteli ya Nane Nane
ulipofanyikia ule wa mwaka juzi.
Awali, mkutano huo ulifanyika mwaka juzi, lakini uliahirishwa baada
ya wajumbe wengi kudai kuwa walichelewa kupelekea nakala ya rasimu hiyo ya
Katiba.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Dioniz Malinzi
ndiye aliyesimamia mkutano huo na kuamuru uahirishwe ili kutoa muda zaidi kwa
wajumbe kupitia nakala hizo.
Nyambui alisema kuwa nakala hizo walizituma mapena na akishangaa
kuona wajumbe wakidai kuwa walichelewa kupelekewa.
Alisema kuwa ni matarajio yake kuwa mkutano wa mwaka huu utakwenda
vizuri na hatarajii kusikia yeyote akidai kuwa hana au amechelewa kupata nakala
hiyo, kwani waliondoka nazo katika mkutano uliotangulia.
“Mkutano wa
mwaka huu utakwenda vizuri na sitatarajii mjumbe yeyote kudai hajapata au
amechelewa kutumiwa nakala hiyo ya rasimu ya Katiba wakati kila mmoja aliondoka
nayo wakati wa mkutano uliopita, “alisema
Nyambui.
No comments:
Post a Comment