Thursday, 5 March 2015

Papiss Cisse afungiwa mechi sabaLONDON, England
PAPISS CISSE (pichani), amefungiwa kucheza mechi saba baada ya kuwa sehemu ya kutemeana mate ambayo pia ilimuhusisha beki wa Manchester United Jonny Evans.

Evans mwenyewe huenda akakabiliwa na kifungo cha mechi sita endapo atapatikana na hatia baada ya Chama cha Soka England (FA) kuwafungulia mashtaka wachezaji wote wawili.

Tukio hilo lilitokea wakati Man United wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu wakati wawili hao walipotemeana baada ya kutokea kutoelewana katika kipindi cha kwanza.

Wote Cisse ambaye ni mshambuliaji wa Newcastle, aliyekubali shitaka lake, na Evans walitoa taarifa Alhamisi ambazo zinakataa kutenda kosa hilo.

Evans alidai kuwa alishtushwa na madai hayo na alipinga. Cisse alijibu kwa kuomba msamaha lakini alisema alichokozwa wakati Evas alipomtemea mate.

MECHI AMBAZO CISSE ATAZIKOSA...

Everton (ugenini), Machi 15

Arsenal (nyumbani), Machi 21

Sunderland (ugenini),Aprili 5

Liverpool (ugenini), Aprili 13

Tottenham (nyumbani), Aprili 19

Swansea (nyumbani), Aprili 25

Leicester (ugenini), Mei 2

No comments:

Post a Comment