Saturday 21 March 2015

Yanga piga Mgambo Shooting hao Mkwakwani



 *Simba wenyewe kushuka dimbani kesho

Na Mwandishi Wetu
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo huku vigogo Yanga wakishuka dimbani kucheza na Mgambo Shooting ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.

Mgambo Shooting hivi karibuni iliitoa nishai Simba kwa kuichapa 2-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.

Wakati Simba ikilambishwa mchanganya Tanga, wenzao Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar na hivyo kukalia kiti cha uongozi.

Yanga leo wanakumbana na mkali huyo wa Simba, Mgambo Shooting kwenye uwanja huo wa Mkwakwani, ambako Simba haikutoka salama.

Yanga iliondoka jijini Dar es Salaam juzi baada ya baada ya ushindi dhidi ya Kagera Sugar ambao umeifanya iongoze ligi kwa kuwa na pointi 34 baada ya mechi 17.

Mgambo imekuwa ikizisimbua timu kubwa inapokutana nazo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kama Simba, Azam FC na Simba.

Yanga haijawahi kupata ushindi kwenye uwanja huo dhidi ya
Mgambo Shooting, lakini leo itabidi kupigana kwa nguvu kuhakikisha inaoondoka na pointi zote tatu ili kuendelea kuwa kileleni.

Kocha wa Mgambo Bakari Shime amesema kuwa Yanga wajiandae kunyolewa leo na hilo halina ubishi na wasifikiri kama wanaweza kutoka.

Mgambo Shooting wana pointi 24 katika nafasi yao ya tano katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 14.

Huko Mtwara; Ndanda FC wataikaribisha JKT Ruvu katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika mchezo wa kwanza JKT Ruvu ilishinda 2-0.

Nayo Stand United ya Shinyanga itakuwa kwenye uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya ikicheza na Kagera Sugar huku Mtibwa Sugar ambao hawafanyi vizuri sasa watakuwa kwenye uwanaja wa Kambarage Shinyanga kucheza na Stand United.

Kesho; Simba ya jijini Dar es Salaam itacheza na Ruvu Shooting wakati Coastal Union itawaalika Azam FC huku
Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Polisi Morogoro ambayo hivikaribuni ilimtimua kocha wake Rishard Adolf.

Msimamo:
                     MP  W   D   L   GF  GA  +/- Pts
    1.Yanga          17  10  4   3   23  10  13  34 
    2.Azam           17  9   6   2   24  12  12  33 
    3.Simba SC       19  7   8   4   22  14  8   29 
    4.Kagera Sugar   19  6   7   6   16  17  -1  25 
    5.Coastal Union  19  5   9   5   14  13  1   24 
    6.Mgambo JKT     18  7   3   8   13  17  -4  24 
    7.Mtibwa Sugar   18  5   8   5   18  18  0   23 
    8.JKT Ruvu       18  6   5   7   15  16  -1  23 
    9.Mbeya City     19  5   8   6   14  16  -2  23 
    10.Ruvu Shooting 19  5   8   6   13  15  -2  23 
    11.Ndanda        19  6   4   9   17  23  -6  22 
    12.Stand United  19  5   6   8   16  23  -7  21 
    13.Polisi Moro   19  4   8   7   13  17  -4  20 
    14.Prisons       18  2   10  6   13  20  -7  16 

No comments:

Post a Comment