NIAMEY, Niger
MALI imetawazwa
kuwa mabingwa wa Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya
kuifunga Afrika Kusini kwa bao 2-0 katika fainali iliyofanyika jijini hapa.
Mabao ya kipindi
cha pili yaliyowekwa kimiania na Siaka Bagayoko na Aly Malle yaliiwezesha Mali
kutwaa taji hilo.
Hii ni mara ya
kwanza katika historia ya Mali timu yake ya vijana inayojulikana kama Eaglets kushinda
taji la mashindano ya vijana.
Awali, nchi hiyo
ilikaribia kushinda taji mwaka 1997, wakati ilipomaliza ya pili nyuma ya washindi
Botswana.
Timu zote Mali na
Afrika Kusini zilienda katika fainali hiyo ya Jumapili zikiwa tayari zimewahi
kukutana katika hatua ya makundi ya mashindano hayo, wakati Afrika Kusini ikiwa
nyuma kwa bao 2-0 na kulazimisha sare ya 2-2.
Hatahivyo, Mali haikuruhusu
hilo utokea tena, na kuhakikisha inaweka ulinzi mkali baada ya kupata bao la
kuongoza na kuhakikisha inaibuka na ushindi.
Bao lao la kwanza
lilipatikana baada ya dakika 67 wakati Bagayoko alipofunga kwa kichwa mpira wa
kona.
The Eaglets waliongeza
bao la pili zikiwa zimebaki dakika 12 kufuatia juhudi binafsi ya Aly Malle. Bao
hilo alilifunga kutoka umbali wa kama mita 20 kutoka nje ya boksi na kuibua
furaha kwa mashabiki wao.
Afrika Kusini
walifikiri wangeweza kupata bao la kufutia machozi wakati Khanyisa Eric Mayo alipokaribia
kufunga, lakini alijikuta akiwa ameotea.
No comments:
Post a Comment