Sunday, 22 March 2015

Wanafunzi Filbert Bayi kushiriki mbio za nyika ZanzibarTimu ya riadha ya shule ya Filbert Bayi, ambayo inatarajia kushiriki mbio Zanzibar.

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya riadha ya shule za Filbert Bayi imethibitisha kushiriki katika mashindano ya mbio za nyika ya Zanzibar yatakayofanyika Machi 28, imeelezwa.

Kwa mujibu wa mratibu wa mbio hizo za kila mwaka za shule za msingi na sekondari za Zanzibar, Mussa Abdurabi, Filbert Bayi ndio shule pekee ya Tanzania Bara itakayoshiriki mashindano hayo.

Mwaka jana shule hiyo iliyopo Mkuza Kibaha mkoani Pwani, iliibuka ya kwanza katika mashindano hayo yenye msisimko mkubwa na hushirikisha wanafunzi kibao kutoka Unguja na Pemba.

Shule hiyo inamilikiwa na mwanariadha bingwa wazamani wa dunia wa mita 1500 na maili moja, ambaye kwa sasa ndiye Katibu Mkuu wa 
Alisema kuwa shule zote za msingi na sekondari nchini zinaalikwa kushiriki mbio hizo, ambazo zinaibua vipaji na kuviendeleza.

Alisema kuwa mbio za mwaka huu zinatarajia kushirikisha zaidi ya wanafunzi 500, ambao watakimbia katika umbali tofauti tofauti.

Alisema kuwa zaidi ya shule 29 kutoka Unguja na Pemba zimethibitisha kushiriki na ni matarajio yake kuwa shule zaidi zitathibitisha.

Amesema kuwa kila shule itapeleka wachezaji 12, sita wavulana na wasichana idadi kama hiyo, ambao watashiriki katika mbio hizo za umbali tofauti.

Akifafanua zaidi alisema kuwa hadi sasa shule za sekondari zilizothibitisha kushiriki ni 10 wakati za msingi ziko 19.

Ameongeza kusema kuwa mbio za kilometa nane zitawashirikisha wavulana wa sekondari wakati zile za kilometa sita zitashirikisha wasichana wa sekondari na wavulana wa shule za msingi.

Amezitaka shule zilizothibitisha kushiriki kuendelea kufanya maandalizi zaidi ili kuhakikisha zinatoa ushindani katika mashindano hayo na sio kushiriki tu.

Anasema kuwa Idara ya Michezo na Utamaduni ya Zanzibar moja ya majukumu yake ni kuandaa vijana, kuibua vipaji na kuviendeleza, hivyo siku hiyo ya mbio pia kutakuwa na mchezo wa soka kwa ajili ya kusaka na kuinua vipaji.

No comments:

Post a Comment