Monday, 16 March 2015

Gareth Bale aanza kurejesha makali yake Real Madrid
Gareth Bale.
MADRID, Hispania
Kocha Carlo Ancelotti anasema kuwa Real Madrid imehamasika vilivyo kabla ya mchezo wao wa Classico dhidi ya Barcelona
Katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania wa La Liga, Gareth Bale ambaye mechi kadhaa alishindwa kuonesha cheche zake, jana aliibuka na kuifungia timu yake mabao mawili katika kipindi cha kwanza.

Mshambuliaji huyo wazamani wa Tottenham, ambaye alifunga mabao 22 katika mechi 44 katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo yakiwemo yale aiyofunga katika fainali ya Kombe la Mfalme na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, alifanya kweli na kuonesha ameanza kurejea katika kiwango chake.

Wakati alipoiweka Real Madrid mbele katika dakika ya 18 katika ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Levante Jumapili usiku, alikimbia na kuziba masikio yake na kukimbilia katika kona wakati akishangilia bao.

Ni bao lake la kwanza katika mechi tisa lakini ni la 16 katika michezo 38 msimu huu akikaribia kuifikia ile ya msimu uliopita.

Mchezaji pekee ambaye alionekana kutoungana naye kushangilia ni Cristiano Ronaldo. Nusura afunge kwa tiktak lakini mpira ulitoka nje kidogo ya lango.

No comments:

Post a Comment