Thursday, 19 March 2015

Mkanda wa Mayweather, Pacquiao ni noma aisee


NEW YORK, Marekani
WAPENZI wa ndondi duniani wametoa mkanda wenye rangi ya kijani, almasi utakaovalkishwa kiunoni mwa ama Floyd Mayweather au Manny Pacquiao baada ya kumalizika kwa pambano lao la thamani ya pauni Milioni 300 litakalofanyika Mei 2 mwaka huu huko Las Vegas.

Shirikikisho la Ngumi Duniani la WBC liliendesha kura za wazi kuwawezesha mashabiki kuchagua mknda usio wa kawaida ambao utatumika kwa mshindi wa pambano ambao utakuwa sio wa kawaida lakini wenye rangi ya kijani ambayo ni ya kawaida kwa mikanda ya shirikisho hilo.
Gharama ya mkanda huo ni takribani pauni Milioni 1.

Mashabiki walichagua aina hiyo ya mkanda ambao atavishwa mshndi wa pambano hilo litakalofanyika Mei 2.

Katika pambano hilo mshindi atapa bonsai ya paumi milioni 180 endapo Mayweather atashinda na Pacquiao atapokea kitita cha pauni Milioni 120.

Katika taarifa yake ya WBC ilisema: 'Mkanda huu wa aina yake umetengenezwa na Shirikisho la Ndondi Duniani na ni wa aina yake na tayari umepewa Baraka.

No comments:

Post a Comment