Sunday, 8 March 2015

Arsenal, Man United kufa au kupona leo FA Cup


Arsene Wenger.

LONDON, England
TIMU za Manchester United na Arsenal leo zinakutana katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA.

Tayari kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na uzoefu wa timu hizo katika mashindano hayo. Timu hizo ndizo zilizotwaa taji hilo mara nyingi.

Wenger alisema anaamini timu itakayoibuka na ushindi leo ndio itakuwa bingwa wa kombe hilo.

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 4:45 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.

Ninauona huu ni mchezo mgumu na utakaotoa sura halisi ya ubigwa hasa ikizingatiwa kuwa atakayeibuka mshindi ndiye anayeweza kutwaa taji hili mwishoni, alisema kocha huyo.

Aidha, nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney atacheza mchezo huo huku akiwa na kumbukumbu ya mataji tisa, lakini katika vikombe hivyo, halipo la FA.

Louis van Gaal 
Rooney akiwa na timu hiyo mwaka 2005 wakati timu yake hiyo ilipocheza na Arsenal pamoja na mwaka 2007 ilipocheza na
Chelsea, haikuweza kushinda kombe hilo.

“Kwa miaka mingi hatujafikia hatua ya kucheza fainali kwa mchezo huu tunaweza kuondoa gundu na kufikia fainali kirahisi na kulitwaa taji hilo, ”alisema alisema Rooney.

No comments:

Post a Comment