Thursday 5 March 2015

Barcelona, Bilbao kucheza fainali Kombe la Mfalme


Kocha wa Barcelona Luis Enrique

BARCELONA, Hispania
BARCELONA sasa itakutana na Athletic Bilbao katika fainali ya Kombe la Copa del Rey baada ya Luis Suarez na Neymar kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 6-2 dhidi ya Villarreal.
Ikiongoza kwa bao 3-1 kutoka katika mchezo wa kwanza, Barca ilifunga mapema kupitia kwa Neymar kabla Jonathan dos Santos hajaifungia timu yake bao la kusawazisha.
Lakini baada ya kutolewa kwa Tomas Pina kutokana na mchezo mbaya, Suarez alimzunguka kipa na bila hajizi na kufunga bao huku Neymar akiongeza kwa kichwa.
Bilbao iliibuka na ushindi wa bao 2-0 huko Espanyol na kushinda mchezo wao kwa jumla ya mabao 3-1, na kutinga fainali itakayochezwa Mei 30.
Fainali inazikutanisha timu mbili zilizopata mafanikio makubwa katika historia ya mashindano hayo wakati Barca, ikishinda mara 26, ikiwa ni mara tatu zaidi ya Los Leones.
Licha ya historia yao katika kombe hilo, Bilbao haijashinda taji kubwa tangu walipoifunga Barca katika fainali ya mwaka 1984 na wanahitaji kuwa katika kiwango bora kama wanataka kikosi hicho cha sasa cha kocha Luis Enrique.
Hii itakuwa fainali ya kwanza katika historia ya ukocha ya Enrique, ambaye alisema timu yake iko katika kiwango kizuri kabla ya mchezo wao wa ugenini dhidi ya El Madrigal katika mchezo wa La Liga.

No comments:

Post a Comment