Friday, 6 March 2015

TAHA, TOC waandaa kozi ya ukocha wa mikono 
Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania, Nicolaus Mihayo (wa pili kulia).
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mpira wa Mikono Tanzania (Taha) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kimeandaa kozi ya awali ya kimataifa kwa ajili ya walimu wa shule sekondari itakayofanyika katika shule ya Filbert Bayi Kibaha kuanzia Aprili 13 hadi 24 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Taha, Nicolaus Mihayo alisema hivi karibuni kuwa, kozi hiyo itawashirikisha jumla ya walimu 30 kutoka shule za Tanzania Bara na Zanzibar.

Akifafanua zaidi alisema kuwa, Tanzania Bara itakuwa na walimu 20 wakati Zanzibar wataleta walimu 10.

Mihayo alisema kuwa kozi hiyo ya ufudishaji wa mpira wa mikono imewalenga walimu ili baada ya kumaliza waende kuueleze mchezo huo mashuleni

Alisema lengo la Taha sasa kuhakikisha mchezo huo unasambaa mashuleni na mitaani baada ya muda mrefu kuchezwa na taasisi za kijeshi.

Alisema kuwa kozi hiyo itafundishwa na mkufunzi wa kimataifa kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono (IHF), Peter Hans atakayesaidiwa na kocha wa siku nyingi nchini Daid Kiama.

Mihayo alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na ni matumaini yao wote waliothibitisha kushiriki watakuwepo katika kozi hiyo maalum kwa walimu wa shule za msingi na sekondari.

No comments:

Post a Comment