 |
Wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari ya Filbert Bayi wakiwa
nje ya hosteli ya Magereza (Chuo cha Mafunzo) Zanzibar katika picha ya pamoja
na viongozi wa timu hiyo iliyoshiriki mbio za nyika mjini Zanzibar. Kushoto
mstari wa nyuma ni kocha wa timu hiyo Zacharia Gwandu. Kulia nyuma ni matroni `Mama
Mdogo’.
|
 |
Baadhi ya washiriki wa mbio za nyika za kilometa nne za wanafunzi
wasichana wakijiandaa kushiriki mbio hizo Jumamosi.
|
 |
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule za pembezoni mwa kisiwa cha
unguja wakiwasili kwenye uwanja wa Maisala kwa ajili ya kushiriki mbio za nyika
za Zanzibar Jumamosi.
|
 |
Kocha wa timu ya riadha ya shule za Filbert Bayi Zacharia Gwandu
akiwapa maelekezo wachezaji wake kabla hawajashindana katika mbio za nyika
Zanzibar Jumamosi.
|
Wanafunzi wa shule ya Filbert Bayi wakipozi kwa picha katika
bahari mjini Zanzibar ambako walikwenda kushiriki mbio za nyika za shule za
msingi na
sekondari ambazo zilitakiwa na shule hiyo ya Mkuza Kibaha mkoani
Pwani.
 |
Baadhi ya washiriki wa mbio za nyika za kilometa nne za wanafunzi
wasichana wakijiandaa kushiriki mbio hizo Jumamosi.
|
 |
Upendo! Dorcus Boniface (kushoto)
akionesha upendo kwa kumpatia maji mwanariadha mwenzake wa shule ya Filbert
Bayi Jumamosi.
|
 |
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa
Filbert Bayi wakati wa mashindano ya mbio za nyika .
|
 |
Washiriki wa shule ya Filbert Bayi kabla ya kuanza mbio. |
 |
Baadhi ya washiriki wakiwa wamejipanga kabla ya kuanza mbio hizo Jumamosi mjini Zanzibar. |
 |
Baadhi ya washiriki wa mbio za kilometa nne kwa wasichana wa shule za msingi wakielekea sehemu ya kuanzia mbio za Nyika katika viwanja vya Maisala Jumamosi. |
 |
One
Two three, One Two Three! Wanafunzi wa shule ya Filber Bayi wakiongoza
katika mbio za kilometa nne kwa wasichana wa shule ya msingi. Wanafunzi hao
ndio walishika nafasi tatu za kwanza.
|
 |
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Filbert Bayi wakiwaongoza washiriki wengine wa mbio za nyika za kilometa sita
wakati wakielekea kuanza mbio hizo Jumamosi mjini Zanzibra. Timu hiyo ndio
ilishinda.
| | |
No comments:
Post a Comment