Thursday 19 March 2015

Senegal, Nigeria kucheza fainali U20



DAKAR, Senegal
SENEGAL itakutana na Nigeria katika fainali ya Vijana 2015 baada ya kuifunga Mali 2-1 na kushinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili Alhamisi.

Wenyeji walitinga nusu fainali kama washindi wa pili katika Kundi A lakini hiyo haikujalisha baada ya kukutana na Mali ambao ni washindi wa kwanza wa Kundi B.

Ulikuwa mchezo wa kuvutia sana wakati timu hizo mbili zilipochuana vikali huku Moussa Kone akifunga bao la kuongoza mwanzoni kabisa mwa mchezo. Bao hilo liliwapa nguvu wenyeji Senegal ikiwa ni kama sekunde 57 tu tangu kuanza kwa mchezo huo.

Kipa wa Mali Sory Ibrahim Traore hakuweza kulizuia shuti hilo na mpira kumkuta Kone na kufunga bao la kwanza kati ya mawili.

Hatahivyo, Mali walijibu mapigo haraka na dakika moja baadae walifanikiwa kusawazisha na kufanya timu hizo kuwa sare kwa bao la mpira wa mbali lililofungwa na
Alhassane Diallo huko Ibrahima Sy, akiwa katika goli la Senegal asijue la kufanya.

Senegal, ambayo haijawahi kufuzu kwa mashindano ya Fifa ya wachezaji wenye umri chini ya miama 20, iliendelea kuweka shinikizo, lakini Mali ndio nusura wapate bao katika dakika ya 36 kupitia kwa Saliou Guindo.

Kipindi cha pili kilishuhudia timu zote zikifanya mashambulizi kwa zamu wakati shuti la Mohamed Guilavogui lilipookolewa na Sy, baada ya kufanya kazi nzuri.

Senegal ilipata bao la ushindi katika dakika 80 lililofungwa tena na Kone na kuiwezesha timu hiyo kutinga fainali hiyo ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chiniya miaka 20.

No comments:

Post a Comment