NAIROBI, Kenya
RAIS wa Kenya
Uhuru Kenyatta amechoma moto tani 15 za pembe za ndovu ikiwa ni sehemu ya juhudi
za mataifa ya Afrika Mashariki kupiga vita uwindaji haramu.
Pembe hizo za ndovu
katika soko la mitaani inafikia thamani ya kiasi cha dola za Marekani Milioni
30 (sawa na pauni Milioni 19.4), ikiwa ni kiasi kikubwa kuharibiwa nchini
Kenya.
"Pembe hizi
nyingi ni mali ya tembo ambao waliuawa na majangiri," alisema katika hafla
hiyo ya kuchoma moto pembe hizo katika mbuga za hifadhi ya taifa.
Pembe za ndovu
zimekuwa na soko kubwa huko Asia kwa ajili ya mapambo.
Katika soko la
mitaani, kilo moja ya pembe ya ndovu ina thamani ya dola za Marekani 2,000.
Faru nao
wanawindwa kwa ajili ya pembe zao kwa ajili ya dawa za asili.
Watu wa mazingira
wameonya kuwa tembo watatoweka kabisa katika baadhi ya nchi za Afrika katika
kipindi cha miaka michache ijayo.
"Miaka 25
iliyopita baada ya historia ya kuchoma pembe za ndovu, mahitaji ya soko kwa
mara nyingine tena yamekuwa tishio kwa tembo wa Afrika na faru, " alisema
Rais Kenyatta.
No comments:
Post a Comment