Saturday, 14 March 2015

Naibu Katibu Mkuu afungua Mkutano wa Mabadiliko ya Katiba RT leo

Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma  (PSPF) moja ya wadhamini wa Mkutano Mkuu Maalum wa Katiba wa Riadha Tanzania (RT) unaoendelea leo mjini Morogoro.
Mgeni rasmi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Katiba wa Riadha Tanzania (RT) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Profesa Elisante Gabriel (katikati) akipokea fulana kutoka kwa Rais wa RT na Katibu Msaidizi Anthony Mtaka (kulia) na Ombeni Zavalla leo mjini Morogoro.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Riadha Tanzania (RT) unaofanyika leo mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Profesa Elisante Gabriel (mwenye suti).
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Maalum wa Katiba ya Riadha Tanzania (RT) wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Profesa Elisante Gabriel (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo mjini Morogoro.
Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania Suleiman Nyambui (kushoto) akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Profesa Elisante Gabriel baada ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Katiba wa RT. Katikayi ni Rais wa RT Anthony Mtaka.

No comments:

Post a Comment