Monday, 16 March 2015

Arsenal kuifanyia maajabu Monaco Ligi ya Mabingwa UlayaLONDON, England
HAKUNA timu, katika mfumo wa sasa wa mashindano, iliyowahi kusonga mbele ikihitaji zaidi ya bao moja la ugenini, ambapo the Gunners wanaangalia kubadilisha matokeo ya kufungwa 3-1 katika mchezo wa kwanza.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amewataka wachezaji wake kuamini kuwa wanaweza kubadili matokeo hayo wakati kesho Jumanne watakapokutana na Monaco katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilipokea kichapo cha 3-1 wakati timu hizo zilipokutama katika mchezo wa kwanza wa mechi za timu 16 bora kwenye uwanja wa Emirates mwezi uliopita.

Hakuna timu katika kipindi cha Ligi ya Mabingwa wa Ulaya imewahi kusonga mbele wakati ikihitaji ushindi wa zaidi ya  bao moja ugenini ili kukwepa kuondolewa katika mashindano hayo.
Endapo itashindwa kubadili matokeo hayo, basi Arsenal itakuwa imeondolewa kwa msimu wa tano mfululizo katika hatua ya kwanza.

Ratiba Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne Machi 17,2015:

Atl├ętico de Madrid  v Bayer 04 Leverkusen   Saa 4:45 usiku.

Monaco   v   Arsenal  Saa 4:45 Usiku.

Jumatano Machi 18, 2015:
Borussia Dortmund v   Juventus saa 4:45 usiku.

Barcelona    v   Manchester City  saa 4:45 usiku.

No comments:

Post a Comment