Saturday, 14 March 2015

Kocha Sylvester Marsh afariki DuniaNa Mwandishi Wetu, Mwanza
ALIYEWAHI kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Sylvester Marsh (pichani), amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Marsh ambaye ni mtaalam wa kukuza vipaji, alikuwa akisumbuliwa na kansa ya koo nah ii karibuni alitolewa Mwanza hadi Dar es Salaam.

Hali ya kocha huyo aliyewahi kuzifundisha klabu mbalimbali na timu za taifa za Kilimanjaro Stars na Taifa Stars na timu za vijana, iliendelea kuwa mbaya hadi umauti ulimpo mkuta leo asubuhi.

Pamoja na hivyo suala la afya yake liliendelea kuwa siri kubwa huku baadhi ya wadau wakisumbuka kutafuta wodi aliyolazwa.

Aliwahi kuugua taabani na kukawa na taarifa za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtelekeza. Lakini baadaye shirikisho hilo lilikanusha taarifa hizo.

Bado haijafahamika lini mwili wa Marsh utapelekwa Mwanza kwa mazishi yake.

No comments:

Post a Comment