![]() |
Fernando Torres (kulia) akichanja mbuga katika moja ya mechi za La Liga. |
MADRID, Hispania
FERNANDO Torres alifunga
bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga katika kipindi cha
miaka nane wakati Atletico Madrid ikiifunga Getafe bao 2-0.
Mshambuliaji huyo, aliyeshindwa kufunga katika mechi zake
tisa za mwanzo tangu aliporejea katika ligi hiyo, aliungamisha wavuni mpira wa
adhabu uliopigwa na Koke ndani ya dakika tatu.
Na muda mfupi kabla ya mapumziko Tiago aliwafungia wenyeji
bao la pili kwa shuti la karibu na lango.
Torres alikuwa mchezaji anayeongoza kwa mabao katika timu ya
Atletico katika kipindi chake cha moiaka mitano iliyopita nchini Hispania kabla
hajaondoka mwaka 2007 na kuhamia Liverpool akiwa na umri wa miaka 23.
Matokeo hayo yameirejesha Atletico pointi moja nyuma ya
Valencia iliyopo katika nafasi ya tatu, wakati Getafe imebaki katika nafasi ya
13 iliyokuwepo awali kabla ya mchezo huo.
Hatahivyo, mabingwa hao watetezi wa La Liga, ambao wako
katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, bado wako pointi sita nyuma
ya vinara Barcelona, ambao leo watawakaribisha vigogo wenzao Real Madrid katika
mchezo wa kufa mtu katika ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment