LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa West
Ham Carlton Cole ameshitakiwa na Chama cha soka cha England kwa maoni yake
aliyoyatoa katika mtandao wa kijamii.
Shitaka hilo
linahusiano na kile alichoweka katika mtandao huo wa kijamii mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 31 kuhusu shabiki wa Tottenham kufuatia sae ya kufungana
bao 2-2 kati ya timu hizo februaria 22 katika mchezo wa Ligi kuu ya England.
Taarifa ya Chama
cha Soka ilisema: "Inadaiwa kuwa maoni yake yalikuwa yaudharirishaji na
kuumiza na kuuweka mchezo wa soka matatani.
Cole mbaye ni
mshambuliaji wazamani wa timu ya taifa ya England amepewa hadi machi 5 awe
amejibu mashtaka hayo.
Cole ameichezea
The Hammers mechi 17 msimu huu na kufung mabao matatu.
Alipigwa faini na
Chama cha Soka kutokana na maoni yake aliyoyatoa katika Twitter
wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa England na Ghana Aprili mwaka
2011.
No comments:
Post a Comment