Sunday, 8 March 2015

Okwi awaliza Yanga Uwanja wa Taifa Simba ikishinda 1-0Na Mwandishi Wetu
SIMBA jana ilidhihirisha umwamba mbele ya Yanga baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao hao wa jadi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao lililowafanya wapenzi wa Yanga kulala mapema huku wenzao wa Simba wakichonga sana, lilifungwa na mshambuliaji wazamani wa Yanga Mganda Emmanuel Okwi (pichani) katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Ushindi huo wa Simba haukutarajiwa kabisa na mashabiki na viongozi wa Yanga mabao kwa wiki nzima walionekana kutamba kuwa timu yao itaibuka na ushindi kwani ina kikosi imara na cha uhakika.

Bao hilo pekee katika mchezo huo lilifungwa na Okwi katika dakika ya 51 ikiwa ni dakika zaidi, aliupiga mpira kifundi na kujaza wavuni na kuibua chereko kwa wapenzi wa Simba huku wenzao wa Yanga wakijipa matumaini kuwa timu yao itarudisha na kupata bao la ushindi.

Tangu awali Simba ilionekana ingeibuka na ushindi baada ya timu yao ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 kuibuka na ushindi wa bao 4-2 dhidi ya wenzao wa Yanga katika mchezo uliochezwa mapema.

Katika mchezo huo Haruna Niyonzima alitolewa uwanjani kwa kadi Nyekundu baada ya kukaidi amri ya mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro, ambapo alipiga mpira langoni licha ya kupigiw filimbi ya kuotea na kusababisha kuoneshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.

Vikosi Vilivyoanza leo:

SIMBA SC: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhan, Mohhamed Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Abdi Banda/Simon Sserunkuma, Ramadhani Singano, Jonas Mkude, Ibrahim Ajib/ Elias Maguli, Said Ndemla na  Emanuel Okwi.

YANGA SC: Ally Mustafa,Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelven Yondani, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amis Tambwe, Mrisho Ngassa/ Khap Sherman na Danny Mrwanda/ Hussein Javu.

WAAMUZI:

Mwamuzi wa kati: Martin Saanya kutoka Morogoro.
Mwamuzi msaidizi namba moja:Soud Lila kutoka Dar es Salaam
Mwamuzi msaidizi namba mbili:Frolent Zabron wa Dodoma.
Mwamuzi wa akiba au mezani: Islael Mjuni.

No comments:

Post a Comment