Mwanariadha wa Kenya David Rudisha. |
NAIROBI, Kenya
BINGWA wa Olimpiki
na anayeshikilia rekodi ya dunia David Rudisha amethibitisha kushiriki katika
mbio za IAAF Diamond League itakayofanyika Juni 7 mwaka huu.
Mbio hizo za aina
yake zinatarajia kufanyika Sainsbury huko Birmingham.
Rudisha alifanya
kweli wakati wa Michezo ya Olimpiki iliyofanyika London mwaka 2012 wakati
aliposhinda mbio za mita 800 akiongoza kuanzia mwanzo wa mbio hadi mwisho.
Mwanariadha huyo
wa Kenya alishinda mbio hizo kwa kutumia dakika 1:40.91, ambapo Mkenya huyo
anataka kuonesha makali yake atakaporejea tena katika ardhi ya Uingereza mwezi
Juni.
“Napenda sana kushiriki
mbio Uingereza na sitasubiri kujipanga katika mbio za Sainsbury's Birmingham Grand Prix,” alisema.
“Nina kumbukumbu nzuri ya
kushinda zaidi ya mita 600 huko Birmingham katika kipindi
kilichopita cha majira ya joto nilipoweka rekodi ya dunia katika Olimpiki ya
London 2012.
“Nategemea
naweza kurudia kiwango kile nilichokuwa nacho wakati ule…”
Mwanariadha huyo
mwenye umri wa miaka 26 mara pekee kwa mara ya mwisho alishinda Birmingham
mwaka jana katika mashindano kama hayo, ambako alishinda mbio za mita 600.
Rudisha alishinda
taji la dunia mwaka 2011 na anatarajia mbio hizo za Birmingham Grand Prix zitakuwa muhimu kabla
hajajaribu kutwaa tena taji hilo Beijing mwezi Agosti.
No comments:
Post a Comment