Sunday, 22 March 2015

Gerrard aomba radhi kwa kadi nyekundu, Liverpool yachapwa na Man UnitedSteven Gerrard akioneshwa kadi nyekundu

LONDON, England
NAHODHA wa siku nyingi wa Liverpool Steven Gerrard tayari ameomba radhi kwa uzembe alioufanya uliosababisha kutolewa nje kwa kadi nyekundi wakati timu yake ikifungwa 2-1 na Manchester United baada ya kumkanyaga Ander Herrera.

Nahodha huyo aliingia akitokea benchi katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Anfield  kuchukua nafasi ya Adam Lallana kuanza kipindi cha pili lakini ndani ya sekunde 38 alitolewa nje ya uwanja baada ya kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na Martin Atkinson kwa kumkanyaga mwenzake.

Gerrard, atakayeondoka na kujiunga na LA Galaxy mwishoni mwa msimu, akizungumza mara baada ya mchezo huo aliomba radhi kwa wachezaji wenzake na mashabiki wa timu hiyo.

 Natakiwa kukubali hili. Kwa kweli ulikuwa uamuzi sahihi, alisema Gerrard.

Napenda kuwaomba radhi wachezaji wenzangu, kocha na muhimu zaidi mashabiki wetu nakubali kuwajibika kwa kitendo changu.

Nilikuwa najaribu kuruka daluga lake, niliona njumu zake na alifanya vibaya. Niko katika soka kwa muda mrefu kujua wakati unafanya kitu fulani kama kile…Nawajibika kwa kosa hilo.

Hatahivyo, kocha wa Liverpool Brendan Rodgers aliunga mkono kitendo cha Gerrard kuomba radhi hadharani.

'Ni jamnbo kubwa kama mtu anatolewa nje na anapokuwa nje anaomba radhi…’

No comments:

Post a Comment