*kupanua
upatikanaji wa huduma za mawasiliano mikoa ya kusini
TIGO Tanzania
imezindua mnara mpya katika kijiji cha Magubike mkoani Iringa jambo linakusudia
kutoa fursa mpya za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Kutokana na
maelezo ya Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Bi. Cecile Tiano, mnara huo mpya ni kati
ya minara 843 iliyopangwa kujengwa nchini kote mwaka huu, ambapo minara 348 au asilimia 41 ya minara
yote itajengwa katika mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo Iringa, Ruvuma, Njombe, Mbeya na
Rukwa.
Mnara huu wa
Magubike umejengwa kwa ushirikiano na serikali kupitia mpango maalum wa
kufikisha mawasiliano nchini kote uitwao ‘Universal Communication Services Access Fund’ (UCSAF). Mpango ambao unategemea
kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo ya vijijini na mijini
kupitia mfumo wa TEHAMA na ambao utahakikisha upatikanaji wa huduma za
mawasiliano katika maeneo ya vijijini na mijini.
Akizindua
mnara huu mpya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Juma Masenza, alikaribisha
uwekezaji wa kampuni hiyo akisisitizia kwamba mnara huo utasaidia kufungua
fursa za kijamii na kiuchumi zilizopo katika mkoa huo.
Masenza
alisema, “Napenda
kuchukua fursa hii kuwahakikishia wawekezaji katika sekta ya mawasiliano kwamba
serikali itaendelea kushirikiana nao na wadau wengine wa maendeleo kwa
kuwapatia mazingira bora ya kufanyia biashara kwa ajili ya kuboresha sekta ya
mawasiliano nchini.”
Wakati huohuo;
Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Bi. Cecile Tiano alisema kampuni hiyo imekuwa
ikiwekeza wastani ya dola za kimarekani milioni mbili kwa wiki katika upanuzi
wa mtandao na uboreshwaji wa huduma zake nchini kote ndani ya miaka miwili iliyopita
ikiwa na lengo la kuwezesha watu kuishi maisha ya kidijitali.
Akielezea
kuhusu umuhimu wa huduma za mawasiliano kwa wakazi wa eneo hilo, Meneja Mkuu
huyo alisema kwamba Tigo Kilimo, ni
huduma mojawapoo watakayofaidika nayo. huduma
nayowasaidia wakulima kupata habari muhimu kama vile bei za mazao, utabiri wa hali ya hewa na taarifa tofauti tofauti za
kilimo kupitia simu zao. Pia watu wanaweza kufaidika kiuchumi kwa kuwa wakala wa
Tigo Pesa.
Alisema Tigo pia ina mipango ya kuongeza matawi
yake ya huduma kwa wateja katika mikoa hiyo mitano, kutoa fursa za vijana
kujiajiri kupitia kuwa wakala wa kujitegemea wa Tigo pamoja na kuchangia miradi
mbalimbali ya kijamii kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii.
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni ya
mawasiliano inayoongoza kwa ubunifu nchini, inafahamika kama kampuni inayolenga
kuleta maisha ya kidijitali katika jamii. Inatoa huduma tofauti tofauti za
mawaliano kwa njia ya simu, intanet ya kasi na kutuma na kupokea fedha. Aidha
Tigo imebuni bidhaa na huduma mbali mbali kama Facebook kwa Kiswahili, Tigo
Pesa App kwa watumiaji wa simu za Android na iOS, na ni kampuni ya simu ya
kwanza Afrika Mashariki kuanzisha huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu kimataifa, yenye uwezo wa
kubadilisha fedha za kigeni.
Kwa kutumia tekinolojia ya 3G Tigo ina wahakikisha
wateja upatikanaji wa huduma bora na za uhakika. Kati ya mwaka 2013 na 2014,
kampuni ilizindua minara mipya zaidi ya 500 na pia ina mipango wa kuongeza mara
mbili kiwango cha uwekezaji ifikapo mwaka 2017 ili kuweza kupanua wigo wa
mawasiliano na uwezo wa mtandao hasa hasa katika maeneo ya vijijini. Tigo ina
wateja zaidi ya milioni 8 na inatoa ajira za moja kwa moja na kwa namna mbali
mbali kwa Watanzania zaidi ya 100,000 ambao wanajumuisha wafanyakazi wa huduma kwa
wateja, wa kutuma na kupokea fedha, watu wa mauzo pamoja na wasambazaji.
Tigo ni kampuni ya simu inayoongoza chini ya
kampuni mama ya mawasiliano Millicom, ambayo imejizatiti katika kuhamasisha na
kufanikisha maisha ya kidijitali katika nchi 44 zenye biashara zake Afrika na
Latin Amerika, pamoja na ofisi za kampuni zilizopo Ulaya na Marekani. Kwa
kutambua kwamba ubunifu ndio utakaowafanya kuendelea kuwa juu ya ushindani,
Millicom inaendelea kuthamini mchango wa wadau wake, wakitumia dhana ya “demand more” kama namna ya kufanya biashara na kuendeleza
nafasi yao kama kampuni inayoongoza katika kufanikisha maisha ya kidijitali
katika baadhi ya masoko makubwa yenye ushindani mkali duniani.
“TABASAMU, UKO NA TIGO”
Kwa maelezo
zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na:
John Wanyancha – Meneja Mawasiliano
Simu: 0658 123 089
![]() |
Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo, Cecile Tiano (katikati)
akisoma hotuba yake mara baada ya kampuni hiyo ya mawasiliano kuzindua mnara
wake wa masiliano katika kijiji cha Maagubike, Iringa Vijijini.
|
No comments:
Post a Comment