Monday, 16 March 2015

Dick Advocaat achukua mikoba ya Poyet Sunderland

LONDON, England
KOCHA mkongwe wa Uholanzi yuko mbioni kutangazwa kuwa mbadala wa Gus Poyet baada ya Mruguay huyo kutupiwa virago Jumatatu, huku safari yake ya kwanza ni kwenda kucheza na West Ham.

Dick Advocaat atachukua nafasi ya Gus Poyet baada ya kuthibitisha kuwa amesaini mkataba wa muda mfupi kuiongoza Sunderland iliyopo katika hatari la kushuka daraja hadi mwishoni mwa msimu huu.

Advocaat alibainisha taarifa hizo katika jarida la michezo la Uholanzi la Voetbal International Jumatatu, saa chache baada ya Poyet kutupiwa virago kufuatia timu hiyo kuchapwa 4-0 katika Ligi Kuu ya England na Aston Villa mwishoni mwa wiki.

Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 67, aliyetumia miezi minne kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Serbia mwaka jana, lakini sasa atakuwa akifanya kazi katika uwanja Mwangaza.

Advocaat kutua Sunderland kunamfanya kocha huyo kwa mara ya kwanza kufanya kazi na timu ya Ligi Kuu ya England, ambapo aliwahi fundisha soka huko Uholanzi, Ujerumani na Scotland.

"Hii ndio kitu wakati wote nilikuwa nakihitaji kufanya, kufundisha timu ya Ligi Kuu. Ligi Kuu ya England ni mashindano ya aina yake na magumu," alisema Advocaat.

"Kama kocha ni mahali ambako unataka kufanyakazi, alisema.

No comments:

Post a Comment