Monday, 9 March 2015

Carlo Ancelotti aitetea Real Madrid butuMADRID, Hispania
KOCHA Carlo Ancelotti (pichani) anasema kuwa kamwe hatabadilisha "sura" wa kikosi chake cha Real Madrid, licha ya washambuliaji wake kuwa butu.

Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale walipambana dakika za mwisho, huku Real Madrid ikishindwa kufunga katika mechi mbili zilizopita.

WBale aliyesainiwa kwa rekodi ya dunia hajafunga katika mechi zake nane zilizopita, lakini anatetewa na kocha wake.
"Wamefunga machache katika mecgi zilizopita lakini nafikiri tunatakiwa kuwasaidia washambuliaji, " alisema Ancelotti.

"Hatutabadili sura ya timu yetu kwa sababu hilo ndilo linatufanya tujisikie vizuri zaidi, " aliongezakocha huyo Muitalia. "Bila wasiwasi wowote nina imani nao.

"Nitamuacha Karim kwa sababu hajafunga katika mechi chache. Nimuache Cristiano. Sifikiri kama Bale atakuwa na furaha kwa jinsi anavyocheza lakini najua kuwa anatakiwa kuimarisha zaidi."

Bale ambaye ni mchezaji wazamani wa Tottenham na mchezaji mwenzake Luka Modric alirejea katika kikosi cha Real kwa mara ya kwanza tangu alipoumia misuli Novemba huku klabu yake ya Hispania ikiongoza kwa jumla ya mabao 2-0 huko Gelsenkirchen katika mchezo wa kwanza.

No comments:

Post a Comment