Sunday 1 March 2015

Chelsea mabingwa Kombe la Ligi




Baadhi ya wachezaji wa Chelsea wakiongozwa na John Terry (katikati) wakishangilia moja ya mabao yao mawili.
LONDON, England
JOSE Mourinho ametwaa taji lake la kwanza tangu arejee kwa mara ya pili katika klabu hiyo kama kocha wa Chelsea baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi kufuatia ushindi dhidi ya Tottenham katika mchezo uliofanyika leo katika uwanja wa Wembley.
John Terry na Diego Costa waliwamaliza wapinzani wao wakisaidiwa na mipira iliyopoteza mwelekeo, ambapo kila mmoja akifunga katika kila kipindi wakati Spurs ikishindwa kurejea mafanikio yao dhidi ya Chelsea katika mashindano haya miaka saba iliyopita.
Ushindi huo umempatia Mourinho taji lake la kwanza tangu alipofanikiwa La Liga alipokuwa na Real Madrid mwaka 2012 na ushindi wake wa kwanza Chelsea ushindi wa fainali ya Ligi ya Ulaya dhidi ya Benfica huko Amsterdam mwaka mmoja baadae.
Pamoja na historia yake kuwa na mataji kibao, Mourinho alidai kuwa fainali hiyo ilikuwa muhimu zaidi kwake.
Aidha; Chelsea wakati ikikaribia kutwaa taji la Ligi Kuu ya England, wapinzani wao wakubwa katika mbio hizo Manchester City walijikuta wakipokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Liverpool Jumapili kabla fainali hiyo haijapigwa.
Chelsea sasa ina mchezo mmoja zaidi mkononi baada ya Jumapili kutoshuka katika mechi ya Ligi Kuu ya England na kucheza Kombe la Ligi.

No comments:

Post a Comment