Monday 31 December 2018

Michuano ya Emirates FA Cup Sasa Ndani ya DStv


Na Mwandishi Wetu
Wateja wa DStv wanauanza mwaka kwa kicheko baada ya kutangazwa rasmi kuwa DStv itaonyesha michuano maarufu ya ya Emirates FA Cup kupitia chaneli za SuperSport kuanzia tarehe 4 Januari 2019. Hii inamaana kuwa mechi za mzunguko wa tatu sasa zitaonekana katika kisimbuzi cha DStv.

Akizungumzia kurejea kwa michuano hiyo katika chaneli za SuperSport, Mkurugenzi wa MutiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso amesema “Lengo letu ni kuwa mstari wa mbele katika kutoa burudani ya soka bora duniani kwa wateja wetu wa DStv hivyo, kuanzia tarehe 4 Januari 2019, wateja wetu wataweza kufurahia michuano ya Kombe la Emirates maarufu kama FA Cup kupitia chaneli za SuperSport zizopatikana ndani ya vifurushi vya DStv".

 Amesema kuwa muda wote MultiChoice imahakikisha kuwa wateja wake wanapata burudani ya hali ya juu na ndiyo sababu wamekuwa wakiongeza maudhui mapya kila uchao katika vifurushi vya DStv.

Sambamba na mechi za michuano ya kombe la FA za mzunguko wa tatu zitakazoanza Januari 4 2019, wateja wa DStv pia wataendelea kuburudika na ligi kubwa za soka zinazotamba duniani ikiwemo ligi kuu ya Uingereza maarafu kama PL, ligi kuu ya Italia Seria A, michuano ya ligi kuu ya Hispania {La Liga} na ligi ya mabingwa Ulaya maarufu kama EUFA Champions League bila kusahau maudhui  mengineyo mengi zikiwamo filamu na tamthilia mpya kutoka nje na ndani ya Tanzania na vipindi vya watoto.

Mechi hizi za michuano  ya Kombe la FA zitakuwa zikipatikana mubashara kupitia chaneli za Supersport ndani ya DStv. Idadi ya mechi zitakazoonekana mubashara zinatofautiana kulingana na aina ya kifurushi huku baadhi ya mechi hizo zikionekana katika kifurushi cha chini cha DStv Bomba kwa Sh 19,000.

Kwa wateja wanaotaka kujiunga na DStv, bado wanaweza kunufaika na ofa inayoendelea ya msimu wa sikukuu ambapo kwa gharama ya Sh.79,000 tu!  Mteja anapata seti kamili ya DStv. Pia kupitia mtandao wa bongoshop.dstv.com mteja anaweza kupata maelekezo ya ziada ya namna ya kujiunga na DStv, ikiwemo kuunganishwa na mawakala na mafundi wa DStv popote alipo.


Tuesday 18 December 2018

Ndege Mpya Mbili za ATCL Kuwasili Jumapili


Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema ndege mpya mbili za ATCL zinatarajiwa kutua Jumapili zikitokea nchini Canada tayari kwa kuanza kufanya kazi ya kusafirisha abiria.

Aidha, aliwaondoa watu hofu kuwa kusimamishwa kwa huduma za ndege ya Fastjet hakutawaathiri kwa vile wamejipanga kusafirisha abiria usiku na mchana ili kuhakikisha hawapati shida ya usafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele alisema ndege hizo zitatua kama ratiba haitabadilika, kwani wameshapeleka rubani na wahudumu wa ndege kwenda nchini humo kwa ajili ya kurudi nazo.

“Mtengenezaji alituahidi mpaka Desemba 23, mwaka huu zitakuwa ziko tayari kurudi kuja kuanza kazi,  tayari tumepeleka wahudumu wa kuja nazo,”alisema.

Waziri huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa  hakuna atakayepata shida ya usfiri wa ndege kwani wamejipanga kwa viwanja vyenye taa kusafiri mpaka usiku na vile visivyokuwa na taa kama Songwe wataongeza ndege kutokana na uhitahiji ili watu wasikose usafiri kwenda na kutoka maeneo yote.

Aliwataka wahudumu wote wa ndege  na wale wa Mamlaka ya Usafiri wa  nchi Kavu na Majini (Sumatra) waliokwenda likizo kurudi haraka kusimamia huduma hizo hasa kipindi hiki cha sikukuu na kuhakikisha nauli haziongezwi upande wa mabasi yaendayo mikoani.

Alizungumzia kuhusu Fastjet kupewa notsi ya siku 28 kwa ndege hiyo kusitisha huduma baada ya kushindwa kulipa madeni yake na kutokidhi huduma za abiria na kwamba hawataruhusiwa kuruka popote hadi kuyalipa ikiwemo huduma, mishahara wanazodaiwa.

Pia Waziri Kamwele aliwataka viongozi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha wanafanyia kazi malalamiko ya abiria wanayoyatoa juu ya mapungufu katika viwanja vya ndege vikiwemo vipoza hewa katika eneo la pili la kuwasili na kuondokea abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Juliuys Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Alisema abiria wamekuwa wakilalamika kuhusu joto lililopo Terminal Two, lakini wahusika hawajachukua hatua yoyote ya kurekebisha na wameendelea kufanya kazi kimazoa tu wakati hiki ni kipindi cha ushindani.

Pia alisema mtandao nao haufanyika  kazi vizuri, hivyo aliwataka TAA kuchukua hatua haraka kurekebisha matatizo hayo, sivyo kuanzia mwakani atachukua hatua kali.

Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela aliomba muda ili kufanyia kazi mapungufu hayo na kusema atachukua hatua za kiutawala kuhakikisha mambo yanakuwa sawa haraka iwezekanavyo.

Mayongela pia aliwataka waandishi wa habari kuwa makini kwa kuandika au kutangaza habari kutoka katika vyanzo vya uhakika au rasmi na sio kupokea taarifa upande mmoja tu, tena kutoka katika mitandao.

Waziri alitoa muda hadi Januari mwakani kufanyia kazi changamoto hizo na ikiwa watashindwa basi wajiondoe wenyewe huku akisisitiza kuwa, sehemu ya tatu ya abiria ya Kiwanja cha Ndeger cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kinatarajia kuanza kutumika Mei mwakani.

Friday 14 December 2018

Wanariadha Arusha Watamba Riadha ya Wazi


Viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kabla ya kuanza kwa mbio za kilometa 10 za mashindano ya wazi ya taifa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha leo.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
MASHINDANO ya wazi ya taifa ya riadha ya Ngorongoro ‘Ngorongoro National Open Athletics Championships’ yamefanyika leo jijini Arusha na kushuhudiwa na watazamaji kibao waliofika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku wanariadha wa Arusha wakitamba.

Tofauti na mashindano hayo yanapofanyikia jijini Dar es Salaam, leo uwanja huo ulikuwa na watazamaji kibao walioshuhudia wanariadha  wao, wengi wakitokea Arusha wakitamba katika mbio na michezo mbalimbali.
 
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa mara ya kwanza katika mashindano ya taifa yalishirikisha mbio za barabarani za kilometa 10 badala ya zile za uwanjani za meta 10,000, ambazo  jana hazikuwepo.
 
Katika mbio za kilometa 10, Jackson Mwakombe alimaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 32:00.22, baada ya kuongoza kwa muda mrefu mbio hizo akiwaacha wenzake mbali.
Wanariadha wakichuana katika mbio za meta 5,000 za mashindano ya wazi ya taifa jijini Arusha leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 Arusha pia ilitwaa medali ya dhahabu katika kilometa 10 kwa wanawake wakati Neema Kisuda alipomaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 40:01.04 akifuatiwa na wanariadha wengine wa Arusha, ambao ni Gloria Makula na Sarah Hiti waliomaliza katika nafasi ya pili na tatu kwa dakika 40:27.98 na 41:26.91.

Benjamin Michael alimaliza wa kwanza kwa kutumia sekunde 10:99, huku Laurent Masatu na Bakari Barnabasi wote wa Arusha wakimaliza katika nafsi ya pili na tatu kwa kutumia sekunde 11:10 na 11:18.
Mwanariadha kipita mbele ya bango la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ambao ni wadhamini wa mbio za wazi za taifa zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Katika mbio za meta 800, Mariam Salim, Grace Jackson na Shamin Ramadhani wote wa Arusha walimaliza kwa dakika 2:18.09, 2:20.72 na 2:21.87 na kushika nafasi ya kwanza, ya pili na tatu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kwa upande wa meta 5,000 wanawake, Arusha ilishika nafasi mbili za kwanza pale, Natalia Elisante na Angelina Daniel walimaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 16:54.52 na 17:18.80 huku Angelina John wa Singida akimaliza wa tatu kwa kutumia dakika 18:10.68.
Ni hatari lakini salama! Mwanariadha Jackson Makombe akipita eneo la Njiro huku magari nayo yakipita wakati wa mbio za kilometa 10 za mashindano ya wazi ya taifa jijini Arusha leo. Makombe alishinda mbio hizo kwa dakika 32:00.22.
Katika mbio za meta 800 kwa wanaume, mwanariadha wa Manyara Gabriel Geay alitamba baada ya kumaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 1:50.75 huku akifuatiwa na Faraja Damas na Simon Francis wote wa Arusha waliotumia muda wa dakika 1:52.28 na 1:52.68.

Washindi wa kwanza katika kila mchezo wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, waliondoka na Sh 150,000 kila mmoja wakati wale walioshika nafasi za pili kila mmoja alipata 100,000 na watatu Sh 50,000.
Watoto nao walichuana katika mbio za meta 100 wakati wa mashindano hayo ya wazi ya taifa leo Sheikh Amri Abeid.
 Washindi wa kwanza wa michezo yote kuanzia ile ya kilometa 10, meta 5,000,  meta 100, meta 800, kuruka chini, meta 400, meta 1500, meta 200 na wale wa kupokezana vijiti, wote kesho watatembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, ikiwa ni ofa kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo.
Wanariadha wakike wakichuana katika mbio za meta 5,000.

Mwanariadha akiruka chini wakati wa mashindano ya wazi ya taifa ya riadha leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Tuesday 11 December 2018

TAA Waendelea Kutoa Kwa Jamii,Yasaidia Tamasha la Ngoma


Mratibu wa Tamasha la Ngoma za Utamaduni na Maonesho ya Biashara la Chato, Amon Mkoga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo katika Kijiji cha Makumusho Jiini Dar es Salaam leo. Tamasha hilo la tatu litafanyika Chato mkoani Geita Desemba 22, 2018. Kulia ni Meneja  Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). 

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha shughuli mbali mbali za jamii, kwa kutoa misaada yenye tija.


Hilo limekuwa bayana leo tarehe 12 Disemba, 2018 kwenye Kijiji cha Makumbosho Jijini Dar es Salaam, ambapo TAA imetoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba, 2018 katika Uwanja wa Mazaina Chato.

Akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bw. Abdi Mkwizu amesema Mamlaka ina wajibu mkubwa wa kuunga mkono shughuli za kijamii, kwa kutoa misaada ya mbalimbali.

   Kaimu Mkurugenzi wa Rasimali Watu na Utawala wa Viwanja vya NdegeTanzania (TAA), Abdi Mkwizu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la za Utamaduni la Chato katika Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo. 
“Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ina wajibu wa Kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania lakini pia mbali na kutoa huduma hizo tuna wajibu wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kwa wadau ambao wanatufanya sisi tuwepo,” amesema Bw. Mkwizu.

Pia Bw. Mkwizu amebainisha kwamba TAA inahudumia Viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara chini ya serikali, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii sehemu yeyote ile kulingana na uhitaji na bajeti iliyopo.



 Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Bw. Habbi Gunze (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Tatu la  za Utamaduni katika Kijiji cha Makumbusho. Kulia ni Meneja Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Abdi Mkwizu na mwingine ni mratibu wa tamasha hilo, Amon Mkoga. Tamasha hilo litafanyika Chato mkoani Geita.


“Ikumbukwe siku za hivi karibuni TAA tumeshirika katika kufanikisha Tamasha la Urithi Wetu lililofanyika kuanzia Oktoba Mosi mpaka Oktoba 7, 2018 katika Kijiji cha Makumbusho, tumetoa pia msaada wa Mafuta Kinga jua ya Ngozi kwa watoto wenye ulemavu wa Ngozi katika baadhi ya shule hapa Dar es Salaam, lakini pia tarehe 24 Novemba mwaka huu tumekabidhi Shule ya Msingi ya Kisasa huko Bukoba inaitwa Tumaini,  na tunaamini itaongeza ufaulu kwa wanafunzi huko Bukoba na hayo ni macheche kati ya mengi ambayo Mamlaka inafanya kwa Jamii” amebainisha Bw. Mkwizu.
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia) akikabidhi moja ya fulana,zilizotolewa na TAA kwa ajili ya Tamasha la Ngoma za Utamaduni la Chato, linalotarajia kufanyika Desemba 22, 2018.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu na niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Bw. Habbi Gunze ameishukuru Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wake kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato.

“Niwashukuru sana Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wao nap engine bila wao hili la leo lisingeweza kufanikiwa. Utamaduni ndio uhai wa Taifa, kwa hiyo nchi isipokua na Utamaduni nchi inakua sio hai, hivyo kwa Mchango huu wa kusaidia hili nawapongeza sana TAA” amesema Bw. Gunze.
Mcheza ngoma za asili, Bw,. Ally Mango akicheza na nyoka mbele ya waandishi wa Habari katika kikiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa fulana 100 kwa tamasha la Utamaduni la Chato zilizotolewa leo na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).  (PICHA ZOTE KWA HISANI YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA)
Naye Mkurugenzi wa Chief Promotions ambaye ndie mratibu wa Tamasha hilo Bw. Amon Mkoga amesema kwamba Tamasha litakuwa na mambo yote ya kiutamaduni ili kuenzi asili ya Kitanzania.

“Kauli mbiu ya Tamasha la Utamaduni la Chato inasema “Maendeleo ya Viwanda yasiache Utamaduni nyuma” ambapo Tamasha hili ni maalum kwa ajili ya kuuenzi utamaduni wa Mtanzania. Katika Tamasha hili kutakua na Vikundi mbalimbali vya Utamanduni. Vikundi vya ngoma vitakuwepo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Tabora na Chato wenyewe, hivyo tunawaomba wananchi mtusaidie kufikisha taarifa hizi kwa watanzania” ameeleza Bw. Mkoga.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga (katikati), Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Salaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu, wakionesha vipeperushi vya Tamasha la Ngoma za Utamaduni la Chato.
Tamasha la Utamaduni la Chato ni tamasha kubwa la ngoma ambalo hufanyika kila mwaka na hii itakua ni mara ya tatu mfululizo likifanyika Chato mkoani Geita.





Saturday 1 December 2018

Mahafali Pre-Unit Shule za Filbert Bayi Yafana

Wahitimu wa darasa la Pre-Unit wa Shule za Filbert Bayi wakipozi kwa picha kabla ya kupiga picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu waziri wa Nishati na Madini, Subira Mgalu Mkuza, Kibaha leo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Subira Mgalu (kushoto) akiwasili katika shule za Filbert Bayi Mkuza leo. Kulia ni Mkurugenzi wa shule hizo, Anna Bayi.


Wanafunzi wa Pre-Unit wa shule za Filbert Bayi wakiwa na mgeni rasmi kabla ya mahafali yao leo Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.


Wazazi wa wahitimu wa Pre-Unit wa Shule za Filbert Bayi pamoja na wageni waalikwa wakati wa mahafali leo Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.

Wazazi na waalikwa wakati wa mahafali ya Pre Unit leo.

Wahitimu wa Pre Unit wakiongozwa na mwalimu wao wakati wa kuingia katika ukumbi leo.

Pre Unit wakicheza wakati wa mahafali yao leo Mkuza, Kibaha.



Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Subira Mgalu (wa pili kulia) akiwatuza wanafunzi wa Pre Unit baada ya kukunwa na uchezaji wao wakati wa mahafali yao leo. Kulia ni Mkurugenzi wa shule hizo, Anna Bayi.