Monday, 9 March 2015

Arsenal yaikwepa Liverpool nusu fainali FA Cup


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger.

LONDON, England
MABINGWA watetezi Arsenal watakutana na Bradford City au Reading katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA baada ya kuifunga Manchester United katika hatua ya nane bora.

Aston Villa watakutana na Liverpool au Blackburn katika nusu fainali nyingine ya kombe hilo.

Reading ambao wako katika Ligi Daraja la Kwanza na Bradford iliyopo Daraja la Pili zitacheza mchezo wao wa nane bora Jumatatu Machi 16 huku tarehe ya mchezo wa Blackburn-Liverpool bado haijapangwa.

Mechi za nusu fainali zinatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Wembley Aprili 18 na 19.

The Gunners wanatumaini kuwa kupangwa na timu za madaraja ya chini kutawawezesha kufanikiwa kwa mara ya pili kucheza fainali ya kombe hilo, baada ya mwaka jana kuifunga Hull City 3-2 na kutwaa taji la 11 la Kombe la FA Mei mwaka jana.
Lakini Bradford iliifunga Arsenal katika robo fainali katika msimu wa mwaka 2012-13 na timu hiyo ndogo ilifanikiwa kutinga fainali, na msimu huu imeziangusha timu za Ligi Kuu za Chelsea na Sunderland katika Kombe la FA.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger alisema: "Mwaka jana tulicheza kiaina kwenye uwanja wa Wembley katika nusu fainali na hilo tunalitarajia tena.

Ratiba kamili:
Bradford/Reading v Arsenal
Aston Villa v Liverpool/Blackburn

No comments:

Post a Comment