Friday 15 June 2018

RATIBA KAMILI LIGI KUU ENGLAND 2018-19


Jumamosi, Agosti 11, 2018
Arsenal v Man City
Bournemouth v Cardiff
Fulham v Palace
Huddersfield v Chelsea
Liverpool v West Ham
Man Utd v Leicester
Newcastle  v Spurs
Southampton v Burnley
Watford v Brighton
Wolves v Everton
Jumamosi, Agosti 18, 2018
Brighton v Man Utd
Burnley v Watford
Cardiff v Newcastle
Chelsea v Arsenal
Palace v Liverpool
Everton v Southampton
Leicester v Wolves
Man City v Huddersfield
Spurs v Fulham
West Ham v Bournemouth
Jumamosi, Agosti 25, 2018
Arsenal v West Ham
Bournemouth v Everton
Fulham v Burnley
Huddersfield v Cardiff
Liverpool v Brighton
Man Utd v Spurs
Newcastle v Chelsea
Southampton v Leicester
Watford v Crystal Palace
Wolves v Man City
Jumamosi, Septemba 01, 2018
Brighton v Fulham
Burnley v Man Utd
Cardiff v Arsenal
Chelsea v Bournemouth
Palace v Southampton
Everton v Huddersfield
Leicester v Liverpool
Man City v Newcastle
Watford v Spurs
West Ham v Wolves
Jumamosi, Septemba 15, 2018
Bournemouth v Leicester
Chelsea v Cardiff City
Everton v West Ham
Huddersfield v Crystal
Man City v Fulham
Newcastle v Arsenal
Southampton v Brighton
Spurs v Liverpool
Watford v Man Utd
Wolves v Burnley
Jumamosi Septemba 22, 2018
Arsenal v Everton
Brighton v Spurs
Burnley v Bournemouth
Cardiff City v Man City
Palace v Newcastle
Fulham v Watford
Leicester v Huddersfield
Liverpool v Southampton
Man Utd v Wolves
West Ham v Chelsea
Jumamosi, Septemba 29, 2018
Arsenal v Watford
Bournemouth v Palace
Cardiff v Burnley
Chelsea v Liverpool
Everton v Fulham
Huddersfield v Spurs
Man City v Brighton
Newcastle v Leicester
West Ham v Man Utd
Wolves v Southampton
Jumamosi, Oktoba 06, 2018
Brighton v West Ham
Burnley v Huddersfield
Palace v Wolves
Fulham v Arsenal
Leicester v Everton
Liverpool v Man City
Man Utd v Newcastle
Southampton v Chelsea
Spurs v Cardiff
Watford v Bournemouth
Jumamamosi, Oktoba 20, 2018
Arsenal v Leicester
Bournemouth v Southampton
Cardiff v Fulham
Chelsea v Man Utd
Everton v Palace
Huddersfield  v Liverpool
Man City v Burnley
Newcastle  v Brighton
West Ham v Spurs
Wolves v Watford
Jumamosi  Oktoba 27, 2018
Brighton v Wolves
Burnley v Chelsea
Palace v Arsenal
Fulham v Bournemouth
Leicester v West Ham
Liverpool v Cardiff
Man Utd v Everton
Southampton v Newcastle
Spurs v Man City
Watford v Huddersfield
Jumamosi Novemba 03, 2018
Arsenal v Liverpool
Bournemouth v Man Utd
Cardiff v Leicester
Chelsea v Crystal
Everton v Brighton
Huddersfield v Fulham
Man City v Southampton
Newcastle v Watford
West Ham v Burnley
Wolves v Spurs
Jumamosi Novemba 10, 2018
Arsenal v Wolves
Cardiff  v Brighton
Chelsea v Everton
Palace v Spurs
Huddersfield v West Ham
Leicester  v Burnley
Liverpool v Fulham
Man City v Man Utd
Newcastle v Bournemouth
Southampton v Watford
Jumamosi Novemba 24, 2018
Bournemouth v Arsenal
Brighton v Leicester
Burnley v Newcastle
Everton v Cardiff
Fulham v Southampton
Man Utd v Palace
Spurs v Chelsea
Watford v Liverpool
West Ham v Man City
Wolves v Huddersfield
Jumamosi, Desemba 01, 2018
Arsenal v Spurs
Cardiff v Wolves
Chelsea v Fulham
Palace v Burnley
Huddersfield v Brighton
Leicester v Watford
Liverpool v Everton
Man City v  Bournemouth
Newcastle v West Ham
Southampton v Man Utd
Jumanne, Desemba 04, 2018
Bournemouth v Huddersfield
Brighton v Palace
Burnley v Liverpool
Fulham v Leicester
Watford v Man City
West Ham v Cardiff
Wolves v Chelsea
Man Utd v Arsenal
Jumatano Desemba 05, 2018
Everton v Newcastle
Spurs v Southampton
Jumamosi Desemba 08, 2018
Arsenal v Huddersfield
Bournemouth v Liverpool
Burnley v Brighton
Cardiff  v Southampton
Chelsea v Man City
Everton v Watford
Leicester v Spurs
Man Utd v Fulham
Newcastle v Wolves
West Ham v Palace
Jumamosi Desemba 15, 2018
Brighton v Chelsea
Palace v Leicester
Fulham v West Ham
Huddersfield  v Newcastle
Liverpool v Man Utd
Man City v Everton
Southampton v Arsenal
Spurs v Burnley
Watford v Cardiff City
Wolves v Bournemouth
Jumamosi Desemba 22, 2018
Arsenal v Burnley
Bournemouth v Brighton
Cardiff  v Man Utd
Chelsea v Leicester
Everton v Spurs
Huddersfield v Southampton
Man City v Palace
Newcastle  v Fulham
West Ham v Watford
Wolves v Liverpool
Jumamosi Desemba 26, 2018
Brighton v Arsenal
Burnley v Everton
Palace v Cardiff
Fulham v Wolves
Leicester  v Man City
Liverpool v Newcastle
Man Utd v Huddersfield
Southampton v West Ham
Spurs v Bournemouth
Watford v Chelsea
Jumamosi Desemba 29, 2018
Brighton v Everton
Burnley v West Ham
Palace v Chelsea
Fulham v Huddersfield
Leicester  v Cardiff
Liverpool v Arsenal
Man Utd v Bournemouth
Southampton v Man City
Spurs v Wolves
Watford v Newcastle
Jumanne Januari 01, 2019
Arsenal v Fulham
Bournemouth v Watford
Cardiff v Spurs
Chelsea v Southampton
Everton v Leicester
Huddersfield v Burnley
Man City v Liverpool
Newcastle v Man Utd
West Ham v Brighton
Wolves v Crystal Palace
Jumamosi Januari 12, 2019
Brighton v Liverpool
Burnley v Fulham
Cardiff v Huddersfield
Chelsea v Newcastle
Palace v Watford
Everton v Bournemouth
Leicester v Southampton
Man City v Wolves
Spurs v Man Utd
West Ham v Arsenal
Jumamosi Januari 19, 2019
Arsenal v Chelsea
Bournemouth v West Ham
Fulham v Spurs
Huddersfield  v Man City
Liverpool v Palace
Man Utd v Brighton
Newcastle  v Cardiff
Southampton v Everton
Watford v Burnley
Wolves v Leicester
Jumanne Septemba 29, 2019
Arsenal v Cardiff
Bournemouth v Chelsea
Fulham v Brighton
Huddersfield v Everton
Wolves v West Ham
Man Utd v Burnley
Jumatano Januari 30, 2019
Newcastle v Man City
Southampton v Palace
Liverpool v Leicester
Spurs v Watford
Jumamosi Februari 2, 2019
Brighton v Watford
Burnley v Southampton
Cardiff v Bournemouth
Chelsea v Huddersfield
Crystal Palace v Fulham
Everton v Wolves
Leicester v Man Utd
Man City v Arsenal
Spurs v Newcastle
West Ham v Liverpool
Jumamosi Februari 09, 2019
Brighton v Burnley
Palace v West Ham
Fulham v Man Utd
Huddersfield  v Arsenal
Liverpool v Bournemouth
Man City v Chelsea
Southampton v Cardiff
Spurs v Leicester
Watford v Everton
Wolves v Newcastle
Jumamosi Februari 23, 2019
Arsenal v Southampton
Bournemouth v Wolves
Burnley v Spurs
Cardiff v Watford
Chelsea v Brighton
Everton v Man City
Leicester v Palace
Man Utd v Liverpool
Newcastle  v Huddersfield
West Ham v Fulham


TAA Yafuturisha Wafanyakazi, Wadau Wake


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela juzi akiwakaribisha wadau na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo katika futari aliyoiandaa kwenye eneo la karibu na Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1).


Na Mwandishi Wetu
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Bw.  Richard Mayongela amesema amewasamehe wale wote waliomkwaza na kumuudhi katika utekelezaji wa majukumu yake kwa bahati mbaya au kwa makusudi aliteleza kama binadamu.

Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa kufuturu katika futari aliyoiandaa na kufanyika eneo la karibu na Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1), ambapo ilihusisha wafanyakazi wa TAA na wadau wengine wanaofanyakazi mbalimbali na Mamlaka hiyo.

“Naomba tusameheane pale tulipokoseana, sisi ni binadamu hatuko kamili katika namna moja au nyingine tumekwazana katika kutekeleza majukumu yetu, kwa bahati mbaya mimi nikiwa ofisini nakuwa ni Mwajiri na halafu wenzangu upande wa pili wanakuwa waajiriwa, hivyo katika kutekeleza majukumu yetu naweza kuteleza mimi ni binadamu naombeni katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan tusameheane, name nimewasamehe wote,” amesema Bw. Mayongela.

 Imam wa Msikiti ulipo karibu na Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1), Shekh Mahmoud Rajab (mwenye kofia nyekundu), akijumuika pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa tatu kulia) katika futari aliyoandaliwa na Mkurugenzi huyo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Lawrence Thobias.

Hata hivyo, Bw. Mayongela amesema dini zetu siziwe vigezo vya kubaguana, kwa kuwa tunashiriki katika shughuli mbalimbali na kufanya kazi pamoja, ambapo TAA wapo wafanyakazi Waislam na Wakristo, hali kadhalika kwa wadau wa Mamlaka wapo wa madhehebu hayo, na wanafanyakazi pamoja.

Pia Bw. Mayongela amesema ni imani yake wataendeleza yale mema waliyokuwa wakiyafanya kwa kipindi chote cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yakiwemo ya kudumu katika sala na kujinyima na kumlilia Mwenyezi Mungu aweze kutusaidia kwa kila jambo na ndio mtakayoyaendeleza hata baada ya Ramadhan.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), juzi wakijumuika na wadau mbalimbali karibu na Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1) kupata futari iliyoandaliwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela.

Hata hivyo, Bw. Mayongela amesema tukio hili la Iftah liwe ni ishara na mwanzo wa ushirikiano mzuri baina ya TAA na wadau wake wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali kwenye Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo hata vitabu vya dini vinazungumzia ushirikiano, ambapo ametaka asiwepo mtumwa wala mtwana na asiwepo bwanyeye wala bosi, kwa kuwa sisi wote tupo sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na tunahaki sawa.  

“Nawapenda sana ndugu zangu Waislam na ningefurahi zaidi kote kungekuwa na mikeka na tukaa chini hiyo ni ishara wote tupo sawa kwa Mwenyezi Mungu na hakuna wa juu, katikati na chini, kwa sababu kuna maisha baada ya maisha ya hapa Duniani,” amesema Bw. Mayongela.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bw. Hamis Amir (wa kwanza kulia), leo kwa kushirikiana na wafanyakazi wenzake wametoa zawadi mbalimbali za vyakula kwa ajili ya Sikukuu ya Idd kwa Watoto yatima wanaolelewa kwenye Kituo cha Kiislam cha Ilemela.
Pia Bw. Mayongela ametoa shukrani alizopewa na Serikali kwa wadau wote kwa kufanikisha huduma bora kwa ndege kubwa ya Emirates Airbus 380 iliyokuwa ikielekea Mauritius na kutua kwa dharura tarehe 24 April, 2018 kutokana na hali mbaya ya hewa nchini huko, ambapo tukio hilo ni la kihistoria na lilizungumzwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo pia  amefungua milango wazi kwa wadau kufika ofisini kwake kwa lengo la kujenga na kuendeleza viwanja vya ndege Tanzania. 

Naye Katibu Mtendaji wa Chama cha Watoa Huduma za Ndege (TAOA), Bw. Laurence Paul amempongeza Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Bw. Mayongela kwa kuwa wa kwanza kuandaa Iftah hii tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hii mwaka 1999, ambapo imeonesha ni namna gani anaushirikiano na upendo mkubwa kwa wadau wake wote.

“Nimefanyakazi hapa kwa muda mrefu tangu mwaka 1971 ingawa nilikuwa nikihamishwa na kurudishwa tena hapa TB1, lakini sikuwahi kuona kiongozi aliyetukutanisha kwa jinsi hii, Mkurugenzi mkuu umetuweka karibu na unatambua kuwa ukaribu wa wadau wako ndio wepesi wa kazi yako, kwani tukiwa hatuko karibu itakuwa shida kwako kutuongoza, hivyo napenda kukupongeza kwa kuwa na mawazo haya ya kutuleta pamoja,” amesema Bw. Paul.

Bw. Paul amesema hatua hii ya Iftah pamoja itasaidia kuweka wadau pamoja na kuweka usalama Kiwanja kwani kinauzika kutokana na kuwa na usalama.

Bi. Doris Uhagile, Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, akimkabidhi moja ya katoni ya maji ya kunywa kwa mmoja wa wazee wanaolelewa kwenye Kituo cha Kiilima mkoani hapa, ambapo walisherehekea pamoja katika Sikukuu ya Idd inayofanyika leo.

Kwa upande wa Imam wa Msikiti ulipo karibu na Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1), Shehe Mahmoud Rajab naye amemshukuru Mkurugenzi Mkuu na kumuombea dua ili aendelee na adhima yake ya kuwaleta wadau pamoja, ambapo haijawahi kutokea.

“Tunashukuru kwa uhusiano huu wa Mkurugenzi huyu mpya kwani haijawahi kutokea kuunganisha watu namna hii, na tunashukuru na sisi Waislam tunasehemu ya kuabudia tukiwa maeneo ya kazi kwani kule Njiapanda ni mbali sana, tunashukuru sana ten asana,” amesema Imam huyo.

Monday 11 June 2018

Huku Kwetu DStv Mambo ni Motoooo!


Na Mwandishi Wetu
ZIKIWA zimebaki siku tatu tu kabla ya kuanza kwa fainali za Fifa za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, mambo yanazidi kunoga.

DStv watakuwezesha wewe mteja wao kufurahia mechi zote 64 za michuano ya FIFA Kombe la Dunia 2018 LIVE zikiwa kwenye picha ang’avu HD kupitia chaneli zake mpaka 6 maalum zilizoandaliwa kwa ajili ya mchuano hii. Wateja wote wa DStv watafurahia mashindano haya kuanzia kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 tu!

DStv pia imekuandalia matangazo ya moja kwa moja ya FIFA Kombe la Dunia 2018 kwa Lugha ya Kiswahili utakaoletwa kwenu na timu yetu mahiri ya wachambuzi Nguli wa soka kutoka hapa nchini akiwamo Oscar Oscar, Maulid Kitenge, Aboubakar Liongo, Ibrahim Maestro, Edoku Mwembe, bila kumsahau Ephraim Kibonde watakaokuletea matangazo haya LIVE kutoka Russia.

Kwa kuongezea, DStv imekuleta ofa maalum kwa wateja wake wapya, Sasa wataweza kujiunga na DStv kwa shilingi 79,000 tu na kupata seti ya DStv pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure kitakachokuwezesha kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia LIVE mechi zote 64 kupitia chaneli za supersport .

Mbali na ofa hiyo na kutangazwa kwa michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili, DStv inataka kuhakikisha kuwa wateja wanaweza kutazama DStv popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, laptop na tablet.  Download App yetu ya “DStv Now”, unaweza kutumia hadi vifaa vitano tofauti ambavyo vyote huunganishwa na dikoda yako hivyo kuwawezesha wanafamilia kutazama vipindi tofauti  wakiwa sehemu yoyote kwa kutumia vifaa vyao.

Kujiunga wasiliana nao kwa namba 0659 070707
Wanasema “Kama Sio DStv Potezea”!!


Thursday 7 June 2018

Makocha Simba Sport Club Wabwaga Manyanga


Na Mwandishi Wetu, Nakuru
WAKATI Simba imetinga fainali ya mashindano ya SportsPesa Super Cup, swali ni je wameachana na makocha wao baada ya leo kuwa katika jukwaani wakishuhudia timu yao ikishinda kwa penalti 5-4 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Kocha Mkuu, Pierre Lechantre na kocha wa viungo wa timu hiyo kutoka Morocco, jana walishuhudia pambano hilo kutokea jukwaani na taarifa zilidai kuwa tayari wameachana na timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wao.

Hatahivyo, taarifa zingine zilidai kuwa, Mfaransa Lechantre ametofautiana na uongozi wa Simba na hivyo hawako tayari kumuongezea mkataba mwingine, licha ya kuipatia mafanikio timu hiyo hadi kuipatia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyoukosa kwa karibu miaka mitano.

Hatahivyo, hakuna kiongozi wa Simba aliyekuwa tayari kulizungumzia hilo, lakini walisema wangekuwa na kikao jana usiku na taarifa kamili wangezitoa baadae.

Timu hiyo jana ilikuwa chini ya kocha msaidizi Mburundi Masoud Djuma, ambaye ndiye akapewa mikoba hiyo.

Wakati huohuo, Singida United ya Tanzania jana ilitolewa katika mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kulambwa mabao 2-0 na mabingwa wa Kenya katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Afraha mjini hapa.

Kwa kipigo hicho, Singida United wanaungana na mabingwa wazamani wa Tanzania Bara, Yanga na JKU ya Zanzibar kuyaaga mashindano hayo baada ya kutolewa katika nusu fainali, Yanga na JKU wenyewe walitolewa katika robo fainali.

Mabao yote ya Gor Mahia yalifungwa na Meddy Kagere katika kila kipindi na kuifanya timu hiyo kujihakikishia nafasi ya kucheza dhidi ya Simba katika fainali itakayopigwa Jumapili kwenye uwanja huo.