Saturday, 7 March 2015

Marseille yaipiku Paris St-Germain Ligue 1PARIS, Ufaransa
TIMU ya Marseille jana imepaa hadi nafasi ya pili na kuwa nafasi moja juu ya Paris St-Germain katika Ligi Kuu ya Ufaransa kwa tofauti ya mabao baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wake.

Michy Batshuayi aliiweka Marseille katika mstari wa kushinda mchezo wa kwanza baada ya mechi tano kabla Baptiste Aloe hajafunga na kuifanya timu hiyo kuwa mbele kwa bao 2-0.

Bao la kujifunga la Francois Moubandje la lile la pili la Batshuayi liliifanya Marseille kuwa mbele kwa 4-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Wissam Ben Yedder aliifungia timu yake bao la kufutia machozi lakini Andre Ayew alijibu mapigo kabla Andre-Pierre Gignac hajafunga bao lake la 16 msimu huu.

Marseille sasa wana pointi moja nyuma ya vinara Lyon, ambao kesho Jumapili watacheza na Montpellier, wakati PSG watakuwa nyumbani wakicheza na Lens leo Jumamosi.

No comments:

Post a Comment