ABIDJAN, Ivory Coast
KIPA wa timu ya
taifa ya Ivory Coast au Tembo kama inavyojuliana sana Boubacar Barry ametangaza
kustaafu soka la kimataifa, chini ya mwezi mmoja baada ya kuiwezesha nchi hiyo
kutwaa taji la Mataifa ya Afrika.
Barry, 35, alifanya
kazi kubwa katika fainali wakati tembo hao wakiwachapa Ghana kwa penati na
kutwaa taji hilo Februaria 8 mwaka huu.
Kipa huyo aliokoa
penati mbili wakati wakupigiana penati kabla hajafanya kazi ya ziada kufunga ya
ushindi iiyowapatia taji Ivory Coast.
"Vitu vyote
vizuri lazima viwe na mwisho. Nimeamua kumaliza kipindi change ca kuichezea Ivory
Coast. Nilikuwa najiunia kuvaa jezi ya nchi yangu, " alisema Barry katika
ukurasa wake wa Facebook.
Barry ameichezea
Iory Coast mechi 86 na kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia mara taty,
yaani 2006, 2010 na 2014.
Pia kipa huyo
alikuwa langoni mwaka 2012 wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika
ambako Ivory Coast ilifungwa na Zambia kwa penati.
No comments:
Post a Comment