Monday, 30 March 2015

Tiger Woods aporomoka kiubora wa viwango 
NEW YORK, Marekani
TIGER Woods ameporomoka kiviwango na kwa mara ya kwanza amejikuta yuko nje ya wachezaji 100 bora katika historia ya maisha yake.

Mshindi huyo mara 14 wa mashindano makubwa, ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa katika nafasi ya 100 mwaka 1996 na na baadae kutumia wiki 683 kuwemo katika nafasi ya kwanza duniani, ameporomoka hadi katika nafasi ya 104.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 39, hajacheza tangu alipojitoa katika mashindano ya Farmers Insurance Open Februari 6.

Woods alisema "anatumaini" ya kurejea katika shindano kubwa la kwanza la mwaka, the Masters, litakaloanza Aprili 9.

Baada ya kujitoa katika shindano hilo la Februari huko Torrey Pines kutokana na maumivu ya mgongo, Woods alitangaza kupumzika mchezo huo kwa muda usiojulikana, akielezea kiwango chake mwaka huu kama "hakikubaliki katika mchezo huo ".

No comments:

Post a Comment