![]() |
Uhaba wa vifaa noma! Mwinga Mwanjala akitumia leki kama mkuki wakati wa kuwafundisha walimu (hawapo pichani) jinsi ya kurusha mkuki wakati wa mafunzo hayo. |
Na Cosmas Mlekani
UKISTAAJABU ya Mussa autayaona ya filauni!
Usemi huo umedhirika mapema leo mchana wakati baadhi ya walimu wa
shule za msingi mkoa wa Dar es Salaam walipokuwa wakipewa mafunzo ya mchezo wa
riadha waliporusha mawe badala ya tufe
.
Mafunzo haya ambayo yalishirikisha zaidi ya walimu 40 wa shule
mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam ambapo mbali na riadha pia yalishirikisha
michezo mingine kama mpira wa mikono, netiboli, wavu na soka.
Hatahivyo, kihoja hicho kilikuwa kwa walimu kama sita waliokuwa
wakihudhuria mafunzo ya riadha, ambapo kasheshe iliibuka pale walipoanza
kufundishwa mazoezi ya vitendo kwenye uwanja wa shule ya Msingi ya Ali Hassan Mwinyi
Magomeni.
Mafunzo hayo yalikuwa kuwaandaa walimu kwa ajili ya Michezo ya
Shule za MsingiTanzania ya Umitashumta itakayofanyika baadae mwaka huu.
Katika mchezo wa riadha mwanariadha wa kimataifa wa zamani wa
Tanzania Mwinga Mwanjala ilimbidi kutumia mawe kuwaonesha waliu hao tufe
lilivyo na linavyorushwa.
Mbali na kihoja hicho cha tufe pia ajabu jingine lilitokea wakati
walimu wakioneshwa jinsi ya kutupa mkuki, ambapo badala ya kutumika kifaa
hicho, badala ya ilitumika leki ya chuma ya kutolea uchafu, ambayo ilionekana
wazi kuwapoteza mwelekeo walimu hao kutokana na uzito wa leki hiyo ya chuma.
Mafunzo hayo ya siku tano ambayo yanamalizika Ijumaa, mbali na
Mwanjala katika riadha mkufunzi mwingine alikuwa Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania
(RT) Suleiman Nyambui.
![]() |
Mwinga Mwanjala akiwaonesha walimu jinsi ya kurusha tufe akitumia jiwe kutokana na uhaba wa vifaa. |
![]() |
Washiriki wa semina ambao ni walimu wakiwa katika mafunzo ya vitendo ya kutupa tufe. |
No comments:
Post a Comment