Monday, 9 March 2015

Ijue rasimu ya Katiba ya Riadha Tanzania (RT)

 *Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuijadili Jumamosi Morogoro Nane Nane

Rais wa Riadha Tanzania Anthony Mtaka.
SEHEMU YA KWANZA TAFSIRI, JINA NA MADHUMUNI 1. TAFSIRI Katika Katiba hii, isipokuwa pale panapoeleza vinginevyo, maneno yafuatayo yanamaana kama ilivyoainishwa hapo chini:
1) AAC –Ina maana, Shirikisho la Riadha Afrika.
2) ATAT-Ina maana, Baraza la Usuluhishi la RT.
3) BMT-Ina maana, Baraza la Michezo Tanzania.
4) EAAR –Ina maana, Shirikisho la Riadha Afrika ya Mashariki.
5) Familia ya Riadha –Ina maana,inahusisha wanachama na wasio wanachama wa RT,wote ni wadau kwa njia moja au nyingine wa Riadha wanaotambuliwa na RT, kama Vyama vya Riadha,Vilabu vya Riadha,Promota,wawakilishi wa wachezaji,wachezaji,wachezaji wastaafu,wakufunzi n.k
6) IAAF –Ina maana, Shirikisho la Riadha Duniani.
7) Kamati ndogo-Ina maana Kamati mbalimbali zilizoanzishwa kwa mamlaka ya katiba hii.
8) Kanuni – Ina maana kanuni ambazo zimeainishwa katika ibara ya 38 ya katiba hii.
9) Kanuni ya Domicile –Ina maana, Makazi ya kudumu ya Mwanariadha kwa wakati huo.
10) Katiba –Ina maana, Katiba ya RT. Nyongeza, kanuni na sheria ndogo za RT ni sehemu ya katiba hii.
2
11) Mashindano baina ya Mikoa-Ina maana, mashindano yanayohusisha timu kutoka mikoa zaidi ya miwili wanachama wa RT.
12) Mashindano ya Mikoa-Ina maana, mashindano yanayoandaliwa na vyama vya mikoa.
13) Mashindano ya Taifa-Ina maana, mashindano yanayoandaliwa na RT yanayohusisha timu za vyama vya mikoa nchi nzima.
14) Mbio za Taifa za Ndani-Ina maana, Mbio za ndani za Taifa zinazoandaliwa na RT, zaidi ya wanariadha watatu wa Taifa kutoka vyama vya mikoa na mkoa mwenyeji, hushiriki.
15) Mfanyakazi-Ina maana Katibu Mkuu aliyeajiriwa, wafanyakazi mbalimbali, watakaoteuliwa kwa muda mfupi ama mrefu, Katibu Mkuu aatakavyo ainisha kwa maandishi kwa ridhaa ya Kamati ya utendaji.
16) Mkutano Mkuu (AGM) – Inamaana mkutano mkuu wa mwaka kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 14 (1) ya Katiba hii.
17) Mkutano wa Dharura (SGM) – Huu ni mkutano mkuu wa wa dharura kama ulivyoainishwa katika ibara ya 14 (2) ya Katiba hii.
18) Mkutano Mkuu wa Uchaguzi (QGM) – Hii inamaana, mkutano mkuu wa uchaguzi kama ilivyoainishwa katika ibara ya 18(2) ya katiba hii.
19) Mwanachama – Mwanacha wa RT kama ilivyoainishwa katika ibara ya 9 ya katiba hii.
20) Mwanariadha-Ina maana, mtu yoyote anayeshiriki katika mashindano yaliyoandaliwa na RT, wanachama wake na mwenye namba ya leseni ya RT.
21) Mwanariadha wa Taifa-Ina maana, ni mwanariadha ambaye jina lake lipo kwenye Orodha ya wanariadha wa Taifa.
3
Mwanasheria wa RT Thabit Bashir ndiye muandaaji wa rasimu hii.

22) Promota-Ina maana muandaaji, mhamasishaji, mdau wa mashindano ya aina mbalimbali ya Riadha.
23) Riadha ina maana,Mashindano ya Ndani,Mbio za Barabarani, Mbio za Kutembea, Mbio za Nyika (ikiwemo Milimani)
24) RT – Ina maana,Riadha Tanzania(Athletics Tanzania)
25) Sheria Ndogo-Ina maana,sheria zote ndogo ambazo zimeainishwa katika ibara ya 38 ya katiba hii.
26) Shirikisho-Ina maana,Shirikisho la Riadha Tanzania (RT)
27) TOC –Ina maana,Kamati ya Olimpiki Tanzania
28) Uanachama Shirikishi-Ina maana, vyama vya kitaifa vilivyosajiliwa nchini Tanzania na vinajihusisha na Riadha kama ilivyoelezwa katika ibara ya 5(2)(a) ya katiba hii.
29) Uanachama Taasisi-Ina maana, taasizi za kitaifa elimu, ulinzi na usalama zinazojishughulisha na Riadha kama ilivyoainishwa katika ibara ya 5(2)(b) ya katiba hii.
30) Wizara-Ina maana, wizara ambayo kwa wakati huo inajishughulisha na Michezo.

Katibu Mkuu wa RT Suleiman Nyambui
4
2. JINA, KUJISHIRIKISHA NA LUGHA RASMI
1) Jina la Shirikisho litakuwa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) (Kiingereza Athletics Tanzania Federation (AT).
2) RT ni Shirikisho la Riadha lililosajiliwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Sheria ya mwaka 1967 ya Baraza la Michezo Tanzania na kurekebishwa mwaka 1971.
3) RT itabakia kuwa shirikisho la Riadha lisilo na mfungamano wa kisiasa na kijamii na mtu yoyote ama chama katika Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.
4) RT itakuwa na mamlaka ya kisheria na pia,kupitia wawakilishi wake walioidhinishwa:
a) kuwa na mamlaka ya kipekee nje ya wanachama na wafanyakazi;
b) kuwa na haki ya kumiliki, kuzuia ama kuuza mali inayoondosheka na isiyoondosheka;
c) kuwa na haki na majukumu kisheria nje ya wanachama na wafanyakazi wake;
5) Haki ya kuingia katika mabadilishano ya kisheria,kufungua ama kujitetea katika shauri lolote kwenye vyombo vya sheria;
6) RT ni shirikisho pekee linalosimamia na kuendeleza mchezo wa Riadha ndani ya mipaka ya Tanzania;
7) RT ni Shirikisho pekee la Riadha la Tanzania linalojishirikisha na:-
a) Baraza la Michezo la Taifa (BMT);
b) Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC);
c) Shirikisho la Riadha la Afrika Mashariki (EAAR);
d) Shirikisho la Riadha la Afrika (AAC);
e) Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF)
8) Makao makuu ya RT yataanzishwa katika kusimamia shirikisho kwa ufanisi kutokana na sera za Shirikisho lenyewe. Kamati ya Utendaji itatoa mapendekezo ya makao
5
makuu kulingana na mikataba ya pango na umiliki wa mali zisizoamishika wa shirikisho;
9) RT itakuwa na majukumu yote ya maendeleo ya Riadha Tanzania;
10) Lugha rasmi ya RT itakuwa Kiswahili na Kingereza, lugha hizi zitatumika katika mawasiliano mbalimbali ya shirikisho;
11) Katika mkutano mkuu,lugha itakayotumika itakuwa Kiswahili ama kingereza, itakapotokea mgongano wa tafsiri, kingereza kitachukuliwa kama ndiyo maana iliyokusudiwa;
3. DIRA NA MADHUMUNI
1) Dira
Kutoa mchango katika ujenzi wa Taifa na maendeleo ya nchi yetu Tanzania, muendelezo chanya wa jamii yetu kupitia maendeleo ya mchezo wa Riadha, kuanzia chini hadi kufikia kiwango kikubwa cha mafanikio;
2) Madhumuni
Katika kufanikisha hii Dira, madhumuni yafuatayo yanachukuliwa kama msingi wa programu mbalimbali za RT:
a) Kuanzisha mahusiano mazuri baina ya wanachama wote kwa faida ya Riadha,kuwa na ufanisi,uongozi mzuri na ushirikiano wenye tija baina ya wanachama na kutangaza wanariadha na riadha kwa ujumla nchini Tanzania;
b) Kuendeleza, Kutangaza, kusimamia na kulinda mchezo wa Riadha nchini Tanzania;
c) Kuboresha na kuendeleza mfumo wa vilabu na vyama vya mikoa nchini Tanzania, ushiriki, ufundishaji, ufundi katika kusimamia mchezo na shughuli nyingine za RT kwa jamii nzima ambayo inapenda kushiriki Riadha,na wale wanaotimiza sifa za uanachama wa Shirikisho;
d) Kuendelea kuhakikisha hakuna ubaguzi wowote,uwe wa rangi,kabila,dini,jinsia ama vinginevyo katika mchezo wa Riadha na

Makamu wa Pili wa Rais RT Dr.Hamad Ndee.
6
kuwa na juhudi za makusudi katika kuhakikisha ubaguzi wowote hautokei;
e) Kutengeneza na kuimarisha kanuni na sheria mbalimbali zinazoendesha mchezo wa Riadha nchini Tanzania kutokana na katiba ya IAAF;
f) Mafunzo ya waamuzi wa Riadha kwa kuwaendeleza kupitia kozi za vitendo na nadharia,mitihani kwa kila mwenye nia ya kushiriki itayopelekea kusajiliwa kama muamuzi waliofuzu,mafunzo haya yatakuwa na nia ya kuhakikisha upatikanaji wa kutosha wa waamuzi katika michezo ya Riadha;
g) Mafunzo kwa wakufunzi katika mfumo unaowaandaa makocha wapya na kozi za upili kama muendelezo wa taaluma yao ili kuweza kusajiliwa kama makocha waliofuzu,mafunzo haya yatakuwa na nia ya kuhakikisha upatikanaji wa kutosha wa wakufunzi katika mchezo wa Riadha;
h) Kuunganisha Riadha Tanzania kwa:
i. Kujivunia rangi za Taifa;
ii. Ushirikiano wa nje na kujishirikisha na TOC, BMT, EAAR, AAC, IAAF na chama kingine chochote cha ndani na nje kinachohusiana na Riadha;
iii. Kutoa leseni kwa wanariadha;
iv. Kusimamia Riadha katika viwango vyote;
v. Kujitayarisha kwa ajili ya mashindano yote ya ndani na nje ya nchi;
vi. Kupanga mamlaka ya vyama vya mikoa vya Riadha;
vii. Programu za maendeleo;
viii. Mengineyo
i) Maboresho ya kanuni zinazosimamia riadha na sifa za mwanariadha kushiriki katika mashindano;
7
j) Kujitayarisha kwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Riadha kimataifa, kusimamia mashindano ya kimataifa yanayofanyika Tanzania na udhamini kwa timu zinazokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa;
k) Kutangaza juhudi za kujituma,heshima kutokana na mashindano yaliyo na usawa, ikiwemo haki ya kila mchezaji kushiriki na kushinda mashindano ya kitaifa bila kizuizi cha uongozi, maamuzi ama vinginevyo;
l) Kuitangaza michezo ya Riadha na Mashindano kupitia kwa wanachama ili kuhakikisha ushiriki sawa na wa haki kwa wachezaji wote kwenye mashindano mbalimbali kwa makundi yote ya umri kutokana na dira na Madhumuni ya shirikisho;
m) Uangalizi mkubwa wa mazingira ya wanariadha na kuwaeleza mambo ambayo yanaweza kuwa hatarishi kwao ikiwemo uwakilishi wao katika kupambana na mambo hayo;
n) Kutangaza mashindano baina ya mikoa na mikoa,ya kimataifa na ushiriki wao katika madaraja yote ili kutoa unafuu kwa wanariadha katika kufanikisha vipaji vyao;
o) Kuonyesha na kufanikisha mahitaji mbalimbali ya Kukuza, kuendeleza na kusimamia Mchezo wa Riadha pamoja na shughuli zote zinazohusu mchezo wa Riadha nchini. na maendeleo na matumizi bora ya miundombinu ya Mchezo wa Riadha;
p) Kushiriki katika masuala mbalimbali ya shirikisho la kimataifa la Riadha na vyama shiriki katika Kukuza na kuendeleza Mahusiano ya Kimataifa;
q) Kupambana ili kupata muunganiko na muendelezo wa Riadha katika madaraja yote;
r) Kusimamia Kanuni za IAAF zinazopinga matumizi ya madawa haramu kwa;
8
i. Kufanya uchunguzi nje wa matumizi ya madawa haramu katika mashindano na kuituma IAAF kila mwaka;
ii. Kukubaliana na mahitaji ya IAAF katika kufanya uchunguzi wa madawa ya kuongeza nguvu katika mashindano ya kitaifa na mashindano mengine,na;
iii. Kukubaliana na mahitaji ya IAAF katika kufanya uchunguzi wa madawa ya kuongeza nguvu nje ya mashindano kwa wanariadha waliosajiliwa na shirikisho;
iv. Kuifanya riadha kuwa rahisi kwenye vifaa,mashindano,ufundishaji,uamuzi,usimamizi n.k, kwa watu wote wa Tanzania bila kuangalia jinsia,rangi,dini ama mahali walipotokea,yote kwa lengo la kufurahia na mafanikio;
s) Maendeleo ya mchezo huu katika daraja la juu la mafanikio;
t) Kuwa na madhumuni mengine kama yafuatayo;
i. Kufanikisha madhumuni yote yaliyomo ndani ya katiba hii;
ii. Kuweka usawa wa maendeleo ya Riadha mikoani kwa kuufanya mchezo wa Riadha kushirikisha zaidi makundi yasiyopewa kipaumbele nchini Tanzania;
A. Wanawake,na;
B. Walemavu;
C. Kufanya mchezo wa Riadha kushirikisha watu kwa urahisi kwa madhumuni ya kufurahia na mafanikio, ndani na nje ya
9
nchi, kwa watu wote nchini Tanzania bila ubaguzi wowote;
D. Kutoa burudani kwa wanariadha na jamii kwa ujumla kupitia riadha;
E. Kuifanya Riadha kuwa mchezo namba moja Tanzania;
u) Kushikilia thamani zifuatazo,kama;
i. Haki binafsi za mtu kama zilivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
ii. Kuisimamia RT kama biashara ambayo;
A. Yenye taaluma ya juu;
B. Yenye uwezo wa kifedha;
C. Yenye kuwajibika kwa wanachama wake, na;
D. Kuwa na uhusiano mzuri kwa familia ya wanariadha na jamii kwa ujumla,na;
E. Yenye weledi na heshima kwa watu;
10

Makamu wa Kwanza wa Rais RT, William Kalaghe.
4. JINSI YA KUFANIKISHA MADHUMUNI YA SHIRIKISHO. Madhumuni ya RT yatafanikishwa kwa njia zifuatazo, ikiwemo;
1) Kujishirikisha na TOC, BMT, EAAR, AAC, IAAF na vyama vingine vinavyofanana kadri inavyowezekana;
2) Kumiliki, kuzuia ama kuuza mali yenye kuhamishika na isiyohamishika kwa nia ya kufanikisha madhumuni ya shirikisho;
3) Kufuata kanuni na mwenendo wa haki katika kufanikisha madhumuni ya RT;
4) Kukusanya fedha kwa madhumuni mbalimbali, ikiwemo, kushangisha fedha kupitia udhamini wa makampuni, serikali, vyama vya kujitolea na watu binafsi;
5) Kuwa na kanuni na sheria zinazofanana katika usimamizi, uendeshaji na ulinzi wa Riadha Tanzania;
6) Kuwa na kanuni zinazoendana na Katiba hii ya shirikisho;
7) Kusimamia na kupitisha timu zinazochaguliwa kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya nje ya nchi na pia katika mashindano yanayohusisha timu kutoka nje ya nchi kuja kushiriki Tanzania;
8) Kusikiliza na kutaja rufaa inayowahusu wanachama katika kutoa leseni ama adhabu ya kinidhamu kwa mwanariadha ama mwanachama aliyekatika kamati mbalimbali;
9) Kuweka kumbukumbu mbalimbali ushiriki wa wanariadha wote waliosajiliwa na Shirikisho;
10) Kuhakikisha mashindano ya mwaka ya Taifa yanafanyika;
11) Kuunganisha umma kupitia Riadha,kulinda rangi za Taifa na kusajili nembo ya Shirikisho;
12) Kuweka, kuhifadhi na kuwekeza thamani na fedha za shirikisho katika kutangaza dira na madhumuni kuwa yanafanikiwa;
13) Kutokana na kifungu cha 3.2 (r);
a) Kuhakikisha matumizi ya madawa haramu hayatumiki katika Riadha kwa kufanya kwa
11
makusudi uchunguzi wa nje wa madawa yasiyoruhusiwa katika mashindano;
b) Kuhakikisha njia za kuzuia matumizi ya madawa haramu michezoni, zinatumika katika mashindano yote ya Shirikisho;
c) Kuhakikisha uchunguzi wa nje wa matumizi ya madawa haramu michezoni, unafanyika katika mashindano yote ya Shirikisho;
14) Kujihusisha katika shughuli mbalimbali ambazo zitafanikisha madhumuni chanya ya Shirikisho;
15) Kutoa majukumu kwa vyama vya mikoa katika kusajili na kutoa leseni kwa wanariadha ndani ya maeneo yao,kwa niaba ya RT;
16) Vyama vya mikoa vitakuwa na haki ya kuwatumia wanariadha waliowasajili na kuwapa leseni kushiriki kama wanariadha wa mikoa katika mashindano ya Taifa;
17) Mwanariadha aliyesajiliwa hataruhusiwa kushiriki katika mashindano yoyote yasiyothibitishwa na RT au wanachama wake;
18) Mwanariadha asiyesajiliwa hataruhusiwa kushiriki kwenye mashindano yoyote yaliyothibitishwa na RT au kwa ushirikiano wa RT au vyama vya mikoa au wanachama shirikishi;
19) Kila mwanariadha aliyesajiliwa na mwanachama yoyote wa mkoani wa RT atasimamiwa na kanuni,sheria mbalimbali na Katiba hiii.
12
SEHEMU YA PILI UANACHAMA
5. Aina za Uanachama:
Kutakuwa na aina kuu mbili (2) za uanachama wa shirikisho la RT;
1) Uanachama wa moja kwa moja;
a) Wanachama wa Mikoa (vyama vya mikoa), majukumu yao ni kusimamia na kuitangaza Riadha ndani ya mipaka yao ya mikoa;
b) Wanachama binafsi, hawa ni wale wenye nyadhifa/nafasi za kiofisi kama waliopo katika kamati ya utendaji,wajumbe wa heshima na wajumbe wa EAAR, AAC na IAAF wanaoishi Tanzania.
2) Uanachama usio wa moja kwa moja;
a) Uanachama Shirikishi: Shirikisho la Riadha litakuwa na wanachama shirikishi watakaotoka kwenye vyama vilivyosajiliwa kitaifa vinavyojishughulisha na Riadha;
b) Uanachama Taasisi: Shirikisho la Riadha litakuwa na wanachama wa Taasisi watakaotoka katika taasisi mbalimali za kitaifa za elimu, vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania.
6. VIGEZO VYA KUKUWEZESHA KUPATA UANACHAMA 1) Uanachama utapatikana kwa maombi rasmi, kila maombi ya Uanachama wa RT utaambatanishwa na;
a) Tamko linaloonyesha kuwa, mwombaji yupo katika eneo ambalo RT ina mamlaka kikatiba, kama ni chama cha mkoa, ofisi kuu iwemo ndani ya mkoa huo;
13
b) Tamko linaloonyesha muundo wa kisheria wa muombaji unaohakikisha kuwa kuna uwezo wa kutoa maamuzi huru yanayohitajika kutokana na ushiriki kwa shirikisho;
c) Tamko kwamba muombaji anatambua kamati ya nidhamu, ya rufaa ya RT, Baraza la Usuluhishi la Michezo Tanzania kama ilivyoelezwa katika katiba hii;
d) Tamko kwamba mwanachama atalipa ada ya kila mwaka ya uanachama;
2). Wanachama wote waliokuwepo kabla ya kupitishwa kwa katiba hii wataendelea kuwa wanachama wa RT kama watakuwa wametuma Matamko yaliyotajwa katika ibara 6(1)(a),(b),(c),(d) na 7(2) ya katiba hii; 3) Mwanachama asiyetimiza masharti hapo juu atasimamishwa katika kupiga kura kwenye mkutano mkuu; 4) Kila muombaji atatuma maombi ya uanachama kulingana na ibara ya 7 ya katiba hii.
14
7. JINSI YA KUPATA UANACHAMA. 1) Maombi ya uanachama wa Shirikisho yanatakiwa kuwa kwa maandishi na yatumwe kwa katibu mkuu; 2) Maombi yaambatane na yafuatayo;
a) Nakala ya katiba ya mwombaji na kanuni;
b) Idadi ya viongozi, waliothibitishwa kuweka sahihi,wenye haki ya kuingia katika mikataba mbalimbali;
c) Tamko kuwa muombaji amekubali kusimamiwa na kuongozwa na katiba hii, kanuni, muongozo na mabadiliko yajayo na maaamuzi ya RT, AAC na IAAF;
d) Tamko kuwa muombaji atahakikisha kuwa katiba hii inaheshimika na wanachama wake au mtu yoyote ( Mwanariadha au Muamuzi) ambaye ana mkataba naye;
e) Tamko kuwa mwombaji anatambua uanzishwaji wa mamlaka ya kutatua migogoro inayohusu mchezo wa Riadha;
f) Nakala ya maelezo ya mkutano mkuu ama mkutano wa kikatiba.
3) Katibu mkuu atapeleka maombi ya uanachama katika kamati ya utendaji ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa maamuzi ya maombi;
15
4) Uanachama uliotolewa na kamati ya utendaji ni lazima upelekwe kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kupitishwa;
5) Kwa dhumuni la ushiriki katika mashindano yaliyothibitishwa na RT, mwanachama anatakiwa kuthibitisha kuwa wanariadha wake wamekubali kufanyiwa uchunguzi ndani na nje wa matumizi ya madawa haramu katika mashindano mbalimbali utakaofanywa na RT, IAAF ama mtu yoyote mwenye mamlaka aliyopewa na IAAF/WADA.
8. KUSIMAMISHWA NA KUFUKUZWA Mwanachama yoyote aliyethibitishwa kuhusika katika utovu wa nidhamu au kwenda kinyume na katiba hii,au kwa vitendo vyake,vikaiweka RT au mchezo wa Riadha katika aibu,anaweza kusimamishwa kwa muda usiojulikana mpaka pale shauri lake litakapopelekwa katika kamati ya nidhamu ya RT kwa uchunguzi na maamuzi zaidi. 9. WANACHAMA WA RT 1) Wanachama wa mikoa (Vyama vya mikoa vya Riadha); 2) Wanachama binafsi; 3) Wote wenye nyadhifa/nafasi katika kamati ya utendaji; 4) Wajumbe wa heshima; 5) Wajumbe wa EAAR, AAC na IAAF wanaoishi Tanzania; 6) Wanachama Shirikishi; 7) Wanachama Taasisi;
8) Wanariadha na Waamuzi
16
10. UPIGAJI KURA
1) Bila kuathiri ibara zilizomo ndani ya katiba hii,haki ya kupiga kura katika kuchagua viongozi mbalimbali wa Shirikisho la Riadha itabaki kwa wanachama wa moja kwa moja,wanachama wa mikoa (vyama vya mikoa vya Riadha) na wajumbe wa kamati ya utendaji tu;
2) Mwenendo wa upigaji kura utakuwa kama ulivyoainishwa kwenye ibara ya 17 ya katiba hii;
3) Upigaji kura katika kupitisha maazimio,mapendekezo,mada katika vikao vya AGM na SGM utawahusu wajumbe wa kamati kuu na vyama vya mikoa;
4) Upigaji kura katika kupitisha maazimio,mapendekezo,mada katika vikao vya kamati ndogo utawahusu wajumbe halali wa kamati hizo kama ilivyoainishwa na katiba hii;
5) Matokeo au maamuzi yoyote,yatakayokuwa yamesababishwa na wajumbe wasiostahili katika upigaji kura,yatakuwa siyo halali;
6) Familia ya Riadha iliyoalikwa na Rais wa RT,haitaruhusiwa kuwemo na kushiriki katika upigaji kura,hata hivyo;
a) Watakuwepo katika eneo la upigaji kura,endapo watakuwa wametengewa eneo lao litakalowatofautisha na wapigaji kura halali;
b) Watakuwepo kwa ajili ya kuangalia tu na si vinginevyo;
c) Kamati ya uchaguzi itakuwa na mamlaka ya mwisho ya kuamua wawepo au wasiwepo;
17
11. MIPAKA YA WANACHAMA WA MIKOA. Mipaka ya usimamizi wa wanachama wa mikoa itatokana na mipaka ya kijiografia ya mikoa yetu kwa dhumuni thabiti la kusimamia riadha mikoani kwa kufuata mipaka na kuzuia muingiliano wa kimaeneo. 12. HAKI ZA MWANACHAMA
1) Mwanachama atakuwa na haki ya kuomba uongozi na kuchaguliwa na kuchagua kiongozi katika ngazi yake na kwa mujibu wa katiba hii.
2) Mwanachama atakuwa na haki ya kushiriki vikao vya shirikisho vinavyomhusu.
3) Mwanachama atakuwa na haki ya kushiriki mashindano yote yanayomhusu yatakayoandaliwa na Shirikisho.
4) Mwanachama atakuwa na haki ya kutetea na kuilinda katiba hii ya Shirikisho la Riadha la Tanzania.
5) Haki hizi hazitawahusu wanachama wa heshima.
18
SEHEMU YA TATU SHIRIKISHO 13. MUUNDO WA VIKAO VYA SHIRIKISHO Shirikisho la Riadha la Tanzania litakuwa na muundo wa vikao ufuatao:
1) Mkutano Mkuu
2) Kamati ya Utendaji
3) Kamati mbali mbali
4) Kamati ya kisheria
14. MKUTANO MKUU
1) Mkutano mkuu wa mwaka;
a) Mkutano mkuu ujulikanao kama mkutano mkuuu wa mwaka (AGM) utakuwa ukifanyika ndani ya miezi sita ya mwisho wa mwaka wa fedha wa RT;
b) Mkutano mkuu wa mwaka ndiyo wenye mamlaka ya shirikisho;
c) Wanachama watapewa taarifa siku sitini (60) kabla ya mkutano mkuu wa mwaka;
d) Mada zote zitakazojadiliwa katika mkutano mkuu wa mwaka zinatakiwa kumfikia katibu mkuu siku arobaini na tano (45) kabla ya mkutano huo;
e) Katibu mkuu atawafahamisha wanachama wa moja kwa moja kuhusu ajenda za mkutano siku thelathini (30) kabla ya mkutano huo;
19
2) Mkutano mkuu wa dharura (SGM);
a) Mkutano Mkuu wa dharura unaweza kuitishwa muda wowote na Kamati ya utendaji kwa uamuzi wake,kupokea maombi kwa maandishi kutoka kwa wanachama wa mikoa angalau thheluthi moja ya wanachama wa mikoa,kuitisha mkutano ambbao utatambulika kama mkutano mkuu wa dharura,kujadili jambo lolote ambalo litahitaji uamuzi wa Mkutano Mkuu.
b) Mkutano mkuu wa dharura ulioitishwa kwa kufuata kifungu cha 14.2(a) utafanyika ndani ya siku arobaini na tano (45) baada ya maombi.
c) Mkutano mkuu wa dharura wowote unapaswa kuitishwa kwa maandishi, na taarifa itolewe angalau ndani ya siku ishirini na moja (21) na iambatane na ajenda zake.
15. UWAKILISHI KATIKA MKUTANO MKUU
1) Mkutano mkuu (AGM na SGM) utakuwa na wajumbe wafuatao:-
a) Wajumbe wa kamati ya Utendaji.
b) Wajumbe watatu (3) kutoka Vyama vya Mikoa vilivyo hai, mwenyekiti, katibu na mwakilishi wa mkoa katika mkutano mkuu.
c) Wajumbe wa EAAR, AAC, IAAF wanaoishi Tanzania.
d) Wajumbe wa heshima.
2) Familia ya Riadha itaruhusiwa kuhudhuria katika AGM au SGM, baada ya kupata mwaliko rasmi toka kwa rais wa shirikisho na hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
20
3) Vyama vya mikoa vitaruhusiwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za shirikisho ikiwamo mkutano mkuu wa mwaka kama imetimiza masharti ya ushiriki ikiwemo ada ya uanachama imelipwa yote.
4) Mkutano mkuu utatoa maamuzi sahihi pale tu wengi (50% + 1) ya wanachama wenye haki ya kupiga kura watakuwepo na kuamua.
5) Iwapo akidi haitatimia ndani ya saa moja tangu mkutano uanze rasmi katika eneo ambalo taarifa ilikwishatolewa, basi Mkutano Mkuu utaahirishwa mpaka siku ya pili yake ukiwa na ajenda ile ile na eneo lilelile. Kama akidi haitatimia tena katika mkutano wa siku ya pili, basi wajumbe waliohudhuria watatengeneza akidi.
16. MWENENDO KATIKA MKUTANO MKUU.
1) Katika mkutano mkuu, Rais atasimamia, asipokuwepo, makamu wa rais atasimamia na baadaye makamu wa pili wa rais. Kama wote hawatakuwepo, kamati ya utendaji itamteua mjumbe mmojawapo kusimamia mkutano.
2) Ajenda zifuatazo zitakuwepo katika mkutano mkuu wa mwaka,lakini sio mwisho wa kuongezeka kwa ajenda nyingine;
a) Ukaguzi kuhusu uhalali wa wajumbe.
b) Kusoma taarifa ya Mkutano.
c) Kusoma (kama itahitajika) kupokea kwa taarifa ya mkutano mkuu wa mwaka uliopita na mkutano wowote mkuu wa dharura.
d) Kupokea na kujadili taarifa / maoni/ mada za maendeleo itakayowasilishwa na Kamati ya Utendaji.
e) Kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za mwaka za Shirikisho.
21
f) Kupokea, kujadili na kupitisha mikakati na makisio ya mapato na matumizi ya kipindi kilichopita.
g) Kujadili suala lolote la marekebisho ya katiba Kujadili jambo lingine lolote litakaloletwa kwa taarifa.
h) Uchaguzi wa nyadhifa/nafasi za ofisi kwa kufuata kifungu cha 18 cha katiba hii.
i) Kuthibitisha ukaguzi wa hesabu wa RT.
j) Ajenda za Mkutano mkuu wa dharura (SGM) zitakuwa kama ifuatavyo;
i. Ukaguzi kuhusu uhalali wa wajumbe.
ii. Kusoma taarifa ya mkutano
iii. Kushughulika na jambo lililosababisha mkutano wa dharura uitwe, mambo hayo yatakuwa yameeainishwa kwenye taarifa ya kuita mkutano.
17. UPIGAJI KURA KATIKA MKUTANO MKUU.
1) Upigaji kura katika maazimio/Maoni/mada itakuwa kwa njia ya kunyoosha mkono,ama kwa masanduku ya siri kama wanachama wawili wasiopingwa wameomba.Hata hivyo,kama hitaji la wanachama wawili ama zaidi limepingwa,Rais ama mwenyekiti wa kikao,baada ya ushauri na kamati ya utendaji,atatoa uamuzi juu ya aina ipi ya upigaji kura utumike. Kama kura zimefungamana, Rais ama mwenyekiti wa mkutano atakuwa na kura ya ziada katika kutoa uamuzi. Kifungu hiki hakihusiani na uchaguzi wa nyazifa za ofisi ya shirikisho.
22
2) Wanachama watakuwa na haki ya wingi wa kura zifuatavyo;
a) Wajumbe wa kamati ya utendaji; kura moja (1) kwa kila mjumbe aliyehudhuria.
b) Wanachama wa mikoa; kura moja kwa kila mjumbe aliyehudhuria.
3) Hakuna mwanachama mwenye kupiga kura zaidi ya moja bila kujalisha nyazifa/nafasi za ofisi alizonazo.
18. MAAMUZI NA UCHAGUZI
1) Kutakuwa na mkutano mkuu wa uchaguzi utokanao na mkutano mkuu wa mwaka,kila mwaka wa nne baada ya uchaguzi wa mwisho na utatumia masanduku ya siri ya kura.
2) Mkutano mkuu wa uchaguzi
a) Mpaka itakapobainishwa tofauti na katiba hii,maamuzi ya mkutano mkuu yatakuwa kwa wingi wa kura wa wajumbe wanaostahili kupiga kura katika kuwachagua wajumbe kumi (10) wa kamati ya utendaji,nyazifa za ajira za ofisi na nafasi nyinginezo za RT.
b) Kura zilizoharibika, kura zilizoachwa wazi ama kura isiyoeleweka haitaingizwa katika uhesabuji wa kura halali.
3) Uchaguzi wa Rais,Makamu wa Rais wa kwanza,Makamu Rais wa pili,utafanyika kwa wingi mkuu wa kura (50%+1) zote halali zilizopigwa na wanachama stahili. Hata hivyo, kama kuna wagombea zaidi ya wawili katika nafasi tajwa hapo juu, wagombea wawili waliopata kura nyingi
23
watashindanishwa tena katika awamu ya pili. Awamu hii itaamuliwa kwa wingi wa kura.
4) Maamuzi mengine ya wanachama yataamuliwa kwa kunyoosha mikono.
5) Upigaji kura wa kuagiza ama kwa barua hautaruhusiwa.
6) Maamuzi yaliyoamriwa katika mkutano mkuu yatatekelezwa mara moja isipokuwa pale mkutano mkuu utakapoamua tarehe nyingine ya maamuzi au kukaimu madaraka kwa kamati ya utendaji kwa ajili ya uamuzi.
7) Maamuzi kuhusiana na mabadiliko ya ofisi kuu ya shirikisho, mabadiliko ya katiba, kanuni au maboresho ya ajenda ya mkutano mkuu wa kawaida wa mwaka au kumsimamisha au kumfukuza mwanachama wa shirikisho, au kumpatia heshima, Rais ama mwanachama wa Shirikisho,au kumuondoa mwanachama wa RT au kuivunja RT,maamuzi haya yatahitaji mbili ya tatu (2/3) ya kura ya wamachama halali wa Shirikisho.
19. SIFA ZA MGOMBEA.
Mtu yoyote anayetaka kugombea nyadhifa yoyote katika RT anatakiwa awe na sifa zifuatazo;
1) Awe mtanzania;
2) Awe anajua kusoma na kuandika;
3) Awe na uzoefu uliothibitishwa wa miaka mine katika uongozi wa michezo;
4) Asiwe amepatikana na hatia ya makosa ya jinai ama amehukumiwa kifungo jela pasipo na faini;
24
5) Awe na umri zaidi ya miaka ishirini na moja (21);
6) Awe ameshiriki katika riadha, ukufunzi au uongozi kwa daraja la mkoa;
7) Mtu anayegombea Urais,Umakamu wa kwanza Rais na Umakamu wa pili Rais,awe na uwezo,haiba na thamani ya kuiwakilisha RT ndani na nje ya nchi.
8) Katibu mkuu wa RT atapokea maombi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za shirikisho kwa kutuma fomu za uchaguzi mikoani, zikiwa zimeambatanishwa na taarifa ya kuitisha AGM.
9) Fomu za uchaguzi zilizojazwa zitarudishwa katika ofisi za Shirikisho siku thelathini (30) kabla ya uchaguzi.
10) Majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za shirikisho na sifa zao yataarishwa na kutumwa na shirikisho kwa wanachama wote siku ishirini na moja (21) kabla ya uchaguzi.
11) Patakuwa na mkutano mkuu mmoja wa uchaguzi uliogawanywa katika vipindi viwili,kipindi cha kwanza kuchagua Rais,Makamu wa kwanza wa Rais na Makamu wa Pili wa Rais na kipindi cha pili kwa kuchagua kamati ya utendaji.
12) Wagombea hawatohitajika kuwemo katika QGM.
25
20. KAMATI YA UTENDAJI
Kamati ya Utendaji itakuwa na wajumbe wa kuchaguliwa wafuatao:
1) Rais
2) Makamu wa Kwanza wa Rais
3) Makamu wa pili wa Rais
4) Katibu Mkuu
5) Wajumbe kumi (10) wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi.
6) Wajumbe wawili walioteuliwa na Rais.
21. KAZI ZA KAMATI YA UTENDAJI.
Kamati ya utendaji itakuwa na mamlaka yafuatayo;
1) Kuanzisha sera na maelekezo yanayoendana na katiba hii, kuthibitisha mipango mbalimbali na kupitisha bajeti ya RT.
2) Kuhifadhi maelezo ya kila mkutano wa Kamati ya utendaji.
3) Kuteua kwa pamoja wajumbe wa kamati ya sheria, kamati ya uchaguzi na kamati za kudumu. Hata hivyo, adhabu yoyote itakayotolewa kwa mjumbe wa kamati ya nidhamu au kamati ya uchaguzi itasubiri kupitishwa na Mkutano mkuu.
4) Kupendekeza mtu anayefaa kupewa urais wa heshima ama ujumbe wa heshima kwa ajili ya kupitishwa na mkutano mkuu.
5) Kuchagua walimu wa Taifa wa Riadha wa timu mbalimbali.
6) Kuweza kuteua mtu kuwemo katika kamati ya utendaji kwa muda wote au kipindi kifupi kwa ajili ya jambo maalumu.
26
7) Kuchagua, ndani ya miezi sita (6) baada ya QGM au AGM kamati zote za kudumu za shirikisho.
8) Kuziondoa, pale inapofaa, kamati au kuzichunguza na kushauri kamati juu ya faida mbalimbali za masoko, habari n.k.
9) Kuchukua hatua muafaka kwa mwanachama yoyote katika familia ya Riadha aliyefanya kitendo kinachochafua mchezo wa Riadha.
10) Kuteua wawakilishi kwenda kwa wanachama shirikishi au wanapohitajika mahala pendgine.
11) Kusimamisha kwa muda au moja kwa moja, mtu yoyote, Klabu au mwanachama ambaye ana makosa ya kuchafua shirikisho ama mchezo wa Riadha, au kumrudishia mtu, klabu au mwanachama nafasi yake aliyokuwa nayo kabla ya adhabu.
12) Kupeleka masuala ya kinidhamu kwa kamati ya Maadili, na kutekeleza maazimio ya kamati ya maadili mara moja.
13) Kufanya jambo lolote muhimu kwa faida ya RT, ambalo kimsingi litasaidia kufanikisha maazimio na madhumuni ya Katiba hii.
14) Kuhakikisha ofisi kuu inakuwa na wafanyakazi waliochini ya katibu mkuu,na wanafanya shughuli zote za RT.
15) Kusimamia masuala ya kifedha ya Shirikisho.
16) Kuazima au kukopa fedha kwa masharti nafuu.
17) Kumiliki, kuuza au kununua mali inayoamishika na asiyohamishika.
18) Kuiwakilisha RT katika masuala ya fedha
19) Kulipa madeni baada ya fufikia muafaka.
20) Kukubali kulipa fedha kwa mtu mhusika kutokana na matumizi aliyoingia kwa ajili ya kazi za RT.
21) Kutoa taarifa ya fedha ya mwaka uliopita katika mkutano mkuu wa mwaka
22) Mamlaka ya kuteua Katibu mkuu, mhasibu na wafanyakazi wengine ndani ya RT.
27
23) Katibu Mkuu atakuwa;
a) Mtendaji mkuu wa shirikisho, anayesimamia masuala ya maendeleo ya fedha, utekelezaji wa sera mbalimbali na maamuzi ya kamati ya utendaji. Katibu mkuu atawajibika kwa kamati ya utendaji.
b) Katibu mkuu atakuwa msimamizi mkuu na atawajibika katika masuala mbalimbali ya kiuongozi ya RT.
24) Pia kamati ya utendaji itashughulika na mambo yote ambayo hayajaelekezwa kwa kamati yoyote na mengine iliyopewa na mkutano mkuu.
25) Kwa maamuzi yake, Kamati ya utendaji itatoa mamlaka kwa mtu mwingine katika masuala ya tenda na manunuzi, kulingana na sheria za nchi.
22. VIKAO VYA KAMATI YA UTENDAJI
1) Kamati ya utendaji itakutana kila baada ya miezi mitatu. Kama kuna mahitaji zaiidi, Rais ataitisha kikao cha ziada cha Kamati ya utendaji.
2) Kikao cha kamati ya utendaji kinaweza kuitishwa pale patakapokuwa na maombi zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya wajumbe wa kamati ya utendaji, Rais ataitisha kikao hicho ndani ya wiki mbili tangu ombi lilipotolewa.
3) Ikiwa Kikao cha kamati ya utendaji kimeitwa na wanachama, wanatakiwa kutuma ajenda za mkutano wiki tatu (3) kabla ya mkutano huo kufanyika kwa katibu mkuu wa RT.
4) Ajenda pamoja na tarehe, muda, eneo la mkutano utakaofanyika, vinatakiwa kutumwa kwa wajumbe wote wa kamati ya utendaji siku saba kabla ya uchaguzi.
5) Mkutano wa kamati ya utendaji utakuwa wa usiri,Kamati ya utendaji inaweza kuomba na kupitishwa na rais kualika baadhi ya watu kuhudhuria,lakini kwa ruksa ya Rais ama mwenyekiti wa kikao wataruhusiwa
28
kutoa maoni yao na hawatahusika katika kupiga kura maamuzi yoyote ya kamati ya utendaji.
23. MAAMUZI.
1) Kamati ya Utendaji haitajishugulisha na jambo lolote mpaka akidi iwe 50% ya wajumbe wake.
2) Kamati ya utendaji itafanya maamuzi kwa wingi wa kura wa wajumbe waliopo.Panapotokea mfungamano Rais au mwenyekiti wa Kikao ataamua kwa kura ya kipekee.
3) Mjumbe yoyote wa kamati ya utendaji atatamka kuhusu mgongano wa kimaslahi alionao na kujitoa katika mjadala uliopo ambao unaweza kuathiri maamuzi yake.
4) Nje ya wakati wa kujitoa, wajumbe watakuwa Na haki ya kutoa mawazo yao.
5) Maazimio yatanakiliwa kama maelezo rasmi ya mkutano.
6) Kura zitapigwa kwa kunyoosha mikono.
7) Maazimio yaliyofikiwa na kamati ya utendaji yatatekelezwa mara moja au kusubiri maelekezo zaidi ya kamati ya utendaji.
24. URAIS: RAIS NA MAKAMU WAWILI WA RAIS.
1) Kutakuwa na Rais,makamu wa kwanza wa Rais na makamu wa Pili wa Rais ambao watachaguliwa na Mkutano mkuu wa RT.
2) Rais atakuwa mwakilishi mkuu wa RT.
3) Rais atahusika na majukumu mbalimbali yakiwemo;
a) Kuiwakilisha RT katiak maswala yote na kuwa msemaji mkuu wa RT.
b) Kuitisha Mkutano Mkuu na Mkutano wa kamati ya utendaji.
c) Kuongoza mkutano mkuu na mkutano wa kamati ya utendaji.
d) Kuhakikisha utekelezwaji wa maamuzi yaliyoamuliwa na mkutano mkuu na Kamati ya utendaji.
29
e) Utekelezaji wa kazi za kamati kuu katika kuhakikisha maboresho ya utendaji kazi ya RT.
f) Kuhakikisha kamati mbalimbali za shirikisho zinafanya kazi kwa weledi kwa ajili nya kutimiza madhumuni ya katiba.
g) Kuteua wajumbe wawili wa Kamati ya utendaji.
h) Kupendekeza uteuzi wowote kwa kamati ya utendaji majina ya wajumbe wa kamati ya Sheria,kamati ya uchaguzi na Kamati za kudumu,na;
i) Kuendeleza mahusiano mazuri baina ya wanachama, vyama vingine vya riadha vya nchi za nje, EAAR, AAC, IAAF, mashirikisho mengine, serikali, vyama vya michezo vya kitaifa, wadau wa michezo kwa faida ya mchezo wa riadha.
4) Katika tukio ambalo rais hatokuwepo au kushindwa timiza majukumu yake, Makamu wa Kwanza wa Rais atamsaidia, Makamu wa pili wa Rais, atasaidia kama wenzake wawili hawatakuwepo.
5) Kama Rais ataacha kutekeleza majukumu yake, Makamu wa Rais wa kwanza atakaimu madaraka ya urais mpaka AGM, atakapochaguliwa rais mpya kumalizia kipindi kilichobaki.
6) Makamu wa kwanza wa Rais atakuwa mwenyekiti wa kamati ya Utawala,Fedha na Mipango na Makamu wa Rais wa Pili atakuwa mwenyekiti wa kamati ya Ufundi na Maendeleo.
7) Rais atawapangia makamu wa Rais, majukumu yanayostahili.
25. UWAKILISHI NA SAHIHI.
1) Kamati ya utendaji itaiwakilisha RT kama mhusika wa tatu.Itatoa sahihi pamoja na Rais, mwekahazina na Katibu mkuu.
2) Uteuzi wa kamati,Kamati ya utendaji itakuwa na mamlaka ya kuteua watu wenye uwezo kuunda kamati mbalimbali;
a) Kamati za RT zimegawanyika katika makundi makuu mawili, Kamati za muda na Kamati za kudumu.
30
b) Kamati za muda ni zile ambazo zitaundwa kutokana na mahitaji mbalimbali. Idadi ya wajumbe katika kamati hii zitatofautiana kulingana na mahitaji yenyewe.
c) Kanuni za kuunda Kamati za muda utatofautiana kati ya kamati na kamati kutokana na mahitaji yake;
d) Kamati za muda zitaundwa kutokana na maombi ya;
I. Kamati ya Utendaji
II. Kamati ndogo
III. Katibu Mkuu
e) Kamati ndogo itavunjwa;
I. Mara baada ya kumaliza madhumuni yake;
II. Kutokana na maamuzi ya kamati ya utendaji
f) Kamati za muda zinaweza kupewa hadhi ya kamati ya kudumu, kama hili likitokea, mabadiliko ya katiba sharti yafanyike kutokana na utaratibu wa katiba hii.
g) Kamati za Kudumu, tofauti na kamati za muda, hizi ni za kudumu. Idadi ya wajumbe ni watano, kati yao angalau wawili wawe ni wanawake. Zifuatazo ni kamati za kudumu zinazoweza kuundwa;
I. Kamati ya Utawala,Fedha na Mipango
II. Kamati ya Wanawake na vijana
III. Kamati ya Wakufunzi
IV. Kamati ya Ufundi na Maendeleo
V. Kamati ya Sayansi na Tiba
VI. Kamati ya Nidhamu
VII. Kamati ya Mashindano
VIII. Kamati ya Uenezi na Masoko
IX. Kamati ya Ukaguzi wa Fedha
X. Kamati ya Matembezi
31
3) Mapitio juu ya namna ya kuunda kamati za kudumu yatakuwa yakifanyika kwa nia ya kuboresha, Kamati zote hazitakuwa na nguvu, mpaka zitakapothibitishwa na kamati ya utendaji.Kamati za kudumu zinaweza kurekebishwa kwa uwezo wa kamati ya utendaji.
4) Tamko la mgongano la kimaslahi.
a) Kila mtu aliye na nyazifa katika RT ,mjumbe wa kamati yoyote ya RT kwa kuzingatia mashindano yoyote yatakayoandaliwa kwa ubia na RT,au vyama vya mikoa,wanachama shirikishi au klabu,watatakiwa kutoa tamko la kimaslahi(iwe kwa mbali au moja kwa moja) kwa maandishi,kwenda kwa kamati ya utendaji,kuhusu maslahi waliyonayo kwenye mapendekezo ya mkataba au biashara enye kufikiriwa na RT au kamati,na atazuiwa kujadili,kupiga kura kwa jambo husika.
b) Haitaruhusiwa kwa mtu aliyeshika nyazifa/nafasi za RT au kamati za kifungu cha 27.2(g), kutumia taarifa taarifa zozote ambazo amezipata kwa kuwa na nyazifa hiyo, kwa maslahi binafsi.
c) Kifungu hiki hakitazuia kwa mwanachama wa RT au mjumbe wa Kamati yoyote ya RT kufanya jambo lolote lenye nia nzuri kwa manufaa ya RT.
d) Zawadi, Bahashishi na faida yoyote atakayopokea mwanachama, ikiwemo mjumbe wa kamati yoyote ya RT kutoka kifungu cha 27.2(g), thamani yake ikiwa zaidi ya Tshs 50,000 itatakiwa kutolewa tamko na RT. Kamati ya Utendaji inaweza kuchukua hatua zaidi, ikibainika, Zawadi, Bahashishi au Faida zinadhumuni la kuchafua heshima ya RT, kama mjumbe yoyote wa kamati ya utendaji amehusika katika hili, atajitoa katika majukumu yote ya RT.
32
26. KAMATI ZA SHERIA
1) Kamati za Sheria ya RT itakuwa;
a) Kamati ya Nidhamu
b) Kamati ya Rufaa
c) Kamati ya Maadili
2) Bila kuathiri mamlaka ya Mkutano mkuu, kamati hizo tatu zimethibitishwa kutoa adhabu mbalimbali kama zilivyoainishwa na katiba hii.
3) Muundo, mamlaka zake, kazi za kamati za sheria zitatokana na kanuni ambazo zitapitishwa na kamati ya utendaji.
4) Wajumbe wa kamati za sheria watateuliwa na kamati ya utendaji.
5) Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na wajumbe watakaa katika uongozi kwa muda wa vipindi viwili tu mpaka itakapoamuliwa tofauti na kamati ya utendaji.
6) Adhabu zitakazotolewa na chombo stahiki kama katiba ilivyoelekezakwenda kwa mtu,klabu,au mwanachama yoyote ambaye ana makosa ya kinidhamu yaliyopelekea kuuchafua mchezo wa Riadha na itakuwa kama ifuatavyo;
a) Onyo;
b) Faini
c) Kurudisha zawadi;
d) Kufukuzwa;
e) Kusimamishwa kushiriki mashindano;
f) Kunyimwa matokeo ya mashindano;
g) Kupokonya,na;
h) Adhabu nyingine yoyote inayofaa.
7) Kamati ya Nidhamu
a) Kutakuwa na kamati ya nidhamu itakayokuwa na mwenyekiti, Naibu mwenyekiti na wajumbe watano walioteuliwa na kamati ya utendaji. Mwenyekiti na Naibu mwenyekiti wanatakiwa kuwa taaluma ya sheria.
b) Kazi za kamati hiizitasimamiwa na katiba hii, kanuni za nidhamu au Kanuni za nidhamu za IAAF kama hakuna kanuni za nidhamu za RT.
33
c) Kamati itapitisha adhabu ikiwa wajumbe watano wakuwepo, mmoja wao lazima awe ni Mwenyekiti ama Naibu Mwenyekiti.
d) Kamati itaweza kutoa adhabu iliyoainishwa kwenye katiba hii au kanuni zilizotokana na katiba hii kwa mwanachama, Klabu, Mwanariadha, Muamuzi, Ajenti au Mshabiki wa Riadha.
e) Vifungu hivi vitakuwa chini ya mamlaka ya Mkutano mkuu na kamati ya utendaji kuhusiana na Kusimamishwa na kufukuzwa kwa mwanachama yoyote.
8) Kamati ya Rufaa
a) Kutakuwa na kamati ya rufaa itakayokuwa na mwenyekiti, Naibu mwenyekiti na wajumbe watano walioteuliwa na kamati ya utendaji. Mwenyekiti na Naibu mwenyekiti wanatakiwa kuwa taaluma ya sheria,wajumbe wawili watateuliwa kutokana na taaluma yao ya Riadha na wajumbe watatu waliobaki,watateuliwa kutokana na uzoefu na mchango wao kwa maendeleo ya mchezo wa Riadha.
b) Kazi za kamati hiizitasimamiwa na katiba hii, kanuni za nidhamu au Kanuni za nidhamu za IAAF kama hakuna kanuni za nidhamu za RT.
c) Kamati itapitisha adhabu ikiwa wajumbe watano wakuwepo, mmoja wao lazima awe ni Mwenyekiti ama Naibu Mwenyekiti.
d) Kamati ya rufaa itakuwa na jukumu la kusikiliza rufaa mbalimbali toka Kamati ya Nidhamu ambazo hazijatamkwa ni za mwisho kutoka kwa mamlaka husika.
e) Maamuzi yatakayofikiwa na Kamati ya Rufaa hayatabatilishwa na yatazifunga pande zote mpaka itakapoelezwa tofauti na kanuni za kimataifa za michezo.
34
27. KUONDOLEWA KWA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI NA KAMATI NDOGO.
1) Bila kuathiri kifungu chochote katika katiba hii, wanachama wanaweza kupitisha azimio katika mkutano mkuu wa dharura, kumuondoa madarakani kiongozi yoyote. Hii haitahusiana na nyazifa za ajira.
2) Pale patakapokuwa na ombi halali la mkutano mkuu wa dharura wenye azimio la kupendekeza kumuondoa mtu madarakani, Katibu Mkuuatatoa taarifa kwa maandishi kuhusu pendekezo hilo kwa wahusika, ikihitajika, kutuma kwa wanachama wote wenye haki ya kuhudhuria mkutano huo.
3) Katika Mkutano mkuu wa dharura, waliopendekezwa kuondolewa madarakani watapatiwa nafasi ya kusikilizwa.
4) Kuondolewa kwa mtu yoyote hakutahusiana na madai ya haki zake alizonazo kwa RT, au RT kuwa na madai juu yake, kabla hajafukuzwa.
5) Wafuatao hawatakuwa na haki ya ya kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji au kamati ndogo;
a) Muajiriwa wa RT;
b) Muajiri,Muajiriwa wa mjumbe yoyote wa kamati ya utendaji au kamati ndogo;
c) Mtu ambaye,yeye au mwenzake au mwajiriwa hufanya shughuli ya katibu muhtasi au mtunza vitabu wa RT;
d) Mtu yoyote aliyepatikana na hatia kuhusiana na utangazaji,uundaji au utawala wa kampuni,au;
e) Mtu yoyote aliyepatikana na hatia ama kuhusishwa na makosa yaliyomo kwenye kifungu namba 472 ya Companies Act, Namba 12 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa.
f) Mtu yoyote ambaye,mahakama imetoa tamko kutokana na kifungu namba 424(1) ya Companies Act, Namba 12 ya mwaka 2002 ,kama ilivyorekebishwa;
i. Amefilisika;
35
ii. Aliyefukuzwa kazini kwa makosa ya nidhamu;
iii. Aliyehukumiwa (iwe ndani au nje ya nchi) kwa wizi, ulaghai, kughushi au kubadili taarifa za kughushi, kuapa uongo, makosa yapatikanayo katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Chapta 329 R.E 2002 (The Prevention and Combating of Corruption Act, CAP 329, R.E 2002),kama ilivyo rekebishwa,au makosa yanayohusiana na kutokua na uaminifu kwa kuhusiana na utangazaji,uundwaji au utawala wa kampuni,amehukumiwa jela bila nafasi ya kulipa faini au kwa faini inayozidi Tshs 500,000.
iv. Mtu yoyote ambaye amekutwa na makosa ya kuichafua RT na mchezo wa Riadha kwa ujumla.
28. KUTOKUWA NA IMANI NA UONGOZI Kama suala la kutokuwa na imani na viongozi litatokea,kifungu namba 28 kitatumika,kuendana na,mada ya kutokuwa na imani kuungwa mkono kwa maandishi na robo tatu (¾) ya wajumbe wa kamati ya utendaji au robo tatu (¾) ya vyama vya mikoa Tanzania. 29. KAMATI NDOGO
1) Kamati zote ndogo zitakuwa na wajumbe,ambapo kati yao,si chini ya wawili watakuwa wanawake,kama ifuatavyo;
a) Mwenyekiti;
b) Makamu mwenyekiti;
c) Wajumbe watatu wa ziada
2) Wajumbe wa kamati ndogo watakuwa kama wafanyakazi vivuli wa kamati ya utendaji, au kamati tajwa ya vyama vya mikoa vilipo.
36
SEHEMU YA NNE MENGINEYO 30. MAKAO MAKUU Ofisi kuu ya RT itakuwa katika eneo ambalo limeamuliwa na Kamati ya Utendaji. 31. UJUMBE WA HESHIMA Ujumbe wa heshima watatunukiwa watu ambao wameitumikia Riadha kwa uwezo wao na kwa kufuata yafuatayo;
1) Kutajwa,pamoja na ripoti za utumishi katika Riadha zilizopelekea kupendekezwa,itahitajikwa kuthibitishwa na kamati ya utendaji bila kujali kupendekezwa huko kumetoka,kamati ya utendaji yenyewe,vyama vya mikoaau familia ya riadha;
2) Pale pendekezo litakapothibitishwa na kamati ya utendaji, sambamba na ripoti ya utumishi, itatumwa kwa wanachama kwa ajili ya kufikiriwa.
3) Wanachama natapiga kura kwa masanduku ya siri,wale wachache waliopata asilimia sabini na tano (75%) ya kura zote watatajwa kw kutunukiwa heshima;
4) Majina ya mwisho yaliyopita, yatapelekwa kwenye AGM inayofuata kwa ajili ya kupitishwa.
5) Bila kuathiri Kifungu cha 32.1 hadi 32.4 cha katiba hii, haitaruhusiwa kutuzwa zaidi ya mara mbili kwa kila muongo kuanzia mwaka 2013.
37
32. FEDHA
1) Mwisho wa mwaka wa fedha wa RT unaoisha utakuwa kila tarehe 31 disemba, kila mwaka.
2) Malipo ya ada ya uanachama kwa wanachama wa moja kwa moja na wasio moja kwa moja;
a) Ada ya Kushirikishwa na ya leseni vitapangwa na Kamati ya utendaji.
b) Kushirikishwa na ada ya leseni italipwa kabla ya siku ya mwisho ya mwezi wa februari ya kila mwaka;
c) Kama ada ya kushirikishwa haitalipwa kwa wakati uliopangwa,mwanachama atasimamishwa kuhusika katika maswala yote ya RT na atarudishwa kutokana na chanzo cha kusimamishwa kuondolewa na kamati ya utendaji kuthibitisha;
d) Kama kiasi kikilipwa, ikiwamo adhabu inayolingana na nusu ya ada ya ushirikishwaji, kamati ya utendaji itaomndoa adhabu hiyo.
3) RT haitagawa faida ya mwaka kwa wanachama wake,itatumia kama ilivyoainishwa kwenye kifungu 33.4 hapa chini;
4) Faida yoyote itakayopatikana itatumiwa na RT katika maendeleo ya mchezo wa Riadha Tanzania;
5) Kila mwanachama anatakiwa kutuma taarifa ya ukaguzi kila mwaka, kabla ya AGM ya RT.
6) Mapato ya RT yatatokana na vitu vifuatavyo;
a) Ada ya uanachama ya kila mwaka;
b) Kiingilio cha wanachama;
c) Msaada wa kila mwaka toka IAAF;
d) Kipato cha asilimia kumi na tano (15%) kutoka katika kipato chochote apatacho mchezaji au timu;
e) Ruzuku,misaada toka katika vyombo vya juu vya michezo hapa nchini,BMT,TOC,Wizara n.k
38
f) Msaada,Uchangishaji fedha toka kwa wahisani,wadhamini ndani na nje ya nchi;
g) Mipango mbalimbali ya fedha kutoka kamati ya fedha;
h) Ada ya leseni kutoka kwa familia ya Riadha.
33. UKOMO WA UONGOZI.
1) Muda wa ukomo wa uongozi wa nafasi zote za kuchaguliwa utakuwa kila baada ya miaka minne (4).
2) Rais,Makamu wa kwanza wa Rais na Makamu wa pili wa Rais,hawataruhusiwa kugombea,baada ya kuongoza shirikisho kwa muda wa vipindi viwili;
3) Kwa nafasi ya kuajiriwa,Kamati ya utendaji ndiyo yenye mamlaka kwenye kuongeza au kusitishwa kwa mkataba wa mwajiriwa.
34. KANUNI ZINAZOHUSU MASHINDANO YA RIADHA.
1) Haki zote kuhusu mchezo wa riadha,kwa udhamini,ndani ya mamlaka ya RT,zitahifadhiwa ndani ya RT iwe haki izo zimetolewa au kuuzwa kwa mwanachama wa RT au mtu mwingine;
2) Haki zote za utangazaji,kwenye luninga,redio na aina yoyote ya utangazaji,kwenye mchezo wowote wa riadha nchini Tanzania,zimehifadhiwa na RT;
3) Wanachama wote watakuwa na haki ya kujadili,manunuzi ya ya utangazaji na udhamini wowote,kuendana na katiba hii pamoja na kanuni na sheria za RT;
4) Ziada ya faida itakayopatikana kutoka katika mchezo wowote wa riadha uliofanywa na mtu yoyote,chama au mwanachama wa RT kwa mamlaka ya RT,sharti zitumike kwa utangazaji na maendeleo ya mchezo huu Tanzania,kama itakavyoelekezwa na kamati ya utendaji;
39
5) Kwa hali yoyote kwamba haki za uandazi wa mchezo huu zimetolewa kwa mtu mwingine,kipengele cha 34.4 cha katiba hii sharti kitumike,kuhakikisha fedha hazitumiki kinyume na Riadha;
6) Hakuna mwanariadha atakayeruhusiwa kushiriki katika michezo iliyoandaliwa na RT(pia kwa wanachama wa RT),bila kuwa na leseni halali kutoka RT,mpaka kamati ya utendaji itakapoamua vinginevyo kutokana na mazingira adimu;
7) Mchezaji anatakiwa kuvaa namba ya leseni yake ya RT nyuma na mbele,haitaruhusiwa mwanariadha kuvaa namba yoyote ile bila idhini kutoka RT;
8) Namba ya leseni iliyovaliwa kwa mbele na mwanariadha,haitafunikwa mpaka haki ya kufanya hivyo imetolewa kwa idhini ya RT;
9) Kuandaa mashindano ya ndani ya Taifa ni haki kuu ya RT. Lakini,yafuatayo yanaweza kutokea;
a) Kama mwanachama yoyote atataka kuandaa mashindano ya ndani ya Taifa ya Riadha,anatakiwa kutuma maombi kwa RT kwa maandishi kuruhusiwa kufanya hivyo,kuonyesha jitihada za maombi hayo;
b) Mikoa itaruhusiwa kuandaa mashindano haya,si zaidi ya wanariadha watatu wa Taifa kutoka mikoa yote ya RT(nje ya mwenyeji) watashindana katika nyanja zao zisizosidi tatu kwenye mashindano hayo. Kinyume na kifungu hiki,adhabu itatolewa kulingana na matakwa ya RT;
10) Mashindano ya Taifa
a) RT itakuwa na majukumu ya kuandaa mashindano ya Taifa yafuatayo;
I. Mbio za nyika;
II. Mbio za barabarani
III. Michezo ya Ndani
IV. Mashindano ya wazi
40
b) Wanachama wote wa mikoa wanalazimika kupeleka timu zao kwenye mashindano ya Taifa;
c) Tofauti na itakapoamuriwa na kamati ya utendaji,washiriki wa mashindano ya Taifa ni lazima wawe watanzania;
11) Mashindano baina ya Mikoa
a) Vyama vya mikoa vyote vina haki ya kuandaa mashindano baina ya mikoa;
b) Kuandaa mashindano haya, vyama vya mikoa vinapaswa kuomba kwa maandishi kwa RT.
12) Vyama vya mikoa,familia ya Riadha ya RT ndiyo wenye haki ya kuandaa mashindano ya Riadha,hii ikiwemo mashindano ya kawaida na matembezi;
13) Mashindano ya Kimataifa;
a) Mashindano yote ya kimataifa yataandaliwa na RT,pia RT inaweza kutoa haki ya kuandaa mashindano haya kwa vyama vya mikoa;
b) Kama RT ikitoa haki ya uandazi kwa vyama vya mikoa, vitapaswa kuweza kulipa ada ya uandazi.
35. WAWAKILISHI WA WANARIADHA NA PROMOTA.
1) RT itaweka kanuni,sheria,mwenendo na mtiririko wa kuendesha, kulinda na kusajili wawakilishi wa wanariadha na promota;
2) Malipo ya ada ya mwaka yataamuliwa na kamati ya utendaji na yatalipwa na mwakilishi wa mwanariadha;
3) Mkataba baina ya mwanariadha na mwakilishi wa mwanariadha hautakuwa na nguvu au maamuzi mpaka mwakilishi awe amesajiliwa na RT na huo mkataba uwe umepitishwa na RT;
4) Mwanariadha hataruhusiwa kuwa na mwakilishi,mwakilishi hataruhusiwa,mpaka kuwe na mkataba halali baina ya mwanariadha na mwakilishi uliozingatia kanuni zilizowekwa na IAAF kuhusu Shirikisho/wawakilishi wa wanariadha;
41
5) Hakuna promota atakayeruhusiwa kuandaa mashindano ya riadha bila idhini ya maandishi kutoka RT,ili;
a) Kuandaa mashindano ya aina yoyote ya Riadha,kama mashindano ya ndani,Marathon,Mbio za Nyika n.k;
b) Kamati ya utendaji itatathmini ada ya malipo ya kwa promota anayetaka kuandaa mashindano hayo;
c) Kamati ya utendaji itatengeneza kanuni katika kuendesha mashindano hayo;
6) Wawakilishi wa wanariadha wanatakiwa kupewa leseni na RT, wakitakiwa kukubali kufuata kanuni na sheria za RT na katiba hii ndiyo watapewa leseni. Tofauti na hapo, RT itashindwa kuwapatia mahitaji yao kama ilivyoainishwa kwenye vifungu 34.3 na 34.4 vya katiba hii.
36. KANUNI NA SHERIA NDOGO
1) Kwa ziada ya katiba hii,kamati ya utendaji itaandaa kanuni na sheria ndogo katika kufanikisha ufanisi wa kazi za RT;
2) Kanuni na sheria hizi ndogo zinaweza kuongezwa,kurekebishwa au kuondolewa na;
a) Mkutano mkuu wa mwaka(AGM),au;
b) Mkutano mkuu wa dharura ulioitishwa kwa jambo hili.
3) Kamati ya utendaji itakuwa ndiyo yenye kutafsiri kanuni hizi. Kama kuna jambo halipo halijaelezwa jinsi ya kulishughulikia ndani ya kanuni hizo,katiba ya IAAF,kanuni zake,maelekezo yake yatatumika moja kwa moja.Mambo ambayo hayajaainishwa kwenye IAAF na kanuni za RT,yataamuliwa na kamati ya utendaji. Masuala ya sheria yatatumika baada ya kupitishwa na mkutano mkuu.
4) Kanuni ya Domicilium;
a) Klabu itakuwa moja ya familia ya Riadha ya RT katika eneo iliyopo ofisi ya klabu;
42
b) Mwariadha atauwakilisha mkoa ule anaoishi;
c) Nje ya mwanariadha wa Taifa,mwanariadha atakuwa mwanachama wa klabu kama klabu na mwanariadha wanaishi katika mkoa mmoja wa RT;
d) Mwanariadha wa Taifa atakuwa katika klabu yoyote aipendayo ncini Tanzania,lakini atauwakilisha mkoa mmoja anaoishi;
e) Hakuna mwanariadha atakayeruhusiwa kuwakilisha mkoa mwingine,bila kuwa na cheti maalumu toka mkoa wake wa kwanza,kinachomruhusu kuwakilisha mkoa mwingine. Bila kutokuwa na cheti cha ruhusa,mwanariadha hataruhusiwa kushindana kwa kuwakilisha mkoa mwingine mpya;
5) Zaidi kwenye suala la ziada,au pale klabu haitopewa ushirikiano na chama cha mkoa,klabu haitakuwa na haki ya kuwasiliana moja kwa moja na RT,zaidi ya kupitia chama cha mkoa;
6) Mwanariadha anaweza kuwasiliana moja kwa moja na RT,kama hajapata ushirikiano toka kwa klabu na chama cha mkoa;
7) Wafanyakazi wa RT wataitumikia kamati ya utendaji,kamati ndogo za RT kama wajumbe vivuli.
8) Mabadiliko ya Katiba;
a) Vifungu visivyo vya kiufundi;
Vifungu visivyo vya kiufundi ni vifungu ambavyo havihusiani na masuala ya kiufundi;
I. Mapendekezo ya mabadiliko ya katiba yatatumwa kwa katibu mkuu na mwanachama,siku 45 kabla ya mkutano mkuu(AGM) ili yafikiriwe.Mapendekezo yote yatatumwa na Katibu mkuu kwa wanachama wote siku 30 kabla ya mkutano mkuu(AGM). Mapendekezo yaliyoletwa na kamati za RT hayatafikiriwa;
43
II. Kupitisha,mapendekezo yoyote yanahitaji kupata mbili ya tatu (2/3) ya kura,ambapo mbili ya tatu (2/3) hiyo lazima iwakilishe angalau nusu ya kura ya wanachama wote wa RT(wingi wa kura);
III. Mabadiliko ya msingi ya maneno ya sheria zilizopitishwa na AGM,yanaweza kufanya na Rais(ama mjumbe wa kamati ya utendaji aliyeteuliwa na Rais),au Katibu mkuu,na hii haitahusiana na ubadilishwaji wa mantiki wa AGM;
IV. Mapendekezo ya mabadiliko ya vifungu visivyo vya kiufundi yanaweza kuletwa na vyama vya mikoa,kamati ya utendaji na wanachama binafsi.
b) Vifungu vya kiufundi
I. Pendekezo (toka kamati ya utendaji,kamati ndogo za RT) kubadili vifungu vya kiufundi,yatatumwa kwa katibu mkuu siku 45 kabla ya AGM ili kuweza kufikiriwa. Pendekezo la kubadili vifungu vya kiufundi linaweza kutolewa na mwanachama,kamati ya utendaji,kamati ndogo au kamati za kudumu za RT;
II. Nje ya mazingira adimu,mabadiliko ya vifungu vya kiufundi yatafikiriwa baada ya kupitishwa na kamati husika;
III. Taarifa iliyobeba maazimio ya kamati ya ufundi na kamati husika yatatumwa kwa wanachama wote,si chini ya siku 30 kabla ya mkutano mkuu (AGM);
IV. Pale kamati ya utendaji itakapotumia madaraka yake kurekebisha vifungu vya kiufundi,ama vifungu vyovyote kama suala la dharula,mabadiliko hayo
44
yanatakiwa kupelekwa na kuthibitishwa katika mkutano mkuu (AGM) unaofuata;
V. Mabadiliko ya vifungu vya kiufundi yakipitishwa na Mkutano mkuu (AGM),tarehe rasmi za kuanza kutumika zielezwe,tarehe hiyo iwape muda mzuri wanachama wote kujitayarisha kwa pamoja ,na;
VI. Mabadiliko ya msingi ya maneno ya sheria zilizopitishwa na AGM,yanaweza kufanya na mwenyekiti wa kamati ya ufundi na mashindano (ama mjumbe wa kamati ya ufundi na mashindano aliyeteuliwa na Rais),au Katibu mkuu,na hii haitahusiana na ubadilishwaji wa mantiki wa AGM;
9) Mabadiliko yoyote ya kanuni na sheria ndogo yataingizwa katika taarifa za kikao kilichofanya mabadiliko hayo na kupitishwa.Kama taarifa hiyo imesambazwa kama ilivyoainishwa kwenye katiba hii,hiyo itakuwa taarifa tosha ya mabadiliko hayo;
10) Hakuna kanuni ama sheria yoyote itakayokwenda kinyume na katiba hii;
11) Wanachama wote wa RT,familia ya riadha ikiwemo,klabu,vyama,watu walioshirikishwa;
a) Wanatakiwa kufuata na kutii kanuni na sheria za RT;
b) Kutoa taarifa yoyote inayohitajika na kamati ya utendaji ambayo inahusiana na mamlaka yanayoangukia kwa mwanachama huyo;
c) Kutokuingiza mabadiliko yoyote ya katiba au kuongeza,ambayo hayaendani na kanuni au sheria za RT,na au;
45
d) Kutowasiliana moja kwa moja na TOC,BMT,EAAR,AAC na IAAF bila kupitia RT;
12) Kwa ziada jinsi ambavyo sheria za IAAF na mabadiliko yake zitatumika kwa RT,zitatumika pia kwa wadhamini wa RT;
13) RT itawasiliana na vyama vya mikoa kupitia anwani ya ofisi ya chama cha mkoa iliyosajiliwa na RT. Ofisi ya RT haitawasiliana kiofisi na watu binafsi,wanariadha,vilabu,kamati za mikoa,bila kupitia chama cha mkoa,nje ya hali kifungu cha 36.6 cha katiba hii,:
14) RT itakuwa na haki,kwa uwezo wake,kuwasiliana na mwanachama wake yoyote au familia ya Riadha(mwanariadha,klabu,mfanyakazi au mwanachama) pale itakapoona inafaa;
15) RT ina mamlaka sawa na maeneo waliyopo wanachama wake au familia ya riadha,suala la mamlaka,RT inahaki ya kumchukulia hatua za kinidhamu mwanachama yoyote ama mjumbe yoyote toka familia ya Riadha;
16) RT itatambua katiba za wanachama wake,pale tu zitakapokuwa zimepitishwa na RT;
17) Muundo wa RT na wanachama wake unapaswa kuzingatia makundi mbalimbali ya watu ikiwemo jinsia;
18) Vyama vya mikoa vitaandaa mashindano ya mikoa kwa mfano wa RT;
19) Mashindano ya vilabu ya Taifa;
a) RT itaamua kuhusu kanuni na sheria za kusimamia mashindano haya;
b) Vilabu na taasisi zinazotambulika na kusajiliwa na RT zinaweza kutuma maombi kwa ajili ya kushiriki;
c) Vilabu na Taasisi zilizofuzu vigezo vilivyowekwa na RT, vitashindana katika mashindano haya.
46
d) Mikoa itakuwa na haki ya kuandaa na kuratibu mashindano ya vilabu mikoani,kwa kanuni na sheria za RT na za vyama vya mikoa zilizothibitishwa na RT.
37. TAFSIRI
1) Kwa kuzingatia vifungu vya katiba hii,,maamuzi ya mkutano mkuu kuhusu uhalali wa kifungu chochote ndani ya katiba hii yatakuwa ni ya mwisho na yenye kufunga.
2) Matatizo yatakayojitokeza ambayo hayajaainishwa katika katiba hii,yatapelekwa kwa katibu mkuu kimaandishi,yatachunguzwa na taarifa kupelekwa kwa kamati ya utendaji kabla hayajawekwa kama ajenda kwenye mkutano mkuu(AGM) utakaofuata.
38 . MIGOGORO
1) Katiba hii itatambua uwepo wa baraza la usuluhishi,mamlaka yake na Mahakama ya Michezo (CAS);
2) RT itaanzisha baraza la usulihishi,litahusika na migogoro yote ya ndani ya RT,wanachama wake,Wanariadha,Waamuzi na wahusika katika familia ya Riadha. Kamati ya utendaji itaandaa kanuni na sheria kuhusu jinsi ya kuunda,mamlaka na mwenendo wa baraza la usuluhishi;
3) Mgogoro wowote kati ya wanachama,mwanachama na RT,mwanachama na mwanariadha,mwanariadha na RT,mwanariadha na IAAF,mwanariadha na AAC,utawasilishwa kwenye baraza la usuluhishi kwa kuangaliwa ndani ya siku tisini (90) tangu ulipoanza;
a) RT itakuwa na mamlaka na migogoro ya ndani kitaifa,migogoro kati ya wanachama wa RT,huku IAAF watakuwa na mamlaka na migogoro ya kimataifa,migogoro baina ya pande toka mamlaka tofauti ama shirikisho;
47
b) Kuendana na ibara ya 59 na 60 ya katiba ya IAAF,rufaa yoyote kuhusu maamuzi ya mwisho na yanayofunga ya IAAF,itasikilizwa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) iliyopo Lausanne,Switzerland.
c) RT itahakikisha kufuata, wakiwemo wanachama, wanariadha, waamuzi pamoja na wawakilishi wa wanariadha,maamuzi ya mwisho yaliyopitishwa na IAAF au CAS;
d) Usuluhishi hautapitishwa na baraza la usuluhishi mpaka iangaliwe kuwa;
I. Mgogoro upo au umetamkwa,na;
II. Njia zote zimetumika kutokana na katiba hii,katika kusuluhisha mgogoro huo
e) Mgogoro utasikilizwa na msuluhishi au wasuluhishi walioteuliwa na baraza la usuluhishi,ndani ya siku thelathini (30) tangu mgogoro huo upelekwe,na kwa kanuni za baraza hilo.
f) Maamuzi yatakayofanywa na msuluhishi au wasuluhishi yatakuwa ya mwisho na yenye kufunga pande zote.
g) Mwenendo na malipo ya ada ya kusikiliza mgogoro yatapangwa na RT;
h) Hakuna Mwanachama wa RT,au wanachama wao,watatoa adhabu inayozidi miaka miwili (2) kwa kosa la kinidhamu;
i) Migogoro yote inayoathiri ushiriki wa wanachama,inayohusisha wachezaji,wanaounga mkono riadha au watu wengine ndani ya mamlaka,ukitokea kwa namna yoyote,iwe kuhusu madawa au siyo madawa,yatasikilizwa na kamati ya Maadili ya RT au kama itakavyoelekezwa tofauti na RT,Usikilizwaji huo utazingatia yafuatayo;
I. Kusikiliza kwa wakati mbele ya chombo kilicho na haki na usawa;
48
II. Haki ya mtu kutaarifiwa kuhusu mashtaka anayotuhumiwa;
III. Haki ya kutoa ushahidi,ikiwepo haki ya kuita na kuwadadisi mashahidi;
IV. Haki ya kuwakilishwa na mwanasheria au mtafsiri (kwa gharama binafsi)
V. Haki ya maamuzi kutolewa kimaandishi na kwa wakati.
j) Mgogoro wowote baina ya RT na IAAF utapelekwa katika kikao cha IAAF (IAAF Council),kikao cha IAAF kitabainisha mwenendo na jinsi ya kutatua mgogoro kulingana na aina ya mgogoro wenyewe;
k) Mgogoro wowote baina ya RT na mwanachama yoyote wa IAAF,utapelekwa kwenye kikao cha IAAF,ambapo kitabainisha mwenendo na jinsi ya kutatua mgogoro kulingana na aina ya mgogoro wenyewe;
39. MAVAZI
1) Nembo na rangi za RT zitaamuliwa na mkutano mkuu (AGM) kila baada ya muda;
2) Nembo na rangi zitakazotumiwa na timu ya Taifa zitakuwa nembo na rangi za Taifa ambazo zitaamuliwa na RT;
3) Wimbo wa Taifa kama ukihitajika,utakuwa wimbo wa taifa wa Tanzania.
40. MABADILIKO YA KATIBA
1) Mabadiliko ya katiba hii yatafanywa na mkutano mkuu wa mwaka (AGM) au mkutano mkuu wa dharura (SGM) ulioitishwa kwa madhumuni hayo.
2) Taarifa ya mapendekezo ya mabadiliko itaonekana katika ajenda kwa kufuata mwenendo uliowekwa katika ibara ya 36.8 ya katiba hii;
3) Taarifa itaelezea kuhusu ibara ipi inatakiwa kurekebishwa,itataja wazi wapi paondolewe au kuongezwa;
49
4) Katiba itarekebishwa kulingana na ibara ya 36.8 ya katiba hii;
5) Mabadiliko yoyote ya katiba hii, baada ya kuanza kutumika,itatumika baada ya mkutano kumalizika,au mkutano utakapoamua tofauti kwa kura ya mbili ya tatu ya wote.
41. KUKOMA KWA SHIRIKISHO Kuvunja shirikisho la RT kutafanyika kwa kufuata ibara za 13, 14 na 15, huku yafuatayo yakiwa yamezingatiwa;
1) Kuteuliwa kwa kamati ya muda kwa ajili ya kumalizia masuala mbalimbali ya RT:
2) Kamati hii ya muda iwe imeundwa na wajumbe wawili kutoka kamati ya utendaji,msimamizi wa masuala ya benki wa RT na katibu mkuu;
3) Mali na majukumu mbalimbali ya RT,yatagawanywa kwa kufuata maelekezo ya maafisa wakaguzi wa RT,kupelekwa kwa chama chenye malengo na madhumuni kama ya RT
42. MAMLAKA YA KATIBA HII
1) Katiba hii itakuwa juu ya katiba zote za wanachama wake,vilabu kama zitakuwa katika mgogoro na katiba hii;
2) Ibara za katiba hii zitakuwa juu ya sheria na kanuni zozote za RT,kama zitakuwa katika mgogoro na katiba hii;
43. MAMLAKA YA KANUNI ZA IAAF Ibara yoyote ya katiba hii ambayo itakuwa na mgogoro na kanuni za IAAF, kanuni hizo zitashinda na kutumika kama zitakavyo badilishwa kila muda.
50
KWA NIABA YA SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA (RT) ______________________ __________________________ ANTHONY MTAKA SULEIMAN MJAYA NYAMBUI Rais Katibu Mkuu
51
NYONGEZA A YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA WAJIBU WA KAMATI NDOGO 44.NYONGEZA;
1) KANUNI NA SHERIA ZA KUSIMAMIA KAMATI NDOGO;
a) RT itakuwa na kamati ndogo maalum nne, Kamati ya Mbio za Nyika, Kamati ya Mbio za Ndani, Kamati ya Mbio za Barabarani na Kamati ya Wanariadha.
b) Kamati hizi zitakuwa sehemu ya RT, hazitakuwa na mamlaka ya kisheria ya aina yoyote kusimama nje ya RT.
c) Kamati hizi hazitakuwa na mkutano mkuu wa mwaka, mkutano wa baraza, wakwao wenyewe nje ya RT.
d) Kamati hizi hazitakuwa na mamlaka yoyote, tofauti nay ale watakayopewa na RT.
e) Lengo kubwa la kamati hizi ni kupanga, kiufundi na kimaelekezo kwa kufuata kanuni na sheria za kamati husika.
f) Kamati zitakutana zikihitajika kufanya hivyo.
g) Fedha zilizokusanywa na kamati hii zitatumika kwa makusudi ya kamati, pato la ziada litatumika zaidi kwa kamati husika.
h) Kamati hizi zina haki ya kuteua mjumbe ambaye atathibitishwa na kamati ya utendaji. Katibu mkuu atashiriki kwenye kamati hizi sawa na anavyoshiriki kwenye kamati ya utendaji.
52
2) MGAWANYO WA MADARAKA
a) Kwa kufuata mamlaka yote ya kamati ya utendaji, mgawanyo wa madaraka utazingatia mwenendo mzima wa RT, au kamati ya utendaji kuamua vinginevyo, maagizo mengine ya kamati hizi yameainishwa katika Nyongeza hii.
b) Kwa suala la mgawanyo, kamati itatengewa bajeti hai kwa fikra za kamati ya utendaji baada ya ushauri wa kamati husika.
3) MAMLAKA YA KAMATI NDOGO
Kamati hizi zitafanya kazi za Riadha kwa hali ya weledi wa hali ya juu kama watakavyopewa na kamati ya utendaji, ikiwemo;
a) Kushirikiana kwa karibu na kamati husika za mikoa katika kuendeleza mchezo wa Riadha.
b) Kuandaa kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji,Kamati ya Ufundi na Maendeleo, Kamati ya Mashindano, Mashindano ya RT,michezo ya kimataifa,uchaguzi wa timu kwa majaribio ya kimataifa na mashinano yoyote yatakayojitokeza.
c) Kuchagua washindani kuiwakilisha RT katika mashindano ya kimataifa, kupendekeza meneja wa timu hiyo iliyochaguliwa kwa ridhaa maalum toka Kamati ya Utendaji.
d) Kulinda kanuni za michezo nchini zinazohusiana na aina ya mchezo wa Riadha na kuhakikisha zinafwata.
e) Kuhakikisha mashindano yote yanayoandaliwa kwa niaba ya RT yanaafiki kanuni za kuzuia matumizi ya dawa haramu.
53
f) Kutoa ushauri kwa wandaaji wa mashindano na kuwasaidia kufuatwa kwa ratiba nzima ya maadili ya mchezo huo.
g) Kutayarisha orodha ya kumbukumbu za kitaifa za ushiriki na viwango.
h) Kuanzisha na kusimamia kanuni na desturi kitaifa, zinazohusu mchezo huu.
i) Kushirikiana kwa karibu na Kamati ya Ufundi na Maendeleo, kukuza maendeleo ya mchezo wa Riadha Tanzania.
j) Kwa ruhusa ya Kamati ya Utendaji, kuandaa kanuni mbalimbali na kuhakikisha kuwa,waandaaji wa mashindano,wanazifuata,lakini hakuna kanuni itakayokwenda kinyume na kanuni za mashindano.
4) MWENENDO WA KAMATI NDOGO
a) Mikutano ya kamati ndogo itaitishwa, kwa taarifa itakayotolewa sio chini ya siku ishirini na moja (21) kwa wajumbe wote wanaohusika na mkutano,kupitia anwani zao walizoandikishwa nazo rasmi na RT.
b) Akidi ya kikao cha kamati ndogo itatimia,angalau wajumbe watatu watahudhuria akiwemo,mwenyekiti au makamu mwenyekiti wa kamati.
c) Mwenyekiti au wajumbe watatu wa kamati kwa kupitia kwa mwenyekiti wanaweza, kuitisha kikao cha dharura muda wowote kwa taarifa ya sio chini ya siku saba (7).
d) Jambo lolote litakaloibuka kwenye mkutano,litaamuliwa kwa wingi wa kura,kama kuna mgongano wa kura,kiogozi wa mkutano atakuwa na kura ya maamuzi.
54
e) Kama mwenyekiti hatakuwepo kwenye kuanza kwa mkutano, makamu mwenyekiti ataongoza mkutano.
f) Kamati zitapanga nakala zote za maelezo ya mikutano yote na Katibu Mkuu.
g) Tofauti na jinsi ilivyobainishwa ndani ya katiba hii, kamati hizi,zitatafakari mwenendo na taratibu zake,zisizokwenda kinyume na katiba hii.

KWA NIABA YA SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA (RT) ______________________ __________________________ ANTHONY MTAKA SULEIMAN MJAYA NYAMBUI Rais Katibu Mkuu

No comments:

Post a Comment