Wednesday, 24 June 2015

Covenant Bank yaipatia Chaneta sh. Milioni 40 kwa safari ya Botswana

*Ni tiketi 20, mabegi na suti za michezo kwa ajili ya mashindano ya Afrika


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Covenant. Sabetha Mwambenja (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi tiketi za ndege kwa timu ya Taifa Queens. Kulia ni nahodha wa timu hiyo Sophia Komba.

Mwenyekiti wa Chaneta Annie Kibira (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhiwa tiketi za ndege na Covenant Bank leo asubuhi.
Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Allen Alex  akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Nahodha wa timu ya taifa ya netiboli, Taifa Queens, Sophia Komba.
 Mkurugenzi wa Coenant Bank (kushoto) akimkabidhi tiketi mmoja wa wachezaji wa Taifa Queens.

Na Cosmas Mlekani
BENKI ya Covenant leo imetoa tiketi 20 za ndege, mabegi na suti za michezo kwa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) ili kuiwezesha timu ya Taifa Queens kwenda Gaborone Botswana kushiriki mashindano ya Afrika.

Mashindano hayo yanaanza Jumamosi na Taifa Queens inaondoka Ijumaa na wachezaji 17 na viongozi watatu tayari kwa mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Benki hiyo ya wanawake ya Tanzania imetoa jumla y ash. Milioni 40 kwa ajili ya tiketi na vifaa hiyo vingine ambavyo itatumika na timu hiyo ikiwa nchini Botswana.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tiketi hizo katika Makao Makuu ya benki hiyo Kijitonyama jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Sabetha M.J Mwambenja alisema kuwa wameisaidia Taifa Queens ili kuwawezesha kushiriki mashindano hayo.

Alisema timu hiyo inaundwa na wanawake hivyo ni moja ya jukumu lao kuwawezesha wanawake kufikia malengo yao kwa njia tofauti.

Mwakilishi wa Wizara ya Kazi, Vijana Utamaduni na Michezo Allen B. Alex liishukuru benki hiyo kwa kubeba `msalaba wa wizara hiyo ambayo ni jukumu lake kuvisaidia vyama vya michezo.

Naishukuru benki ya Covenant kwa kuchukua msalaba wa serikali wa kuvisaidia vyama vya michezo kuisaidia Chaneta kupeleka timu Namibia alisema Alex.

Alizitaka tasisi zingine kuiga mfano wa Cevenant Bank wa kusaidia jamii.

Mwenyekiti wa Chaneta Annie Kibira aliishukuru benki hiyo hasa mkurugenzi wake (Mwambenja) kwa kukubali kuisaidia Chaneta licha ya kuombwa kwa muda mfupi.

Nawapongeza Covenant na hasa dada yangu (Sabetha) kwa kukubali kutusaidia licha ya kuwasilisha maombi siku chache zilizopita alisema.

Naye nahodha wa timu hiyo Sophia Komba alisema kuwa, wamejiandaa izuri kwa ajili ya mchezo huo na wanatarajia kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Mkwasa atangaza Taifa Stars mpya na kuwatema saba


Kocha Mkuu mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni msaidizi wake, Hemed Morocco.

 Na Seba Nyanga
KOCHA wa timu ya  Soka ya Taifa,  Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema watajitahidi kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano kufuzu  kwa fainali ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan)   dhidi Uganda, huku akisisitiza kuwa mashabiki wasitarajie miujiza.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkwasa alisema kwa muda mfupi waliokabidhiwa timu, hawataweza kufanya mabadiliko makubwa, lakini watajitahidi kwa uwezo wao kuleta matumaini mapya.

Aidha, Mkwassa amefanya mabadiliko kwenye timu ya taifa pamoja na benchi la ufundi, ambapo mbali na kuita wachezaji 26, amemteua kocha wa zamani wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni kuwa mshauri wa timu.

Katika timu yake Mkwasa amewapumzisha wachezaji saba waliotumika kwa muda mrefu na kuwaita watatu wapya ambao hawakuwahi kuitwa kwenye timu iliyopita.

Mkwasa aliteuliwa juzi kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, akirithi mikoba ya Mholanzi  Mart Nooij aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki kufuatia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa Chan.

Alisema wachezaji walioteuliwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajitunza na kujiheshimu ndani na nje ya uwanja, huku akisema  atashirikiana na benchi jipya la ufundi kujenga timu imara bila upendeleo.

Wachezaji  waliowekwa kando ni pamoja na Amri Kiemba, Deogratias Munishi, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Kevin Friday, Oscar Joshua na Hassan Dilunga.

Sura mpya ambazo hazikuwahi kuitwa ni Mudathir Khamis (KMKM), Michael Aidan(Ruvu Shooting) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).

Walioitwa kwa jumla ni Mohamed Hussein Tshabalala(Simba) , Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano (Simba),  Mwadini Ally (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub Cannavaro (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), na Hassan Isihaka (Simba).

Wengine ni  Aggrey Morris (Azam),  Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam), Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera) Ramadhan Singano Messi (Simba). John Bocco (Azam), Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar),
Wachezaji wa akiba ni Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu).

Wachezaji hao wote watazungumza na makocha kesho kwenye hoteli ya Tansoma na keshokutwa wataanza mazoezi rasmi kwenye uwanja wa Boko Veteran kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.

Katika hatua nyingine, Mkwasa alitangaza benchi la ufundi la Taifa Stars chini ya usaidizi wa Hemed Morocco wakati kocha wa makipa ni Peter Manyika, mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi na meneja wa timu ni Juma Mgunda.

Alisema kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.

Jackson Mayanja aingia mkataba wa miaka miwili Coastal UnionNA Mwandishi Wetu, Tanga
MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988,Coastal Union,Wagosi wa Kaya imeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni raia wa Uganda kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu.

Utiliaji wa saini wa Kocha huyo ulifanyika (leo)jana mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu ya Coastal Union akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter na Katibu Mkuu wa timu hiyo,Kassim El Siagi.

Akizungumza baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi kuu msimu ujao.

Amesema kuwa uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini kuja wake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo. 

Mayanja ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Vipers  FC ya Bunamwaya  na KCC ya Uganda amesema kutua kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha anatoa mchango wake kwenye kuipa mafanikio.

Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inangara katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki, wanachama na wapenzi.
Kocha Mkuu mpya wa timu ya Coastal Union,Jackson Mayanja kushoto akisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo kulia ni Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.
 Amesistiza pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka kuona timu hiyo inangara kwenye medani za kitaifa na kimataifa.

Sunday, 21 June 2015

Man City yakubali kuilipa Liverpool pauni Mil 50 kumnunua SterlingMANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City hadi sasa imewasilisha maombi mara mbili huku lile la mwisho likiwa linakaribia kiasi cha pauni Milioni 40. Yote yametupiliwa mbali na Liverpool.

Imebainishwa kuwa Liverpool hawataki kumuuza mchezaji wao Raheem Sterling mwenye umri wa miaka 20 chini ya kiasi cha pauni Milioni 50.

Chanzo kilichokaribu na klabu hiyo ya Merseyside imedokeza kuwa Man City haina mpango wa kukubali kumuachia mchezaji huyo endapo Man City hawataongeza pauni Milioni 10 ndipo wataweza kumuachia.

Man City pia wanajua kuwa klabu zingine kibao nazo zinamtaka mchezaji huyo ikiwemo Real Madrid ya Rafa Benitez, Arsenal na Chelsea.

Hawataki kabisa kumkosa Sterling na wanatarajia siku chache sijazo wanatarajia kuwasilisha ofa ambayo itawaridhisha Liverpool.

Man City pia wako tayari kuijaribu Arsenal kumnunua mwenzake na Sterling wanaecheza naye timu ya taifa ya England Jack Wilshere.

Hatahivyo, kocha wa Gunners Arsene Wenger anasisitiza kuwa shujaa huyo wa England aliyefunga mabao mawili wakati England ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Ulaya huko Slovenia Jumapili ya wiki iliyopita hauzwi.