Sunday, 8 March 2015

Liverpool yashindwa kuifunga Blackburn Rovers FA CupLONDON,England
TIMU ya Blackburn Rovers imeikalia kooni Liverpool na kulazimisha kurudiwa kwa mchezo huo war obo fainali wa Kombe la FA.

Pamoja na Liverpool kucheza mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa Anfield, bado walishindwa kufurukuta na kujikuta muda ukimalizika timu hizo zikiwa suluhu.

Craig Conway aliikosesha timu yake bao la mapema baada ya kupaisha mpira kabla ya Kolo Toure bao lake kukataliwa baada ya kudaiwa kufunga akiwa tayari ameshaotea.

Baadae Alex Baptiste mpira wake uliokolewa wakati Blackburn Rovers iliyopo daraja la kwanza kucheza vizri baada ya mapumziko.
Gerald akiwa jukwaani akishuhudia timu yake ikicheza robo fainali ya FA Cup.

No comments:

Post a Comment