Tuesday 17 March 2015

Yanga kuiondoa Azam FC Kileleni leo?



 *Inacheza na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa

*Simba wageni wa Mgambo JKT Mkwakwani Tanga

Kikosi cha Yanga.
Na Mwandishi Wetu
VIGOGO vya soka nchini vya Yanga na Simba leo vitashuka katika viwanja tofauti kucheza mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya Afrika, leo watashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakiikaribisha Kagera Sugar ya Bukoba.

Wakati Yanga wakiwa Uwanja wa Taifa, wenzao Simba watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuumana na Mgambo JKT ya huko.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Yanga walipokea kichapo cha bao 1-0 na hivyo leo itakuwa na hasira ya kulipa kisasi.

Yanga ambayo ilicheza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Simba kwenye uwanja huo huo na kupokea kichapo cha bao 1-0, na hivyo itataka kurejea kwa kishindo katika ligi hiyo na kurejea kileleni.

Yanga inahitaji kushinda mchezo wa leo kama inataka kurudi na kuwa kinara katika msimamo wa ligi.

Azam FC imewashusha Yanga kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kushika usukani wa ligi hiyo, lakini Yanga leo inaweza kurejea.

Katika mchezo mwingine leo; Mbeya City ambayo msimu huu haifanyi vizuri itaikaribisha Stand United ya Shinyanga katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.

Msimamo:
                 MP  W  D   L   GF GA  +/- Pts
    1.Azam       17  9   6   2   24  12  12   33 
    2.Yanga      16  9   4   3   21  9   12   31 
    3.Simba      18  7   8   3   22  12  10   29 
    4.Kagera     18  6   7   5   15  15   0   25 
    5.Coastal    18  5   8   5   13  12   1   23 
    6.Mtibwa     18  5   8   5   18  18   0   23 
    7.JKT Ruvu   18  6   5   7   15  16  -1   23 
    8.Shooting   18  5   7   6   12  14  -2   22 
    9.Ndanda     19  6   4   9   17  23  -6   22 
    10.Stand     18  5   6   7   16  21  -5   21 
    11.Mgambo    17  6   3   8   11  17  -6   21 
    12.Polisi    19  4   8   7   13  17  -4   20 
    13.Mbeya City18  4   8   6   12  16  -4   20 
    14.Prisons   18  2   10  6   13  20  -7   16 

No comments:

Post a Comment