TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Tigo yatoa msaada wa
millioni 30 Tshs kwa waathirika wa mafuriko mjini Kahama
Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kutumika
nyumbani vyenye thamani ya millioni 30 kwa familia zilizoathirika na mvua kubwa
ya mawe na mafuriko wiki iliyopita, iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 50 mjini
Kahama, mkoani Shinyanga
Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa
mafuriko na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya ziwa Bwana Ally Maswanya, alie sisitiza
ahadi ya kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida.
“Tupo hapa kujumuika
na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole walioathirika na maafa hayo, na
tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza
wapenzi wao na mali zao,” Alisema Maswanya.
Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni magodoro, unga wa
mahindi,mchele,maharage,dagaa,mafuta ya kula,chumvi,sukari,ndoo,sabuni, karai,
vikombe na masahani.
Tigo pia kwa kupitia mtandao wake, imejitolea
kuchangisha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko, ambapo mteja wa Tigo
anaweza kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15741 kwa ajili ya kuchangia Tshs 200
kutoka kwa mda wake wa maongezi au kupitia vipochi vyao vya Tigo Pesa kuenda
namba 0714048435.
Mvua zilizonyesha mjini Kahama, wiki iliyopita,
iliripotiwa kwamba zilisababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na kuacha watu 3,500
kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu yaliharibika au kubebwa
na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally
Rufunga.
Msaada kutoka Tigo, kulingana na Maswanya, ni katika
mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza
baadhi ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika
kusaidia jamii majanga yanapo ibuka.
![]() |
Baadhi ya magodoro na vyakula vilivyotolewa na Tigo, kama msaada kwa waathirika wa mafuriko katika kijiji cha Mwakata, wilaya ya Kahama,mkoani Shinyanga. |
No comments:
Post a Comment