Thursday 19 March 2015

Arsene Wenger alia na sheria ya bao la ugenini


Arsene Wenger.

LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger amesisitiza kuwa hakuna mgogoro wa soka la England Ulaya licha ya mwaka wa pili mfululizo kwa timu za nchi hiyo kutolewa katika hatua ya 16 bora katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa, lakini anaamini kua wakati umefika wa kubadili mfumo wa sheria ya bao la ugenini.
 .
Arsenal na Chelsea zote zilitolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa faida ya bao la ugenini katika hatua ya kwanza ya mtoano, zikifungwa na Monaco na Paris Saint-Germain.
Hatahivyo, Wenger, amekuwa kwa muda mrefu akipigania kubadilishwa kwa sheria hiyo.

'Hiyo ni sheria iliyopitwa na wakati na sasa wakati umefika wa kuibadilisha, ' alisema kocha huyo wa Arsenal. 'Labda sheria hiyo ituike baada ya kuchezwa muda wa nyongeza. Ilianzishwa miaka 1960  ili kuziwezesha timu kushambulia zikicheza ugenini.

'Tangu wakati huo ilipoanzishwa sheria hiyo soka limebadilika sana na uzito wa bao la ugenini kwa sasa ni mkubwa sana. Labda bao hilo lihesabike baada ya muda wa nyongeza kama vile katika Kombe la Ligi England.

'Nafikiri kiwango cha Ligi Kuu ya England ni kikubwa na siko katika hali ya kuelezea sana nini tatizo la soka la Uingereza. Sifiiri kama kuna tatizo kubwa. '

Wenger sasa anatakiwa kuwaweka tayari wachezaji wake kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Newcastle United wakati mpambano wa kusaka nafasi nne za kwanza ukiendelea katika ligi hiyo.

Aliongeza: 'hali iko chini ya tumekatishwa tamaa. Mpambano ulidumu kwa takribani dakika 180 na hatukuwa na tahadhari ya kutosha katika dakika 90 za kwanza. Tunajua kwanini tumetolewa, ni tatizo ka kuzuia katika mchezo wa kwanza.

SHERIA YA GOLI LA UGENINI:
Endapo mpira utamalizika watimu hizo zikilingana magoli, timu iliyofunga mabao mengi ugenini itatangazwa kuwa mshindi wa mchezo huo.

Mfano, Monaco iliifunga Arsenal 3-1 ugenini kabla ya kufungwa 2-0 huko Monte Carlo.

Huku matokeo yakiwa bao 3-3, Monaco imesonga mbele baada ya kufunga goli nyingi zaidi ugenini ukilinganisha na bao mbili za Arsenal ugenini.

No comments:

Post a Comment