Wednesday, 11 March 2015

Nyilawila, Mada Maugo kuzichapa Jumapili Indoor StadiumNa Seba Nyanga
MABONDIA Kalama Nyilawila na Mada Maugo watapanda ulingoni Machi Jumapili Machi 15 katika Uwanja wa Taifa wa Ndani kutwangana katika pambano na ndondi za kulipwa.

Pambano hilo limeandaliwa na Mwazoa Promotion na viingilio vitakuwa Sh. 10,000 kwa eneo la kawaida na Sh. 20,000 kwa wale watakaokaa katika viti maalum (VIP).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam, kutakuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi ili kunogesha pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu.

Katika pambano la kwanza la utangulizi, Abdallah Pazi atazichapa na Thomas Mashali katika pambano la raundi 10 wakati Said Mbelwa atakuwa na kibarua kizito wakati atakapotoana jasho na Japhet Kaseba.

Mbali na hayo, pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambayo yatatangazwa siku hiyo ya mpambano ili kutoa burudani zaidi kwa wapenzi watakaofika Uwanja wa Taifa wa Ndani siku hiyo.

Waandaji wamesema kuwa siku hiyo pia kutauzwa DVD za mapambano mbalimbali makali pamoja na vifaa vingine ambavyo vitauzwa na kocha mahiri wa ndondi Super D.

No comments:

Post a Comment