Monday 24 August 2015

SERENA Williams, Roger Federer watwaa mataji ya Cincinnati Masters


Serena Williams akiwa na taji lake la Cincinnati Masters

OHIO, Marekani
SERENA Williams na Roger Federer mwishoni mwa wiki walitwaa ubingwa wa tenisi wa mashindano ya Cincinnati Masters kwa upande wa wanawake na wanaume.

Williams ambaye ni bingwa namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wachezaji tenisi wanawake, alimshinda bingwa namba tatu Simona Halep na kutwaa taji hilo.

Mchezji huyo mwenye umri wa miaka 33 alishinda mchezo huo kwa 6-3 7-6 (7-5) na kumsambaratisha Mromania Halep, mwenye umri wa miaka 23,ambaye kwa kucheza fainali ya mashindano hayo tayari alishapangwa katikanafasi ya pili ya kushiriki mashindano ya US Open.

Halep alimzidi Williams mwanzoni mwa mchezo, lakini bingwa huyo wa Wimbledon alipambana na kushinda mchezo huo.

"Shukrani kwa Simona kwa kucheza mchezo mzuri kama ule, " alisema Mmarekani huyo, ambaye alishinda mchezo huo kwa kutumia saa moja na dakika tisa.
"Siungwi mkono kokote ninakocheza, lakini hapa nimeoneshwa upendo mkubwa na ninataka kurudi tena.

Halep alisema: "Ni furaha ilioje kwa yeye kucheza fainali. Anampongeza bingwa.

Naye Roger Federer alitwaa ubingwa huo baada ya kumshinda bingwa namba moja kwa ubora Novak Djokovic na kushinda taji la saba la Cincinnati Masters.

Mchezaji huyo Mswis mwenye umri wa miaka 34, aliyemtoa Muingereza Andy Murray katika nusu fainali, alipata ushindi huo kwa 7-6 (7-1) 6-3.

Federer, ambaye sasa atapangwa katika Kundi la Pili katika mashindano ya US Open, alishindamchezo huo kwa saa moja na dakika 30.
Roger Federer akipozi na kombe lake.

No comments:

Post a Comment