Sunday 22 January 2017

Broos siku moja kurejea Cameroon

KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon Hugo Broos anataka Joel Matip kurejea katika timu ya taifa baada ya kumalizika kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika.

Matip alikataa wito wa kuichezea Cameroon katika mashindano hayo ya Afcon na badala yake akaenda kuichezea Liverpool.
"Nafikiri atabadili mawazo yake na tutamuona katika mchezo ujao (baada ya kumalizika kwa Afcon) kwa sababu ni mchezaji mzuri sana, alisema Broos.

Sheria za Fifa zinasema kuwa mchezaji huenda akazuiwa kuichezea klabu yake endapo atakataa kuichezea nchi yake lakini Ijumaa Matip alishafisha kuichezea klabu yake.
Broos aliongeza: "Nina furaha sana kuwa hili tatizo limetatuliwa na anaweza kuichezea tena Liverpool na nina tumaini anaweza kuichezea tena Cameroon.

"Nafikiri kila mmoja yuko huru kufaya uamuzi na kuamua kutokuja nasi hapa katika mashindano ya Mataifa ya Afrika.
"Kwa kweli naheshimu uamuzi lakini pia nafikiri Shirikisho la Soka la Cameroon kimefanya kile kilichofanya kwa kufuata sheria za Fifa na ni rahisi sana kusema hapa
"Lakini tatizo hilo sasa limetatuliwa, kwangu hakuna tatizo zaidi nab ado nina tumaini kama nilivyofanya tangu nilipokuwa kocha wa Cameroon, atakuja na kucheza nasi tena.

Matip hajaichezea Cameroon tangu mwaka 2015 na hajakuwemo katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya mashindano hayo.
Cameroon inaongoza katika Kundi A na ilikuwa ikihitaji pointi moja kutoka katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya wenyeji Gabon jana ili kufuzu kwa robo fainali.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment