MALABA, Equatorial Guinea
KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana ya Black Stars Avram Grant (pichani) analitaka
Shirikisho la Soka la Afrika kumfungia kipa wa Guinea Naby Yattara.
Kipa huyo anayecheza soka Ufaransa alipewa onyo Jumapili katika
mchezo war obo fainali wa Mataifa ya Afrika (Afcon) walipocheza na Ghana wakati
alipomrukia mshambuliaji Asamoah Gyan katika kipindi cha mwisho kabisa cha
mchezo huo.
"Wakati matokeo yakiwa ni 3-0 na tulikuwa katika dakika za
mwisho kabisa za mchezo, faulo ile ilionesha kutokuwa na nidhamu. Sifikiri kama
atacheza soka tena kwa sabbau kama unataka kuwaondoa mchezoni wachezaji, watu
wanatakiwa kufikiriakuhusu hilo…
"Nafikiri anatakiwa kufungiwa maisha yote. Hatakiwi kucheza
soka kwa sababu alijaribu kumuumisha Mghana Gyan. Alifanya kosa lile kwa
makusudi kabisa katika neo la tumbo la mwenzake."
Kocha huyo Muisraeli alifananisha faulo hiyo na ile iliyofanywa na
kipa wa Ujerumani Holord `Toni’ Schumacher
alipomchezea vibaya mchezaji wa Ufaransa Patrick
Battison.
"lakini hii ni mbaya zaidi, " alisema Grant aliyewahi
kuwa kocha wa Chelsea ya England.
Gyan alipandishwa ndege kwenda Mongomo Kaskazini ya Equatorial
Guinea kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya scan wakati Ghana ilipoanza mazoezi
jijini Malabo bila ya nahodha wao huo kwa ajili ya kuwakabiri wenyeji katika
mchezo wa nusu fainali kesho.
No comments:
Post a Comment