*Alikuwa akiandaa maandamano makubwa kumpinga Rais Putin
MOSCOW, Russia
MAELFU ya watu
wanatarajia kushiriki katika maandamano makubwa katika mitaa ya jiji hili kuonesha
heshima kwa mwanasiasa wa upinzani Boris Nemtsov, aliyeuawa kwa kupigwa risasi
Ijumaa.
Mwanasiasa huo
Jumapili alitarajia kuongoza maandamano makubwa, lakini wafuasi wake sasa
watatumia maandamano hayo kwa ajili ya kuomboleza kifo chake.
Rais wa Russia Vladimir
Putin amelaani mauaji ya Bwana Nemtsov na kuahidi kuwa, Serikali yake itahakikisha
wauaji wanapatikana.
Mauaji ya Bwana Nemtsov
yanahusishwa na masuala ya kisiasa hasa kutokana na kumpinga Bwana Putin na
ugomvi na Ukraine.
Wafuasi wa
upinzani wanatarajia kuandamana Jumapili mchana katikati ya jiji la Moscow
kabla ya kuelekea huko Great Moskvoretsky Bridge,ambako Bwana Nemtsov aliuawa.
Mamlaka ya jiji la
Moscow awali waliidhinisha kuwa hadi watu 50,000 watashiriki katika maandamano
hayo lakini waandaaji walisema kuwa watu zaidi wanawea kushiriki kushiriki
kutokana na mauaji hayo.
Sarah Rainsford anasema
kuwa mauaji hayo yameushtua upinzani wa Russia.
Katika eneo
alilopigiwa risasi mpinzani huyo kumuwekwa lundo la mashada ya maua.
Watu wengi
wanasema kuwa mauaji ya Boris Nemtsov yamefanyika kwa sababu za mtazamo wake
kisiasa na wamemlamu rais Putin kwa tabia yake ya kupinga upinzani.
Nemtsov alizaliwa
Oktoba 9 mwaka 1959 ni mwanasayansi na mwanasiasa na
alifanikiwa sana kisiasa chini ya rais Boris Yeltsin katika
miaka ya 1990, na tangu mwaka 2000 alikuwa akimkosoa Vladimir Putin.
Wakati akiuawa, Nemtsov
alikuwa jijini Moscow akisaidia maandalizi ya mkutano wake mkubwa kwa ajili ya
kupinga sera za rais Putin za kuiingiza Russia katika vita huko Ukraine na nchi
hiyo kuwa katika matatizo ya fedha.
No comments:
Post a Comment