Friday 20 February 2015



 
 
Kocha wazamani wa Burkina Faso Paul Pt.
OUAGADOUGOU, Burkina Faso
KOCHA wazamani wa Burkina Faso Paul Put ni miongoni mwa majina yaliyotajwa kwa ajili ya kutaka kuifundisha timu ya taifa ya Senegali, ambaye atatangazwa Machi 5 mwaka huu.

Wengi wa makocha hao wenye kuwania kibarua hicho ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya kungatuka kwa Alain Giresse baada ya timu hiyo kufanya vibaya katika fainali za Mataifa ya Afrika.

Rais wa Shirikisho la Soka la Senegal Augustin Senghor alisema makocha kibao, wengi wao wakiwa kutoka Ulaya, wameomba kibarua hicho.
"Hatukujibana wenyewe, hivyo kocha mpya anaweza kuwa Msenegal au mgeni, " alisema.

Mbelgiji huyo aliifundisha Burkina Faso kwa takribani miaka mitatu na kuongoza timu hiyo hadi katika fainali za Mataifa wa Afrika za mwaka 2013, lakini alichemsha katika fainali zilizopita zilizofanyika Guinea ya Ikweta.

Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi baada ya kumaliza ya mwisho katika kundi lake.

Kocha mwingine wazamani wa Burkina Faso Paulo Duarte ni mwingine ambaye anawania kiti hicho cha kuifundisha Senegal, pamoja na kocha wazamani wa Guinea Michel Dussuyer na Patrice Neveu.

Majina mengine yliyomo katika orodha hiyo ni pamoja na Wafaransa Jose Anigo, Frederic Antonetti, Luiz Fernandez na Jean-Pierre Papin, pamoja na Michel Pont kutoka Uswisi.

Amara Traore, ambaye aliifundisha timu hiyo inayojulikana kama Simba wa Teranga kati ya mwaka 2009 na 2012, anaongoza majina ya makocha wa nyumbani katika orodha hiyo, akiwemo nahodha wazamani wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 na kocha wasasa wa timu hiyo Aliou Cisse, Lamine Dieng na  Oumar Diop.

Aliou Cisse, aliyeichezea timu ya Uingereza ya Birmingham City na Portsmouth kati ya mwaka 2002 na 2006, ameonesha nia yake ya kutaka kuifundisha timu hiyo iliyofikia robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2002.
Senegal ilishindwa kufuzu kuvuka hatua ya makundi ya fainali za Mataifa ya Afrika zilizofanyika Guinea ya Ikweta.

No comments:

Post a Comment