Saturday 21 February 2015

Mo Farah avunja rekodi ya dunia




Mo Farah.
LONDON, England
MWANARIADHA Muingereza Mo Farah amevunja rekodi ya dunia yam bio za ndani za maili mbili katika mbio za Birmingham Indoor Grand Prix.
Farah, 31, aliondoka uwanjani baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia dakika 3.40 akiivunja rekodi iliyotanguliwa iliyowekwa na Muethiopia Kenenisa Bekele.
Hiyo ni rekodi ya kwanza kuwekwa na mwanariadha huyo bingwa mara mbili wa Olimpiki.
"Hii ina maana kubwa kwangu, " alisema Farah. "Napenda kuliwakilisha taifa langu, kutoa kitu fulani kwa watu wote. Siamini. "
Maandalizi ya kabla ya kuanza kwa mbio hizo za Jumamosi yalitawaliwa na malumbano dhidi ya mchezaji mwenzake Muingereza Andy Vernon.

Farah alidai kuwa Vernon alihoji uraia wake baada ya bingwa huy mara mbili wa Olimpiki kushinda mbio za Ulaya za mita 10,000 mwaka 2014, huku Vernon akielezea kuwa huo ulikuwa ni upotoshaji mkubwa.
Pamoja na suala hilo lakini Farah hakutetereka kwani alitawala mbio hizo zilizofanyika jijini Birmingham, na kuwaacha Mkenya Paul Koech na Mmarekani Bernard Lagat na kushinda mbio hizo.
"Ni (malumbano na Vernon) ndio yaliyonihamasisha mimi, nilitaka kufanya hivyo, " alisema Farah.

No comments:

Post a Comment