*Ni wakali Al Merreikh ya Sudan
KIKOSI CHA Al Merreikh ya Sudan |
Na Seba Nyanga
TIMU ya Al Merreikh ya Sudan Alhamisi Februari 12 inatarajia kutua
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza na mabingwa wa Tanzania Bara Azam FC
katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Mchezo huo utafanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja unaomilikiwa
na mabingwa hao wa Bara wa Azam Complex uliopo Chamazi Mbagala.
Ofisa Habari wa Azam FC Jaffar Idd, alisema kuwa baada ya kuwasiri,
miambao ambao ni mabingwa wa Kombe la Kagame watakutana na waandishi wa habari
katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Azam FC wanaikumbuka Al Merreikh kwani walipokutana nao katika
robo fainali ya Kombe la kagame huko Rwanda, matajiri hao wa azam walipokea
kichapo na kutolewa kwa penati.
Idd alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanaenda vizuri na timu
hiyo kesho Jumatano itacheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Azam FC walifungashwa virago na
Mtibwa Sugar katika michuano ya Kombe la Mapinduzi huko kisiwani Zanzibar,
hivyo Azam watataka kulipa kisasi katika mchezo huo wa kesho.
Vijana hao wa Azam FC ndio kwanza wamerejea nchini wakitokea
Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC), ambako walijichimbia kwa siku kadhaa wakichza
mechi mbalimbali ya kimataifa za kirafiki.
No comments:
Post a Comment